Wananchi wa kata zilizopo
liuli,Lupingu,Lumbila,Lifuma,Iwela na Kilondo zilizopo Tarafa ya Mwambao
wilayani Ludewa mkoa mpya wa Njombe wameilalamikia Serikali kupitia halmashauri
ya wilaya hiyo kwa kushindwa kuwaondolea kero zilizopo katika tarafa hiyo tangu
nchi ipate uhuru mwaka 1961 hadi sasa.
Wakizungumza
na Lumemo blog wananchi hao walisema kuwa vijiji vilivyopo kwenye kata
hizo vinakabiriwa na changamoto nyingi lakini viongozi wa serikali na
halmashauri wameshindwa kuondoa changamoto hizo kwa muda mrefu na kuwa
wamepeleka malalamiko yao kwa maandishi juu ya matatizo ya Tarafa hiyo lakini
hakuna kinachoendelea.
Dadi
mapunda mkazi wa kijiji cha Liunji alisema kuwa Tarafa hiyo ya mwambao
inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo ya ukosefu wa umeme,maji
safi,mawasiliano,barabara ,shule,vituo vya afya na uhaba wa watumishi ambao
wengi wao hutoroka kufanya kazi mara baada ya kuripoti kutokana na miundombinu
mibovu pamoja na ukosefu wa huduma za msingi za kijamii.
Alisema
kuwa katika suala la mawasiliano wamekuwa wakipanda juu ya miti na kupanda
kwenye mirima mirefu huku wengine wakitembea umbali mrefu kufuata huduma za
network hali ambayo inahatarisha maisha yao na kuwa watoto wao pia hutembea
umbali mrefu kwenda shule kutokana na kuwa na shule chache huku elimu katika
Tarafa hiyo ikizidi kushuka siku hadi siku.
Nyongo
Makwaya mkazi wa kijiji cha Ndowa kwa upande wake alisema kuwa Tarafa hiyo ya
mwambao imekosa huduma za vituo vya afya vilivyopo havikidhi mahitaji ya
wananchi hali inayopelekea watembee umbali mrefu wa kutumia Boti na Mitumbwi
kufuata huduma za matibabu katika hospitali ya misheni ya Matema beach na
kusababisha baadhi ya wagonjwa kufia njiani kabla hawajafika hospitali kutokana
na umbali mrefu.
Alisema
kuwa walikwisha andika barua kuiomba halmashauri juu ya kero hizo ili iweze
kutafuta tiba ya kutatua tatizo hilo lakini bado hali ni tata na kuwa kama hali
itaendelea kuwa hivyo kunauwezekano wa vijana wote ambao ndiyo nguvu kazi ya
vijiji hivyo kuyatelekeza makazi hayo na kwenda kuishi sehemu nyingine ambako
hakuna changamoto kwa lengo la kutafuta unafuu wa maisha.
Hata
hivyo baadhi ya viongozi katika Tarafa hiyo wakiongozwa na Sosten
Haule,Chrispin Mwendapole mbali na kukiri kuwepo na tatizo hilo pia walisema
kuwa serikali kupitia halmashauri ya wilaya ya Ludewa wanalijua tatizo hilo na
wanajipanga ili kujalibu kupunguza changamoto zilizopo.
Na, Lumemo blog
Post a Comment
Post a Comment