Baba mzazi wa mtoto John akiwa amekaa na mwanae mara tu baada ya hukumu kutolewa
MWANAMKE Mwanahawa Nassoro(32) Mkazi wa
Mtaa wa Airport jijini Mbeya amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka mitatu
jela baada ya kupatikana na hatia ya kunyanyasa na kumtesa mtoto.
Mwanamke huyo alipandishwa katika
Mahakama ya Mwanzo ya Mbeya mjini juzi kutokana na kosa lililokuwa likimkabili
la kumtesa mtoto John Paul(03) ambaye ni mtoto wa kaka yake.
Akisoma mashitaka mbele ya Hakimu wa
Mahakama ya Mwanzo Mbeya mjini, Salome Mwakyosi, mwendesha mashitaka wa Polisi
Kopro Anthon alisema mtuhumiwa alitenda kosa hilo Machi 12, Mwaka huu kwa
nyakati tofauti kwa kumfungia ndani na kumnyima chakula kinyume cha sheria
namba 241 ya makosa ya jinai sura ya 16 ya kanuni ya adhabu iliyofanyiwa
marekebisho mwaka 2002.
Alisema Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa
Airport, Rehema Mohammed ndiye aliyebaini na kutoa taarifa kwenye uongozi wa
Mtaa ambapo mtuhumiwa alikamatwa na hatimaye kufikishwa katika kituo cha Polisi
kwa ajili ya hutua za kisheria.
Upande wa Mashitaka ulikuwa na mashahidi
wane, ambapo wawili kati yao ndiyo waliotoa ushahidi ambao ni pamoja na
Mjumbe wa Serikali ya Mtaa na Mtoto aliyefanyiwa ukatili huo ambaye alimtambua
mahakamani Shangazi yake Mwanahawa licha ya kuwepo watu wengi.
Mtoto huyo alifika mahakamani kutoa
ushahidi baada ya afya yake kuimarika kutokana na kupatiwa matibabu katika
Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.
Hakimu alipomuuliza mtoto kuhusu
mtu aliyekuwa akimpiga alimuonesha Mwanahawa mara tatu ambapo alizidi kumuonesha
Shangaza yake huyo.
Kwa upande wake mtuhumiwa wa kesi hiyo
alipoulizwa kuhusiana na kosa hilo alikiri ambapo Hakimu aliridhika na ushahidi
uliotolewa na pande zote mbili ikiwa ni pamoja na kukiri kwa mtuhumiwa.
Kutokana na ushahidi huo Mahakama hiyo
na ilimtia hatiani mshitakiwa kwa kumuadhibu kutumikia kifungo cha miaka
mitatu jela ili iwe fundisho kwa watu wanaofanya vitendo vya kikatili dhidi ya
watoto.
|
Post a Comment
Post a Comment