GuidePedia

0


TIMU ya Taifa ya Tanzania (TAIFA STARS) imeweka kambi wilayani Rungwe mkoani Mbeya  ikiwa na wachezaji 33 chipukizi ambao wanafanya mazoezi kwenye uwanja wa shule ya sekondari ya Msasani chini ya kocha Oscar Koroso kwa lengo la kupata timu imara itakayoiwakirishi nchi katika mashindano ya kimataifa.

Akizungumza na waandishi wa habari katika kambi hiyo iliyowekwe kwenye Hotel ya Landmark  meneja wa timu hiyo Bonifas Clemens alisema kuwa timu hiyo imeweka kambi wilayani humo wiki iliyopita na itakuwepo kwa siku 60 ikiwa na wachezaji 33 makocha 3 kati yao mmoja ni wa makipa,daktari 1 na meneja 1.

Alisema wachezaji hao watachujwa na kubakia 15 ambao wataungana na wachezaji 15 ambao hawajawahi kuchezea Taifa stars ambao watachambuliwa tena na kubakia 15 watakaoungana na kocha mkuu wa timu ya Taifa Stars ambaye atawaita wachezaji wa timu hiyo watakaoungana na wachezaji 15 watakaoshaguliwa.

Clemens aliongeza kuwa wachezaji ambao hawatachaguliwa wataingizwa kwenye kumbukumbu ya Taifa kwa ajili ya kuongezwa pindi timu hiyo itakapohitaji kuongeza wachezaji.

Naye kocha mteule wa Timu hiyo Oscar Koroso alisema kuwa Chama cha Mpira wa miguu Nchini (TFF) kimeandaa mpango huu chini ya udhamini wa Bia ya          Kilimanjaro kwa lengo la kupata timu nzuri ya Taifa itakayoweza kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya kimataifa na kuondokana na ukichwa cha mwandawazimu.

Koroso ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha makocha wa mpira wa miguu nchini (TAFCA) aliendelea kusema kuwa mpango huu utaweza kuleta mapinduzi ya mpira wa miguu hapa nchini na kuwa kinachotakiwa ni watanzania kuwa na subira kwani mpango wa TFF unatija ndani yake.

Alisema kuwa wamechagua wilaya hiyo kwa ajili ya kuweka kambi kutokana na hali ya hewa kuwa nzuri na watakuwepo kwa muda wa siku 60 na kwamba siku ya tarehe 4/05/2014 kutafanyika mchezo wa kujipima nguvu unaotambulika na FIFA kati yao na  timu ya Taifa ya Malawi kwenye dimba la Sokoine na mwisho wa programmer hii ya siku 60 kutafanyika mchezo wa ujirani mwema kati yao na Timu ya Taifa ya Burundi kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es Saalam.

Koroso aliongeza kuwa hali ya mazoezi inaendelea vizuri huku wachezaji wakiwa na mudi na mazoezi hali ambayo inawapa hamasa wao kama waalimu kuwapa mazoezi kwa utaratibu mzuri na kwamba katika wiki la kwanza aliwapa mazoezi magumu na wiki hili la pili wanafanya mazoezi mepesa ya kucheza mpira kwa makundi.

Aliongheza kuwa changamoto kubwa inayo wakabiri katika mpango huo ni hali mbaya ya miundombinu ya barabara ya kutoka kambini hadi kwenye Msasani ulipo uwaja huo ambapo gari la wachezaji limekuwa likikwama mara kwa mara na kuleta usumbufu mkubwa,mvua zinazoendelea kunyesha wilayani humo imekuwa ni maja ya changamoto lakini mambo yanaendelea vizuri.

Katibu wa chama cha mpira wa miguu (RUFA)wilayani humo Joel Mpanda na mwenyekiti Frankylin Mwaisobo waliipongeza TFF kuandaa mpango huo utakaoweza kuongeza tija kwa timu ya Taifa katika mashindano ya kimataifa na kuondokana na usindikizaji katika mashindano.

Mkuu wa wilaya hiyo Chrispin Meela alisema kuwa ujio wa timu hiyo ya Taifa kuweka kambi katika wilaya ya Rungwe kumeleta chachu kubwa kwa vijana kuhamasika kutaka kuupenda mchezo huo na kuwa hali ya uchumi utapanda kutokana na timu hiyo kununua mahitaji mbalimbali yanayouzwa kwa wafanya biashara ambao wataongeza pato lao na wilaya kwa ujumla.

Alisema kuwa kamati yake ya ulinzi na usalama imeboresha ulinzi katika hotel hiyo kwa lengo la kujihami na hali ya uvunjifu wa amani unaoweza kujitokeza.

                                     Na, Lumemo blog

Post a Comment

 
Top