GuidePedia

0

Gari ya askari wa kutuliza ghasia ikiwa katika eneo la tukio na askari wakiwa ndani ya gari hilo.

Wananchi wa    kata    ya lwangwa   Halmashauri  ya Busokelo wilayani  Rungwe mkoani Mbeya wameandamana  mpaka katika ofisi za Halmashauri  hiyo    wakishiniza  serikali wilayani  humo   kuwatoa  watu  walio kamatwa   baada ya kuhusiwa kuhusika  na kifo cha  Gabriel Mwandemwa  mwenye  umri wa mika  {40} aliye uwawa na  wananchi   katika  siku za   hivi karibuni kutokana na imani za  kishirikina.

Wakizungumza  na   waandishi wa habari   wakati  wa mandamano hayo  wanachi  hao   walisema hatua  hiyo ilikuja  kufuatia   jeshi  la polisi wilayani  humo kuwakamata   baadhi ya wananchi   kwa madai ya kuhusika na kifo  cha kijana  huyo  aliyefariki dunia siku za hivi karibuni  kutokana  na    vitendo vya  ushirikina.

Walisema  mnamo majira ya   usiku  wa kuamkia oktoba   moja  jeshi la polisi  liliwasili kinyemela katika maeneo hayo  kwa  kuwakamata  baadhi ya  wananchi   bila kushirisha  uongozi wa  maeneo husika   kwa kufikishwa  kituoni,  ambapo hali  hiyo  ilikupelekea  wao kama  wanachi kuchukua  hatua ya  kupinga   kitendo hicho   kwa  kuungana  kwa pamoja   na kufanya maadamano ya amani  hadi katika ofisi  ya mkurugezi  wa Halmashauri hiyo  wakitaka kutolewa  kwa ndugu  zao.

Hata  hivyo jeshi la  polisi liliwasili  eneo  la  tukio   na kisha kuanza  kusaidia kuzuia    ghasia  hizo   ikiwa  ni pamoja  na kuwatia  hatiani wale  wote ambao walionekana kuanzisha vurugu hizo.

Diwani wa kata  hiyo Robati Mwaibata alikiri kuwapo kwa  adha hiyo  na kusema  mpaka sasa wameshindwa kuongea  na wananchi wake  kutokana na  vurugu kuendelea kuchukua nafasi  yake.

Alisema    chanzo   cha  tukio hilo ni  baada  ya jeshi la polisi  kuwakamata  baadhi ya  vijana wa  eneo hilo kwa  tuhuma  za  kuhusika  na  mauji  ya    Gabriel Mwandemwa aliye fariki dunia siku za  hivi karibuni kwa   kukatwa na  mapanga na kisha mwili wake kuchomwa moto.

Alisema mpaka sasa wanaendelea  kutuliza ghasia  hizo kwa  kushirikiana na jeshi la  polisi  wilayani humo .

Hata  hivyo     juhudi za kumtafuta mkuu wa wilaya ya rungwe krspini meela ziligonga mwamba  mara  baada  ya    simu yake  kuita bila kupokelewa.

         Na, Baraka Lusajo Rungwe 

Post a Comment

 
Top