GuidePedia

0

Waziri wa maliasili na utalii Mh, Lazaro Nyalandu akizunguza na waandishi wa habari.





Waandishi wa habari wakimsikiliza waziri wa maliasili na utalii akiongea jambo.


Baadhi wa waandishi wa habari wakipiga picha na waziri wa maliasili na utalii nje ya ukumbi huo baada ya kumaliza mazungumzo nae.

 


Serikali imesema haitasita kumchukulia hatua za kisheria mtu yeyote anaejihusisha na kitendo cha uwindaji haramu katika hifadhi za Taifa bila kujali wadhifa alionao ilihali amethibibitika akifanya kitendo hicho.
Hayo yamesemwa na waziri  wa maliasili na utalii Mh, Lazaro Nyalandu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini mbeya katika ofisi za mkuu wa mkoa wa mbeya Mh, Abas Kandoro.

Aidha Nyalandu amesema moja kati ya hatua aliyoifanya katika wizara hiyo ni kupunguza kiwango cha uwindaji katika kutoka asilimia mia moja mpaka kufikia asilimia hamsini na kutotoa vibali vya uwindaji kiholela.

Nyalandu amesema kuwa kumekuwa na tabia kwa baadhi ya vyombo vya habari kuandika habari zisizo na ukweli hususani magazeti na mujoa kati ya habari ilioandikwa isiyo na ukweli ni baada ya waziri huyo kuipiga marufuku kampuni moja ya uwindaji kutoka nje ya nchi ndipo gazeti moja likaandika kuwa Nyalandu aisababishia hasara serikali ya Tanzania Tsh, bilioni tatu.

Kuhusu tuhuma zilizozungumzwa hivi karibu zinazomuhusu yeye na msanii wa Bongo Movie Aunty Ezekieli kutanua nae huko marekani Nyalandu amesema sio kweli bali yeye alikwenda kwaajili ya shughuli tofauti na msanii huyo hivyo tuhuma hizo si zakweli bali ni njia ya kumchafu kutokana na kazi nzuri anazozifanya.


                               Na, Lumemo blog






Post a Comment

 
Top