Mkuu wa mbeya Mh, Abas Kandoro akiongea neno katika hafla hiyo
Mwenyekiti wa usalama barabarani mkoa wa Mbeya ambaye pia ndio Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwaji Group iliyopo uyole jijini Mbeya Allan Mwaigaga akiongea jambo kuhusu hafla hiyo.
Mkuu wa mkoa wa mbeya Mh, Abas Kandoro na Kamanda wa Polisi Mkoa wa mbeya Ahmed Msangi wakikiwa katika moja kati ya mabasi hayo wakijaribu kukaa katika siti za mabasi hayo.
Meza kuu katika hafla hiyo kutoka kushoto wa tatu Mkuu wa mkoa wa mbeya Abas Kandoro na kutoka kulia wa kwanza kamanda wa Polisi Mkoa wa mbeya Ahmed Msang.
Hii ni sehemu ya ndani ya mabasi hayo
Moja kati ya madereva wa mabasi hayo Bi, Nusura Maguluko akiwa ndani basi.
Madereva mkoani Mbeya kujihadhari na vitendo vinavyoweza kuwapunguzia
umakini wawapo safarini ili kuepusha ajali ambazo zimekuwa zikigharimu roho za
watanzania wasiokuwa na hatia.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro wakati akizungumza kwenye hafla ya
uzinduzi wa mabasi ya kisasa ya Ndenjela Jet kuwa tabia ya ulevi, matumizi ya
simu wanapoendesha magari, mazungumzo na mwendo kasi ni vitu vinavyoweza
kumpunguzia dereva umakini awapo safarini.
Kandoro amesema
pia madereva waache kuyapita magari mengine katika maeneo yasiyoruhusiwa abiria
na wamiliki wa magari wakishirikiana wanaweza kutoa mchango mkubwa katika
kupunguza ajali nchini
Aidha Kandoro
ameongeza kuwa kumekuwapo na madai kutoka kwa madereva kwamba wanaendesha kwa
mwendokasi kutokana na kwamba wanalipwa kidogo na wamiliki wa magari sababu
ambazo si za msingi sana bali wanapaswa kuwajali abiria wanaokuwa wamewabeba na
wao wenyewe.
Kwa upande
wake Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Ahmed Msangi akizungumza katika hafla hiyo
aliwakumbusha wana Mbeya umuhimu wa kutoa ushirikiano katika kuimarisha ulinzi
ili mkoa uendelee kuwa tulivu utakaowavutia wawekezaji.
Awali
akizungumza wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi mmiliki wa mabasi hayo Allan
Mwaigaga amewaasa watanzania kutumia fursa ya mazingira yaliyopo katika
kuwekeza ili kuchangia katika kuinua uchumi wan chi kwakuwa hakuna mtu mwingine
wa kuja kuwekeza nchini bali ni watanzania wenyewe.
Ameseongeza
kuwa magari yanayozinduliwa ni magari ambayo yamesanifiwa hapa nchini ili
kukidhi mahitaji ya barabara za Tanzania na kwamba kumwezesha msafiri kujiona
kama safari sio kero bali ni sehemu ya kupumzika.
Post a Comment
Post a Comment