GuidePedia

0


 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji). Dk. Mary Nagu (katikati) akikabidhi pikipiki kwa moja ya vikundi 130 vya Vicoba vilivyo chini ya Taasisi ya PFT katika hafla ya kuviongezea uwezo kwenye Ukumbi wa PTA, Sabasaba, Dar es Salaam . Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Temeke, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo. Abbas Mtemvu. (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

 Mwenyekiti wa PFT, Abbas Mtemvu akihutubia wakati wa hafla hiyo

 Waziri, Dk Mary Nagu akihutubia katika hafla hiyo, ambapo alimsifia Mtemvu kwa kuanzisha taasisi hiyo ambayo imewasaidia kupunguza umasikini wa wananchi jimboni humo.

 Mtemvu akimpatia Dk. Mary Nagu tuzo kwa ajili ya Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ameisaidia Taasisi hiyo

 DK. Mary Nagu akimkabidhi mmoja wa viongozi wa VICOBA pikipiki ya mkopo

 Waziri Dk. Mary Nagu akimkabidhi gari dogo mmoja wa viongozi wa Vicoba. PFT imetumia sh. mil. 195 kununua magari, pikipiki na Bajaji vilivyotolewa mkopo kwa wanachama.

 Waziri, Dk. Mary Nagu akimkabidhi gari aina ya Toyota Noah mmoja wa viongozi wa VICOBA

 Kikundi cha Msanii Snura (katikati), kikitumbuiza wakati wa hafla hiyo

 Wageni waalikwa wakifurahi wakati Snura  ‘mama wa Majanga’ akitumbuiza katika hafla hiyo

 Sehemu ya wana Vicoba


                                         Snura ‘Majanga’ akifanya vitu vyake ukumbini

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Juma Kassim ‘Juma Nature’ akitumbuiza wakati wa hafla ya kuviongezea uwezo vikundi vya Kuweka na Kukopa (VICOBA) 130 ambavyo ni wanachama wa Taasisi ya PFT kwenye Ukumbi wa  PTA Sabasaba, Dar es Salaam, ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji). Dk. Mary Nagu. Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ni Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu. Baadhi ya vikundi hivyo viligawiwa pikipiki, bajaji na magari pamoja na fedha taslimu.
Wana Vicoba wakishangilia wakati Nature akifanya mambo ukumbini

Mary Nagu akiondoka huku akisindikizwa na Mtemvu

Post a Comment

 
Top