Serikali mkoani mbeya inatarajia kufanya kampeni ya utoaji wa
chanjo ya Surua-Rubella kwa watoto wenye umri kati ya
miezi tisa mpaka miaka kumi na tano kwa
lengo la kudhibiti na kukinga milipuko ya Surua ili kutokomeza ugonjwa huo.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa wilaya ya mbeya Dk.
Norman Sigala kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa mbeya Mh. Abas Kandoro katika ofisi
za mkuu wa mkoa huyo amesema serikali ilianzisha mpango wa kufanya kampeni chanjo
hiyo tangu mwaka 1999 huku kampeni ya mwisho ilifanyika mwaka 2011 na kampeni
ya mwaka huu itaanza tarehe 18 oktoba mapaka tarehe 24 oktoba.
“kuanzia oktoba 18
mpaka oktoba 24 wizara ya Afya na ustawi wa jamii kupitia mpango wa taifa wa
chanjo ikishirikiana na wadau wa chanjo itafanya kampeni ya chanjo ya
Surua-Rubella kwa watoto wote walio na umri wa kati ya miezi tisa mpaka kumi na
tano” alisema Dk, Sigala.
Dk. Sigala alisema kuwa kampeni hii itahusisha mikoa yote ya
Tanzania Bara na Zanzibar na itaendeshwa katika vituo vya kutolea huduma ya
Afya, shule za msingi na sekondari, na vituo maalumu vitakavyoundwa kipindi cha
kampeni ili kuongeza huduma karibu na walengwa.
Dk. Sigala alisema licha ya kiwango cha chanjo kuendelea kuwa
juu milipuko imekuwa ikitokea kutokana na kuwa watoto takribani asilimia 20kwa
baadhi ya wilaya hawapati chanjo.
“ni wazi kuwa watototakribani
asilimia 20 kwa baadhi ya wilaya hawapati chanjo na kwa wale waliopata chanjo
kwenye umri wa miezi tisa asilimia 15 hawapati kinga kwasababu ya kibailojia
katika umri huo, hivyo kampeni ya Surua huwapa watoto ambao hawakupata kinga
kwasababu zozote zile, hiyo ndio fursa nyingine
ya kukingwa na ugonjwa hatari wa Surua na Rubella kwani huu ni mpango wa kidunia wa kutokomeza
maradhi ya surua na rubella ifikapo mwaka 2020 hivyo nawaomba wakazi wa mkoa wa
mbeya kujitokeza kwa wingi kuwaleta watoto wao ili kukamilisha zoezi hili kwa
kiwango kikubwa na kwamba kampeni hiyo kwa mkoa wa mbeya itafanyika katika
Halmashari zote kumi na uzinduzi rasmi utafanyika oktoba 18 wilayani Ileje” alisema Dk Sigala.
Aidha Dk Sigala alisema ni kudumisha upunguzaji wa magonjwa,
ulemavu na vifo vinavyotokana na surua na rubella, ambapo kampeni hiyo itakwenda
sanjari na utoaji wa matone ya vitamini A na dawa ya kukinga ugonjwa wa minyoo,
usubi, mabusha, matende, na ngiri maji na kwamba chanjo hiyo itatolewa bure.
Hata hivyo mratibu wa huduma za chanjo mkoa wa mbeya Japhat
Mhaye alisema chanjo hiyo inafaida kubwa kwa wananchi kutokana na maradhi
yanayojitokeza kwa watoto wanapofikia umri fulani pia amewatoa hofu wananchi
kuhusu uwenda chanjo hiyo inamadhara, amesema chanjo hiyo ni salama wala haina
madhara yeyote.
Post a Comment
Post a Comment