Mh, Philipo Mulugo Mbunge wa jimbo la songwe aliye vaa shati ya rangi ya machungwa mchanganyiko aliyesimama katikati, alipokuwa kituo cha Polisi Galula chunya akipokea matatizo ya usafiri katika kituo hicho yaliyotolewa na Askari, sangent Deograsias Fusi aliyevaa kofia,
Mh, Mulugo alipokuwa katika jengo la kituo cha Polisi kipya linalojengwa katika kijiji cha mpona na kumkabidhi fedha afande Fusi kwaajili ya kukarabati pikipiki ya kituo cha Galula shilingi laki mbili 2,00000/-
Mh, Mulugo akiwasaidia mafundi wanaojenga kituo hicho cha Polisi akichanganya mchanga na saruji
Hili ndilo jengo linalongwa kwaajili ya kituo cha Polisi katika kijiji cha mpona
Mh, Mulugo alipokuwa kijiji cha mbuyuni akiwa kabidhi fedha shilingi milioni tano vijana wajasiria mali aliyowaahidi siku chache zilizopita.
Diwani wa kaya ya Mbuyuni Daudi Mpakasi aliyesimama akisema neno la kumshukuru Mh, Philipo Mulugo kwakukamilisha ahadi yake kwa vijana.
Baadhi ya vijana pamoja na Diwani Daudi Mpakasi wakihesabu fedha baada ya kukabidhiwa na Mh, Mulugo.
Mh, Mulugo alipokuwa katika kijiji cha kanga hapo pia aliwaahidi vijana shilingi milioni mbili na akawapatia fedha hizo.
Baadhi ya wananchi wakimpokea Mbunge wao Mh, Mulugo kwa maandamano katika kijiji cha kanga.
Wakazi wa vijiji vya malangali, mpona, mbuyuni chang’ombe,
kanga na vijiji vingine vilivyopo katika jimbo la songwe lililopo wilaya ya
chunya vinatarajia kunufaika na miradi mbali mbali iliyoanzishwa na mbunge wa
jimbo hilo Mh, Philipo Mulugo.
Miradi hiyo ikiwemo ni kituo cha polisi ambacho kinajengwa
katika kijiji cha mpona, vijana wasiriamali waendesha pikipiki (bodaboda)
pamoja na vikundi vya vikoba.
Jitihada za kuanzisha kwa miradi hiyo ilianza muda mrefu
ambapo baadhi ya vikundi vimesha piga hatua ya kimaendeleo, kufuatia hali hiyo
imempamsukumo Mh, Mulugo kuwaahidi wajasiriamali hao kluwaongezea fedha za
mitaji yao.
Mh, Mulugo siku za nyuma aliwaahidi wajasiriamali hao fedha
jumla ya shilingi milioni saba 7,000,000/= katika vikundi hivyo.
Hivyo Mbunge huyo siku ya jana aliweza kukamilisha ahadi yake
katika vikundi hivyo ambapo alifika katika vijiji hivyo na kuwapatia fedha
hizo.
Mbali na ahadi hizo katiak vikundi pia Mulugo ali wapatia
fedha shilingi laki mbili 2,00000/= askari wa kituo cha polisi Galula ya
kutengeneza pikipiki iliyokuwa imeharibika na kuwaahidi kuwapatia pikipiki mpya
yenye dhamani ya shilingi million mbili na laki nne.
Post a Comment
Post a Comment