GuidePedia

0

Afisa uhamiaji Mkoa wa Mbeya Wilson Bambaganya akiwa studio za Radio bomba fm pamoja na mtangazaji wa kituo hicho na mwandishi wa habari Martha Haule katika kipindi cha Amka bomba.

Afisa huyo akiwa studio humo akiendelea kutoa mada hiyo

Afisa bado akiwa studio za Bomba fm na watangazaji hapa yupo na mtangazaji na mwandishi wa habari wa Bomba fm, ambae pia ni mmiliki wa blog hii ya Lumemo anaitwa Maiko Ngalya.






Wakazi wa mkoa wa Mbeya wametakiwa kutoa ushirikiano katika ofisi za uhamiaji zilizopo sehemu mbali mbali katika mkoa huo kwa lengo la kuwabaini wahamiaji haramu wanaoingia katika mkoa wa mbeya.

Wito huo umetolewa na Naibu kamishna na Afisa uhamiaji nmkoa wa Mbeya Wilson Bambaganya alipokuwa akiongea na Radio Bomba fm katika kipindi cha Amka Bomba kinachoruka kila siku ya jumatatu mpaka ijumaa kuanzia saa kumi na mbili asubuhi mpaka saa nne.

Bambaganya amesema moja kati ya sababu ya ongezeko la wahamiaji haramu ni wananchi kutokuwa na ushirikiano na maafisa uhamiaji waliopo karibu nao.

Aidha amesema kwa kipindi cha mwaka 2013 wamefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 383 na kufanya mikakati ya kuwarudisha makwao.

Amesema kumekuwa na tabia kwa baadhi ya wananchi ya kutotoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama kwasababu ya kudanganywa na wahamiaji hao kwa kiasi Fulani cha fedha ili wananchi wasiwezekutoa taarifa katika vyombo husika.

Bambaganya amesema vitendo vya kuwaacha wahamiaji haramu kuishi nchini bila utaratibu, vinamadhara makubwa yakiwemo ya wizi wa vitu mbali mbali na kuwa na taifa lenye mchanganyika wa watu wamataifa mbali mbali.

Hata hivyo Bambaganya amesema kwasasa wameanza kuweka maafisa uhamiaji kila kata katika mkoa huo ili kuleta uraisi wa utoaji wa huduma hiyo pindi wahamiaji hao wanapokuwepo.

                                      Na, Lumemo Blog







Post a Comment

 
Top