Afisa uhamiaji Mkoa wa Mbeya Wilson Bambaganya akiwa studio za Radio bomba fm pamoja na mtangazaji wa kituo hicho na mwandishi wa habari Martha Haule katika kipindi cha Amka bomba.
Afisa huyo akiwa studio humo akiendelea kutoa mada hiyo
Afisa bado akiwa studio za Bomba fm na watangazaji hapa yupo na mtangazaji na mwandishi wa habari wa Bomba fm, ambae pia ni mmiliki wa blog hii ya Lumemo anaitwa Maiko Ngalya.
Wakazi
wa mkoa wa Mbeya wametakiwa kutoa ushirikiano katika ofisi za uhamiaji zilizopo
sehemu mbali mbali katika mkoa huo kwa lengo la kuwabaini wahamiaji haramu
wanaoingia katika mkoa wa mbeya.
Wito
huo umetolewa na Naibu kamishna na Afisa uhamiaji nmkoa wa Mbeya Wilson
Bambaganya alipokuwa akiongea na Radio Bomba fm katika kipindi cha Amka Bomba
kinachoruka kila siku ya jumatatu mpaka ijumaa kuanzia saa kumi na mbili
asubuhi mpaka saa nne.
Bambaganya
amesema moja kati ya sababu ya ongezeko la wahamiaji haramu ni wananchi
kutokuwa na ushirikiano na maafisa uhamiaji waliopo karibu nao.
Aidha
amesema kwa kipindi cha mwaka 2013 wamefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 383
na kufanya mikakati ya kuwarudisha makwao.
Amesema
kumekuwa na tabia kwa baadhi ya wananchi ya kutotoa taarifa kwa vyombo vya
ulinzi na usalama kwasababu ya kudanganywa na wahamiaji hao kwa kiasi Fulani cha
fedha ili wananchi wasiwezekutoa taarifa katika vyombo husika.
Bambaganya
amesema vitendo vya kuwaacha wahamiaji haramu kuishi nchini bila utaratibu,
vinamadhara makubwa yakiwemo ya wizi wa vitu mbali mbali na kuwa na taifa lenye
mchanganyika wa watu wamataifa mbali mbali.
Hata
hivyo Bambaganya amesema kwasasa wameanza kuweka maafisa uhamiaji kila kata
katika mkoa huo ili kuleta uraisi wa utoaji wa huduma hiyo pindi wahamiaji hao
wanapokuwepo.
Na, Lumemo Blog
Na, Lumemo Blog
Post a Comment
Post a Comment