Mkaguzi mkuu wa Osha Tanzania bara Dr, Akwilina Kayumba na Meneja wa Osha kanda ya nyanda za juu kusi Eng, George Chali wakiwa studio za Radio Bomba fm na mtangazaji na mwandishi wa habari wa bomba fm Martha Haule katika kipindi cha Amka Bomba kinachoruka asubuhi kuanzia saa kumi na mbili na nusu mpaka saa nne.
Dr, Kayumba na Eng, George wakiendelea kutoa mada katika Studio za Bomba fm Mbeya.
Wamiliki wa makampuni na mashirika binafsi mkoani Mbeya
wametakiwa kujisajiri kwa wakala wa afya
na usalama mahali pa kazi kutoka katika ofisi ya Wizara ya afya, Occupational Safety and
Health Authority (OSHA).
Kauli hiyo imetolewa na mkaguzi mkuu wa OSHA Tanzania bara
Dr, Akwilina Kayumba alipokuwa akiongea na katika kituo cha Radio Bomba fm
katika kipindi cha Amka Bomba kinachorushwa kila siku ya jumatatu mpaka ijumaa
kuanzia saa kumi na mbili na nusu asubuhi mpaka saa nne asubuhi.
Kayumba amesema kuna makampuni mengi hayajajisajiri na osha,
ambapo si sahii kuanzisha kampuni bila pasipo kujisajiri na osha na kwakufanya
hivyo ni kutowatendea haki wafanya kazi waliopo katika makampuni hayo.
Aidha Kayumba amesema
katika kuelekea katika siku ya maazimisho ya afya na usalama mahali pa kazi
kunakila sababu ya makampuni na mashirika ambayo hayajajisajiri na osha ni
vizuri yakajisajiri ili kuleta usawa kati waajiri na waajiriwa.
Kwaupande wake Meneja wa osha kanda ya nyanda za juu kusini Eng.
George Chali amesema kuna baadhi ya wamiliki wa makapuni wamekuwa wakidhani
kusajiriwa na osha ni jambo gumu bali ni jambo jepesi na halina mzunguko
mkubwa.
Eng. Chali ameto wito kwa baadhi ya makampuni yasiyosajiriwa
kuchukua hatua ya kujisajiri sasa na kwamba siku ya jumamosi kuta kuwa na kikao
baina osha na wadau wake wakiwemo wamiliki wa makampuni na wafanyakazi wake katika
ofisi za osha jijini Mbeya kuanzia saa nne mpaka saa sita.
Hata hivyo Chali amewataka wadau wa makampuni na wafanyakazi
wake kujitokeza kwa wingi ili kuzungumza mambo mbali mbali yanayohusu afya na
usalama mahali pa kazi.
Na Lumemo blog.
Post a Comment
Post a Comment