UTUMIKISHWAJI
wa watoto walio chini ya miaka 16 limeibuka wilayani Rungwe mkoani Mbeya baada
ya wajasiliamali wanaojishughurisha na biashara ndogondogo wakiwemo wauza nyama
za kuchoma(MISHIKAKI) wanaodaiwa kwenda vijijini na kuwarubuni watoto wadogo na
kuwatumikishwa katika biashara zao na kuwapa ujira mdogo.
Lumemo Blog hii ilifanya uchunguzi wa siku tatu na kufanikiwa kuwapata watoto 15
waliochini ya miaka 16 na kufanikiwa kufanyanao mazungumzo na kubaini kuwa wapo
zaidi ya hao ambao wengi wao walihitimu darasa la saba na kuchaguliwa kujiunga
na kidato cha kwanza na kushidwa kujiunga kutokana na ukosefu wa fedha kwa wa
zazi wao.
Mtoto Bonifas
Elyud (15) mkazi wa Kasumulu Boda wilayani Kyela alisema kuwa yeye alihitimu
darasa la saba katika shule ya msingi Ruangwa na kuchaguliwa kujiunga na kidato
cha kwanza katika shule ya Kiwira Col mine (KCM) mwaka 2013 lakini alishindwa
kujiunga na masomo kutokana na wazazi wao kuishi tofauti baada ya ndoa yao
kuvunjika.
Alisema kuwa
baba yake anaishi jijini mwanza baada ya kuachana na mama yake ambaye kwa sasa
ni mremavu wa macho (Kipofu) anayeishi na dada yake maeneo ya Bujesi Kijiji cha
Ikomelo kata ya busale wilayani kyela huku yeye akiwa hana muelekeo wa maisha
pamoja na kuwa alichaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza katika
shule ya sekondari ya KCM.
Aliongeza kuwa
baada ya siku kadhaa alikuja kijana mmoja anayeitwa Jeremia Sanga mkazi wa Kata
ya Kawetele Rungwe akimuhitaji akafanye kazi ya kuuza mgahawa wake uliopo
Tukuyu mjini na kumuahidi kuwa baada ya muda atampeleka shule,lakini amemaliza
mwaka akimtumikia bosi wake huyo lakini hakuna dariri zozote za uwepo wa
kumpeleka shule huku akiendelea kutumikishwa kwa malipo ya Tsh.1000 kwa siku.
Aliendelea kusema
kuwa yeye hana mawasiliano na Baba yake lakini kama kuna msamalia mwema anataka
kumsomesha yupo tayari kuingia darasani na kuwa amekuwa hakikosa raha kutokana
na umri wake kuwa mdogo huku akifanya kazi ngumu huku watoto wenzake
wakiendelea na masomo.
Lumemo Blog hii iliutafuta uongozi wa kata hiyo ya kawetele na kufanikiwa kumpata diwani wa
kata hiyo Anyimike Mwasakilali ambaye mbali na kukiri kuwepo na hali hiyo
lakini alisikitishwa na kasi ya ongezeko la watoto hao wanaotumikishwa kinyume
na sheria huku akiahidi kufanya msaka wa nyumba hadi nyumba ili kuwabaini
watoto hao pamoja na kuwachukulia hatua wale wanaowaajiri.
Mwasakilali alisema
kuwa katika kata yake wanaoutaratibu wa kuwasajiri watoto yatima walifiwa na
wazazi wao na wale waishio katika mazingira magumu ambao wamewasajiri na
kuwapeleka shule pamoja na kuwapa huduma
kadhaa za msingi na kuwa uwepo wa watoto hao wanaotumikishwa yeye hana taarifa
nao kutokana na kuingizwa katika wilaya hiyo kwa njia za panya.
Aliongeza kuwa
kwa kushirikiana na uongozi wa kata na wilaya kwa ujumla watafanya msako
utakaoambatana na kuwachukulia hatua watu watakaobainika kuwa ndiyo
wanaowaajiri watoto hao ili iwe fundisho kwa wengine wasiokuwa na huruma kwa
watoto hao.
Uchunguzi wa
gazeti hili umebaini kuwa asilimia 80 ya watoto wanaotumikishwa wanatoka katika
kata ya Busale wilayani Kyela na tayari mawasiliano yamefanyika na uongozi wa
kata hiyo ukiongozwa na diwani wa kata hiyo Ezekia Msyani ambaye ameahidi
kuanza kulifanyia kazi tatizo hilo.
Na Lumemo blog
Post a Comment
Post a Comment