GuidePedia

0

Mwenyekiti wa kamati ya uchangiaji  Mr, Olaisi Oleseenga aliyesimama, upande wake wa kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh, Abas Kandoro ambae pia ndio alikuwa mgeni rasmi wa hafla hiyo.


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh, Abas Kandoro alipokuwa anajibu risala ya kamati hiyo ya uchangiaji.

Baadhi ya waratibu wa kamati ya uchangiaji wakipeana mkono na Mkuu wa Mkua wa mbeya.

Mkuu wa wilaya ya momba Mh, Abiudi Saideya akieleza jinsi alivyoguswa na jambo hilo

Mkurugenzi wa mawasiliano katika kamati ya uchangishaji, AWARD MPANDILAH akieleza kufurahishwa na kitendo cha kushikana mkono na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh, Abas Kandoro.





Serikali mkoani Mbeya  imewataka  wananchi na  wadau mbali mbali wa afya  kuwa  na mwitikio mkubwa, pindi wanapo takiwa kuchangia michango katika sekta ya afya.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa mbeya Mh, Abasi Kandoro alipokuwa katika harambee ya ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika Hospitali ya mkoa wa Mbeya uliyofanyika juzi katika ukumbi wa mkapa jijini humo.

Katika harambee hiyo iliyofanikiwa kupata kiasi cha fwedha zaidi ya milioni thelathini na nane 38 keshi na ahadi ni shilingi milion arobaini na mbili 42.

Kandoro amesema sekta ya afya inamgusa kila mtu kwa nafasi yake maana hakuna binadamu anyeishi bila kuugua hivyo tunakila sababu ya mwananchi anyeishi mkoa wa mbeya na hata hule anaeishi inje ya mloa huo ili hali tu ana familia katika mkioa wa mbeya anawajibu wakuchangia katika sekta hiyo.

Aidha mkuu wa mkoa huyo amewapongeza waratibu wa kamati ya harambee ya ujenzi huo kwa kuonesha jitiada za dhati mpaka katika hatua waliyofikia wa shughuli hiyo.

Hata hivyo Kandoro alisema kumekuwa na tabia ya baadhi ya wananchi ya kuchangia masherehe mbali mbali ambayo yanagharama kubwa kuliko kuchangia kiasi Fulani cha fedha katika mambo ya kijamii kama hayo.


                                  Na, Lumemo blog







Post a Comment

 
Top