GuidePedia

0

Safu ya viongozi wa ngazi mbali akiwemo mtendaji wa kijiji cha ijumbi Zephania Mgaya aliesimama na Diwani wa kata ya ruiwa alievaa suti ya kijivu mh, Alex Mdimilaje.

Wananchi wakiwa katika mkutano wa huo wa hadhara wakimsikiliza mtendaji wa kijiji.

Mwalimu wa shule hiyo Laitony Ngole akielezea jinsi alivyokuwa akiwafundisha watoto.


Mwananchi akisoma barua ya mwalimu aliomwandikia diwani kuhusu kukili kufundisha wanafunzi wa darasa la kwanza mpaka la sita.

Tofari na msingi unaojengwa kwaajili ya madarasa  mapya katika shule hiyo

 




Wakazi wa vitongoji vya Ilanji na Ishungu vilivyopo katika kata ya Rwiwa Wilaya ya mbarali Mkoani Mbeya wameulalamikia uongozi wa Serikali ya kata hiyo kwa kushindwa kusimamia kikamilifu maendeleo ya kata yao.

Wakizungumaza na waandishi wa habari katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na mtendaji wa kijiji cha ijumbi Zephania Mgaya katika kitongoji cha Ishungu wakazi hao wamesema kuwa wamekuwa wakichangia miradi mingi ya maendeleo pasipo mafanikio.

Aidha wamesema moja kati ya miradi waliowai kuchangia ni pamoja na shule ya msingi ishungu ambayo mpaka sasa haijakamilika licha ya kutoa michango yao.

Wamesema walipokuwa wakihoji kuhusu mwendelezo wa shule hiyo wamekuwa wakipatiwa majibu yenye mkanganyiko kutoka kwa viongozi wao, huku viongozi wakidai kuwa shule hiyo sio ya msingi bali ni ya awali jambo ambalo limewashangaza wakazi hao pamoja na mwalimu aliyekuwa akifundisha shule hiyo.

Kwa upande wake mtendaji wa kijiji cha ijumbi kata hiyo Zephania Mgaya amsesema  ubadhirifu wa fedha uliojitokeza yeye hakuwa na taarifa nao hivyo atafuatilia kwa ukaribu ili kubaini tatizo hilo kwa kupitia majina ya watu waliotoa michango katika stakabadhi na kuhusu shule hiyo kuitwa shule ya msingi ni jambo ambalo si la kweli maana shule hiyo haijasajiliwa kisheria hivyo kama kuna wanafunzi wanasoma shule hiyo wa darasa la kwanza ni kinyume na sheria.

Akijibu hoja za wakazi hao Diwani wa kata ya Rwiwa Mh, Alex Mdimilaje amesema sababu iliopelekea shule hiyo kubaki kuwa shule ya msingi ni pamoja na kutokuwa na mwalimu mwenye taaluma ya ualimu kwani mwalimu aliopo katika shule hiyo taaluma yake ni kufundisha watoto wanaosoma chekechea na sio darasa la kwanza.

Kwa upande wake mwalimu wa shule hiyo Laitony Ngoli amekanusha kuitwa shule hiyo ya chekechea badala ya kuitwa shule ya msingi kwani amefundisha watoto wa darasa la kwanza mpaka la sita  kwani shule hiyo imeanza tangu mwaka 2007 na yeye ndio aliyekuwa akiwafundisha wanafunzi hao huku mitihani yao wakienda kufanyia katika shule ya msingi ruiwa ambayo ndio shule mama.

Amesema kuhusu vifaa vya kufundishia alikuwa akivipata kutoka kwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi rwiwa moja kati ya vifaa hivyo ni pamoja na vitabu vya kufundishia.

Hata hivyo makubaliano walioafikiana katika mkutano huo ni kujenga madarasa mengine ndipo viongozi hao watawaleta walimu wenye taaluma ya kufundisha watoto wa shule ya msingi hivyo wananchi kwa pamoja wamekubaliana na tamko hilo na kuanza kuelekeza nguvu zao upya ili kufanikisha zoezi hilo.


                                 Na, Lumemo blog




Post a Comment

 
Top