Serikali kupitia idara ya afya katika
Halmashauri ya Busokelo wilayani Rungwe mkoani Mbeya
imetoa kiasi ya cha sh. 4000000/= kwa
ajili ya ujezi wa zahanati ya Matamba ambayo inaendelea
kujengwa kwa nguvu za wananchi.
Akizungumza na mwandishi wetu mganga
mkuu wa Harimashauri ya wilaya ya Busokelo wilayani humo
Gibert Tarimo alisema kutokana na
wananchi wa kijiji hicho kuonyesha moyo
katika ujenzi wa zahanati yao baada ya kusumbuka
kwa muda mrefu katika kutafuta huduma
ya matibabu, serikali kupitia bidala hiyo
imetoa shiringi milioni nne kwa
ajili ya kusadia kumalizia ujenzi
wa zahanati hiyo.
“ Serikali kupitia idara ya
afya iliona ni vyema ikashirikiana na wananchi wa
kijiji hiki katika ujenzi wa kituo chao cha afya kwakuwapatia
msaada wa pesa kiasi cha shilingi milioni nne
ambazo zitatumika kumalizia ujenzi wa zahanati hii
Adha Tarimo aliwataka wanachi kuendelea na
moyo huo na kusema kufanikisha kwa
kazi hiyo kuta tegemea na uelekezi wa nguvu zao
katika ujenzi wa zahanati hiyo.
Jampyoni mbuguru ambaye ni
mwanachi wa kijiji hicho mbali na kuupongeza uongozi huo
kwa jitihada walizo zionesha alisema uwepo wa kituo hicho utasaidia
wao kupunguza vifo vya watoto na ndugu zao
ambao walikuwa wakipatwa na maafa wakati wa kuwakimbiza
katika vituo vya afya .
“
sisi kama wananchi tuliamua kuanza ujenzi wa kituo hiki
baada ya kutembea umbali mrefu katika kutafuta huduma
muhimu ya afya ambayo inapatika zaidi ya
kilometa {7} na kusema wakati mwingine ndugu zetu
wamekuwa wakifia njiani pindi tunapowapeleka katika
vituo hivyo kwa matibabu zaidi na ukizingatia kuwa
katika maeneo haya hakuna usafiri zaidi ya baisikeli”.
alisema Mbunguru.
Mwenyekiti wa kijiji
hicho Johan mwakyoma kwa upande wake
alisema katika kukamilisha hatua hiyo
walijipangia kutoa kiasi cha shiringi elfu thelatini
kwa kila mmoja 30000/= ambazo wanazitoa kwa
awamu sita na kusema mpaka sasa wamemaliza hatua
ya linta na wamenza ufyatuaji wa tofari na
kuwalipa mafundi.
Na, Baraka lusajo Rungwe
Post a Comment
Post a Comment