Kamanda wa UVCCM wilaya Mbarali Ibrahim Mwakabwanga aliyeshika karatasi akimuapisha kamanda wa kata ya mahango Brown Mwakibete aliyevaa suti nyeusi.
Baadhi ya viongozi wa UVCCM wakiwapatia kadi za chama hicho vijana mara baada ya kumuapisha kamanda wa kata ya mahango Brown Mwakibete katika kijiji cha Ilongo.
Baadhi ya vijana waliyokuchukua kadi wakinyoosha mikono juu kwaajili ya kula kiapo cha chama hicho.
Kamanda wa UVCCM kata ya kongolo Mickdad Mwazembe aliyevaa taji akiapishwa akiwa na mke wake pembeni.
Kamanda Mwazembe akisema maneno machache baada ya kuapishwa.
Vijana wa umoja wa chama cha mapinduzi (UVCCM) wilaya mbarali wametakiwa kujitokeza katika kugombea nasafi mbali mbali za chama hicho pindi zinapotokea.
Hayo yamesemwa na kamanda wa umoja wa vijana wa chama cha
mapinduzi UVCCM wilaya mbarali Ibrahim Mwakabwanga alipokuwa akiwasimika
makamanda wa umoja huo katika kata za mahango na kongolo mswiswi.
Kamanda mwakabwanga amesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya
vijana kusita kugombea nafasi mbali mbali katika chama hicho kwa kile
kinachodaiwa kuwa ni uwonga na kutojiamini.
Aidha amewakikishia wazee ambao wamemaliza muda wao wa
kukitumikia chama hicho kuwa watafanya jitihada za kukiimarisha chama na kuleta
maendeleo ya jamii.
Mwakabwanga ameongeza kuwa anaimani na makamanda
aliyowaapisha katika utendaji kazi wao hivyo kutokana na kazi zao wanazozifanya
itakuwa ni jambo jepesi la kuleta maendeleo ya vijana katika kata hizo.
Makamanda waliyoapishwa ni Brown Mwakibete wa kata ya Mahango
ambae pia ni diwani wa kata hiyo na Mickdad Mwazembe wa kata ya kongolo mswiswi.
Hata hivyo makamanda hao wamesema wafurahishwa sana na tukio
hilo la kuapishwa na kuahidi watafanya kazi hiyo kwakushirikiana na vijana
wenzao kwa umakini na kwa uadilifu kulingana na kiapo walichokula.
Katika ziara hiyo ya kuwaapisha makamanda chama hicho pia
kinafanya kazi ya kuwaamasisha vijana kujiunga na chama pamoja na kugawa kadi
kwa vijana ambao wameridhia kujiunga na chama hicho.
Kwa upande wao vijana waliyochukua kadi za chama wapatao saba
wamesema ni jambo ambalo limeleta furaha kubwa kwao kwakujiunga na chama hicho
rasmi na kuwa wanachama wakamilifu hivyo waliwashauri vijana wenzao kujiunga na
chama.
Mbali na shughuli hizo kazi nyingine ambayo chama hicho
ilikuwa ikiifanya ni kuwapatia vyombo vya mgahawa vijana wa chama hicho
kwaajili ya kufungua biashara ya mgahawa.
Miongoni mwa vyombo ambavyo walivyokuwa wakiwapatia ni chupa
za chai, vikombe, sahani, vijiko na bakuli.
Na, Lumemo blog.
Post a Comment
Post a Comment