MWALIMU wa shule ya msingi Katani wilayani Nkasi
mkoani Rukwa Ringtone Rayson (36)amehukumiwa kwenda kutumikia kifungo cha
miaka miwili jela au kulipa faini ya Tshs,100,000 kwa kosa la kufumaniwa na mke
wa mtu Beata sangu (31) na kumjeruhi mme wa mwanamke huyo kwa mapanga na
msumeno iliyokuwemo ndani ya nyumba hiyo
Kwa
mujibu wa maelezo yaliyotolewa mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya
wilaya Nkasi Ramadhani Rugemalila mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi
Hamimu
Gwelo alisema kuwa mtuhumiwa mnamo oktoba 12 mwaka jana majira ya saa 3
usiku mme wa mwanamke huyo alipata taarifa kutoka kwa msiri wake kuwa
mwalimu huyo aliingia ndani ya nyumba yake na kufanya mapenzi na mkewe wakati
yeye alipokuwa amekwenda kulala kwa mke mdogo
Alisema
kuwa mme wa mwanamke huyo Richard Feruzi (33) baada ya kupata taarifa hizo
alikwenda kumtafuta mdogo wake Stanslaus Feruzi na viongozi wa mtaa ule
kwa lengo la kwenda kumfumania mwalimu huyo na baada ya wote kufika katika
nyumba ile walipiga hodi lakini hawakufungua na ndipo walipoanza kuvunja mlango
ili waweze kumkamata mtuhumiwa aliyekuwa katika nyumba hiyo
Mwendesha
mashitaka huyo wa jeshi la polisi aliifafanulia mahakama hiyo kuwa wakati
mlango ule ulipokuwa ukivunjwa mtuhumiwa ambaye ni mwalimu aliamua kuchukua
panga na msumeno vilivyokuwamo katika nyumba hiyo na kuamua kutoka na kuanza
kuwashambulia kwa mapanga mme wa mwanamke huyo Richard Feruzi na mdogo wake
Stanslaus Feruzi na kuwapatia majeraha makali na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu
Baada
ya mtuhumiwa kukiri kutenda kosa hilo mahakama hiyo ilimuadhibu mtuhumiwa
kwenda jela miaka miwili au kulipa faini ya Tshs,100,000 na fidia ya
Tshs,150,000 kwa kila majeruhi kati ya wale wawili mme na mdogo wa mme kutokana
na majeraha waliyoyapata
Hakimu
wa mahakama hiyo Bw,Rugemalila alisema kuwa mtuhumiwa alitiwa hatiani chini ya
kifungu No,225 sura ya 16 ya kanuni ya adhabu
Mtuhumiwa
baada ya kutiwa hatiani na mahakama hiyo alilipa faini ya Tshs,100,000 na fidia
zote na jumla ya Tshs,400,000 zilitolewa katika mahakama hiyo na kuachiwa huru
Na, Lumemo blog
Post a Comment
Post a Comment