GuidePedia

0

MKUU wa Wilaya ya  Sumbawanga , Mathew Sedoyeka  amesema ni aibu kwa wakazi wa mkoa wa Rukwa kuwa na watu wadumavu wakati mkoa huo ni miongoni mwa mikoa michache nchini inayoongoza kwa uzalishaji wa mazao ya chakula hususani mahindi.

Kwa mujibu wa takwimu za sasa za Wizara ya  Afya  na Ustawi  wa Jamii mkoa wa Rukwa una nusu ya watoto wenye chini ya miaka mitano ni wadumavu kwa asilimia 50 kutokana na kukosa lishe  bora katika makuzi yao.

Pia  asilimia  22 ya akina mama wenye umri kati ya  miaka 15 hadi 49 ambao  ni umri wa uzazi  na aslimia 42 ya watoto  wenye umri wa miezi  sita  hadi miezi 59  wanakabiliwa na upungufu mkubwa  wa damu mkoani humo .

Sedoyeka  alisema hayo  jana  wakati  wa uzinduzi  wa kampeni ya uchangiaji  damu kwa hiyari  unaofanywa na  Asasi  isiyo ya Kiserikali ya Evidence  for  Action (E4A) kupitia mradi wao wa  mama ye! Iliyofanyika  katika  viwanja  vya Nelson Mandela , Manispaa ya Sumbawanga baada ya kutembelea  banda  la Shirika lisilo la Kiserikali  la Africare linalotekeleza  mradi  wake  wa wazazi  na mwana.

“Takwimu  hizi  si  nzuri hata kidogo  mie  binafsi  zimenistusha sana  ukizingatia  kuwa  mkoa  huu  ndio  unaongoza  kwa uzalizishaji  wa  chakula cha ziada   hususani nafaka ikiwemo mahindi  lakini bado  wakazi wake hususani akina mama  na  watoto  wao  wanakabiliwa  na  magonjwa  yakiwemo  udumavu na upungufu mkubwa  wa damu  kwa kiwango cha juu” alieleza

“Akina mama  wanyonyesheni watoto wenu maziwa  mpaka  wapumue  wenyewe  ili kuboresha  afya  zao  kwani maziwa  ya aina mbalimbali  za virutubisho “ alisisitiza .

 Awali  akisoma risala ,Tizowelo Mlondeya  ambaye  ni  muuguzi , Manispaa  ya Sumbawanga  alibainisha kuwa Halmshauri  ya manispaa hiyo inatumia kila mbinu  kuhakikisha huduma za  afya  ya mama na mtoto  inaimarika  kila siku  ikiwwemo  kuongeza  vitendea kazi  katika  vituo  vya  kutolea huduma ya  afya.

Mbinu zingine alizitaja   zikiwa ni pamoja  na  kuimarisha  huduma mkoba  katika maeneo  yote  ya Manispaa hiyo  pia kutoka chanjo  katika Hospitali  ya Mkoa  na  Hospitali ya Dr Atman  katika siku zote za mapumziko  na Sikukuu.

Pia  kutoa motisha  kwa wakunga  wa jadi  wanaowasindikiza  wajawazito  katika  vituo vya kutolea  huduma ya afya  pamoja  na  kuwaelimisha  jamii juu  ya afya ya mama na mtoto.

                                    Na, Lumemo blog

Post a Comment

 
Top