SERIKALI mkoani Rukwa imewataka wazazi
wanaowakataza vijana wao kwenda kufanyiwa tohara kwa mwanaume kuacha mara
moja kwani huduma hiyo imethibitika kitaalamu kuwa ina faida nyingi ikiwa
ni pamoja na kupunguza uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi mapya ya ukimwi
kwa asilimia 60
Wito
huo umetolewa na mkuu wa wilaya Nkasi Idd Hassan Kimanta kwenye ufunguzi wa
kampeni ya tohara kwa wanaume mkoani Rukwa iliyofanyika katika zahanati
ya Chala wilayani Nkasi ambapo alimwakilisha mkuu wa mkoa Mhandisi stella
manyanya ambapo amesema kuwa tohara ni jibu la kupambana na magonjwa
yatokanayo na ngono
Hivyo
amewataka wanaume wote ambao bado hawajajitokeza kufanyiwa tohara hiyo
kujitokeza na kuitumia fursa hiyo ambayo inapatikana bure kutokana na umuhimu
wa kiafya katika kujenga jamii iliyo salama
Pia
kimanta amefurahishwa na maendeleo yaliyopo sasa toka zoezi la tohara kuanza
katika zahanati ya chala na kwani mpaka sasa wanaume 583 wamejitokeza kufanyiwa
toharan ndani ya wiki mbili tu na kudai kuwa kasi hiyo inaleta matumaini
makubwa ukilinganisha na agizo la taifa ambalo linataka wanaume 22000 mkoani
Rukwa wawe wamefanyiwa tohara na kuwa hadi sasa ni watu 7000 tu na kuwa bado
safari ni ndefu
Mganga
mkuu wa mkoa Rukwa Dkt,John Gurisha kwa upande wake alisema tohara kwa mwanaume
inawasaidia wanandoa wote wawili kuweza kuondokana na matatizo yasiyo kuwa ya
lazima kama magonjwa ya kansa ya shingo ya kizazi kwa wanawake,uwezekano wa
kupata maambukizi ya virus vya ukimwi kupungua kwa asilimia 60 ikiwa ni pamoja
na suala la usafi kwa ujumla
Hivyo alidai kuwa hatarajii kusikia kuwa kuna baadhi
ya watu ambao watashindwa kujitokeza kufanyiwa tohara hiyo,lakini pia
alionyesha kufurahishwa na kasi ya tohara katika kituo hicho cha Chala kwa
maana kuwa kwa siku moja wanaume 150 wanafanyiwa na kuwa kasi hiyo ikiendelea
hivyo mkoa Rukwa unaweza ukafanikiwa kwa kiasi kikubwa juu ya tohara hiyo
Zoezi
hili lililoanza marchi 17 mwaka huu linatarajia kumalizika marchi 30 na mkoa
Rukwa una vituo sita vinavyotekeleza mradi huo wa tohara bure kwa mwanaume
chini ya ufadhili wa shirika lisilokuwa la kiserikali la Waterleed Tanzania na
vituo ni Chala,Korongwe,Muze,Ilemba,Kapozwa na mkowe ukiachana na vituo vitano
tofauti vinavyoendelea na utoaji wa huduma hii ya tohara ambavyo ni
Mtowisa,Matai,Nkomolo,Kirando pamoja na kituo mama cha hospitali ya mkoa
iliyopo Sumbawanga
Na, Lumemo blog
Post a Comment
Post a Comment