GuidePedia

0
Diwani wa kata ya Rwiwa Allex Mdimilaje akiongea na waandishi wa habari kuhusu tatizo la choo cha soko la wimba mahango ambapo tatizo hilo limedumu kwa muda mrefu, takribani mwaka mmoja.
Diwani Allex Mdimilaje alipokuwa anachangia mchango wake wa kumalizia choo hicho ambapo alichangia kiasi cha shilingi elfu themanini.
Hili ndo shimo la choo kinachotakiwa kumaliziwa wimba.
Hawa ni wananchi wakijiji cha wimba wakiwa katika mkutano na kumsikiliza mwenyekiti na diwani wakihutubia katika mkutano huo.
Huyu aliyevaa kofia y kijani ni mwenyekiti wa kijiji cha wimba mahango, Witson Kazimotoakiwa katika mkutano huo.
............................................................................................................................................................
Wananchi wa kijiji cha wimba mahango Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya wameulalamikia uongozi wa serikali ya kijiji cha wimba mahango kwa kutokamilisha tatizo la choo cha soko la kijiji hicho kwa muda wa zaidi ya mwaka mmjo sasa.
Wakiongea na waandishi wa habari katika mkutano uliyofanyika katika kijiji hicho wananchi hao wamesema kuwa wao wamechangishwa michango mara kadhaa lakini serikali haijatoa mchango wowote ili kukamilisha ujenzi huo.
Hta hiuvyo wananchi hao wamesema wanashangazwa na uongozi wa kijiji kwakutokamilisha choo hicho ikiwana ushuru wa soko hilo wanachukuwa kila siku, pia soko hilo limekua linamkusaniko wa watu wengi hasa siku za mnada kutokana na watu kutoka sehemu mbali mbali wanafika sokoni hapo kwaajili ya kujipatia mahitaji.

Kwaupande wake Diwani wa kata hiyo ya Rwiwa Bw, Allex Mdimilaje amekiri kuwepo kwa tatizo na kuhaidi kuwa atalifuatilia kwa undani ili kuhakikisha linakamili halaka iwezekanavyo
Pia ameanza kwa kutoa mchango wake wa shilingi elfu themanini ili ziaze kufanya kazi kazi katika ujenzi huo
Aidha amesema licha ya shimo hilo kuwa linahitaji fedha nyingi lakini atajitahidi kadri ya uwezo wake ili kufanuikisha ujenzi huo.
Awali kamati ya ujenzi wa choo hicho imesema kuwa mpaka sasa shimo hilo limeghalimu kiasi cha fedha zaidi ya shilingi elfu themanini na kwamba kunamfadhili ambaye alijitokeza kuwafadhili kiasi cha fedha shilingi elfu themanini katika ujenzi huo ndizo lilizoweza kusaidia kufikia hatua hiyo.
Hata hivyo kamati hiyo iliwaomba wananchi wawe na imani na kamati hao kwa kile wanachokifanya ni uhakika na kwa maslai ya wananchi hivyo wataenda kinyume na taratibu zilizowekwa.


Post a Comment

 
Top