GuidePedia

0

Mkuu wa Wilaya ya Momba Mh, Abiud  Saidea akisoma hotuba yake katika warsha hiyo.

Kaimu Meneja wa TFDA kanda ya nyanda za juu kusini Rodney Alananga akiwatambulisha wageni waalikwa.


                        Baadhi ya vipodozi vilivyopigwamarufuku

Mwandishi wa Radio Mbeya Highlands fm James John  (  JJ  ) aliyevaa Phone akirusha warsha hiyo LIVE




Wakazi wa mikoa ya nyanda za juu kusini wametakiwa kuepuka vipodozi na vyakula vilivyopigwa marufuku ili kulinda afya zao.
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya momba Mh, Abiud Saidea katika warsha ya kuelimisha jamii kuhusu vyakula na vipodozi vilivyopigwa marufuku.

Warsha hiyo iliandaliwa na mamlaka ya chakula na dawa kanda ya nyanda za juu kusini na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali kutoka makao makuu ya mamlaka hiyo jijini Dar es salaam pamoja na viongozi kutoka serikalini.

Saidea ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika warsha hiyo ameongeza kuwa kunaumuhimu wa mwananchi kuhakikisha kutotumia vipodozi hivyo na kumuelimisha mwingine kuhusu madhara yanayotokana na vipodozi hivyo.

Kwa upande wake kaimu meneja wa mamlaka ya chakula na dawa kanda hiyo Rodiney Alananga amesema mamlaka hiyo imeamua kutoa elimu kwa jamii pamoja na wafanyabiashara kuhusu madhara ya vipodozi hivyo sambamba na kuwaonesha vipodozi ambavyo wasivyovifahamu ili wananchi hao waweze kujilinda wenyewe badala ya kutumia nguvu ya kisheria.

Aidha amesema sheria zipo ambazozinaweza kutumika kwa lengo la kudhibiti vipodozi hivyo, isipokua mamlaka imeona si vyema kuchukua hatua hiyo kabla ya kutoa elimu ya kutosha kwa wafanyabiashara na jamii kwa ujumla.

Alananga amesema baada ya kutoa elimu hiyo anamani kuwa kila mwanachi aliyefika katika warsha hiyo atakuwa ameelimika vyakutosha hivyo atakama mamlaka hiyo ikichukua hatua ya kisheria hakutakuwa na lawama kwa jamii kutokana na elimu waliyoitoa.

Hata hivyo wananchi waliyohudhuria warsha hiyo wamesema wamefurahishwa na elimu waliyopatiwa kwani wengi wao hawakuwa na elimu hivyo kusababisha kutumia bidhaa pasipo kujua madhara yake.

Hivyo wameiomba mamlaka hiyo kuendelee kutoa elimu hiyo mara kwa mara ili kuwanusulu na madhara yatokanayo na vipodozi na vyakula ambavyo si sahihi.

                                              Na, Lumemo blog




Post a Comment

 
Top