WENYEVITI
wa Vijiji na Vitongoji 135 wa vyama
mbalimbali Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya wametishia kugoma kufanya shughuri za
maendeleo ya kuwatumikia wananchi kwa madai kuwa Serikali wilayani humo imeshindwa
kuwapa stahiki zao.
Wakizungumza
jana kwa nyakati tofauti kwenye mkutano mkuu uliofanyika katika ukumbi wa CCM wenyeviti hao walidai kuwa
Halmashauri ya wilaya hiyo Imeshindwa kuthamini mchango wao na kuwa wamegeuzwa misukule kwa
kuwatumikisha bila kuwapa chochote.
Ezekiel
Mwakataja mwenyekiti wa Mpelangwasi na Noh Mwakasege wa msasani (CCM)
walisema
kuwa Serikali imewasariti kwa kuwaona hawana maana kwa kutowapa stahiki zao
hivyo na wao kama wenyeviti hawapo tayari kufanya nao kazi na kuwa wamekuwa
wakifanya kazi katika mazingira magumu huku wakikosana na wananchi kwa
kukusanya michango ya maendeleo lakini halmashauri hiyo imekuwa ikiwabeza.
Stephen
Ngonya mwenyekiti kitongoji cha Mpuguso na Issa Mwaikambo mwenyekiti kijiji cha Mpuguso (CCM) walisema kuwa halmashauri ya wilaya hiyo imeshindwa kuwapa
stahiki zao kwa muda mrefu huku wakizidi kuwatumikisha kwa kuwahamrisha
kukusanya michango ya maendeleo huku posho wakipewa madiwani na maafisa
watendaji na kuwa kuanzia leo (jana) hawapo tayari kutumikishwa tena hadi pale
watakapopewa madai yao.
Elia
Kinanasi mwenyekiti wa kitongoji cha Mbyanga na Tumaini Kibo mwenyekiti wa
kitongoji cha Lumbila (CHADEMA) wao walidai kuwa wametumikia sana wananchi na
maendeleo yamesonga mbele kwa kujituma kwao lakini wanaopata sifa ni madiwani
na watendaji wakati wao ndiyo wanaokusanya michango ya shughuri zote katika
vijiji husuika.
Walisema
kuwa wenyeviti wanakabiliwa na changamoto kubwa hali inayopelekea hadi kuwekwa
lumande pale mauaji yanapotokea katika sehemu zao na kuwa jeshi la polisi
linapofika katika maeneo hayo kwa ajili ya kuwatafuta waarifu lazima wapiti kwa
wenyeviti ndipo wawakamate waarifu lakini bado halmashauri hiyo pamoja na
wanasiasa wengine wamewageuza wao kuwa ni madaraja.
Mwenyekiti
wa wenyeviti wilayani humo Anton Mwalugembe(CCM) alisema kuwa wameitisha
mkutano mkuu kwa lengo la kujadili namna ya kupata malipo yao ya posho kama
ilivyoagizwa na Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania lililoketi tarehe
31|10|2013 wakati mbunge wa vunjo (TLP) Augostino Mrema alipouliza swali kuwa
ni lini wenyeviti wa vijiji wataanza kulipwa posha zao za kila mwezi.
Alisema
swali hilo lilijibiwa na Naibu waziri (TAMISEMI)Agrey Muanry ambaye alijibu
kuwa fedha za malipo ya wenyeviti zinapelekwa kwenye halmashauri za wilaya kila
mwaka na kuwa kwa majibu hayo wao kama wenyeviti waliamuandikia mkurugenzi wa
halmashauri siku ya Tarehe 24|12|2013 ambapo nakala walimpelekea mkuu wa wilaya
kupitia kalani wake ikieleza kutaka kupatiwa malipo yao.
Katika
barua hiyo wajumbe wote walikubaliana kwa pamoja kuwa wamefanya kazi katika
mazingira magumu ambayo ni hatari kwa maisha yao hivyo ifikapo tarehe 16|2|2013
watarudisha mihuri na vitendea kazi vyote vya kijiji kwenye ofisi ya mkurugenzi
mtandaji wa halmashauri na kuwa itakuwa ndiyo mwisho wao kufanya kazi na
kitakachoendelea ni kufungua kesi mahakamani dhidi ya halmashauri hiyo kutowapa
stahiki zao.
“Ndugu
zangu kama kutumika tumetumika vya kutosha kilichobaki sasa ni kuitisha mgomo
pamoja na kumpeleka mahakamani mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ili uweze
kutulipa fedha zetu hivyo tutakutana tena tarehe 16 mwezi huu kutoa tamko la
mgomo na kumtafuta mwanasheria ili aanze kusimamia kesi hiyo ya madai”alisema mkuu
wa wenyekiti huyo.
Kaimu
mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo Gwabo Mwansasu alipofuatwa na
waandishi wa habari ofisini kwake ili atoe ufafanuzi wa madai hayo
hakuweza kuzungumza na
kudai kuwa anasafari kidogo atazungumza siku nyingine.
Mkuu
wa wilaya hiyo Chrispin Meela mbali na nakala ya lalamiko hilo kufika kwa
kalani wake alidai kuwa wenyeviti hao kama waliona mkurugenzi hajaweza
kuwasikiliza ilipaswa wangefike ofisini kwake ili kuzungumzia suala hilo, kwani
lilipofikia ni mahali pabaya linaweza likakwamisha shughuri za maendeleo na
kuzuka kwa mgogoro mkubwa.
Post a Comment
Post a Comment