WANANCHI
wa kijiji cha Lema kata ya Busale wilayani Kyela mkoani Mbeya wameilalamikia
Idara ya elimu iliyochini ya Halmashauri ya wilaya hiyo kwakutosikiliza kilio chao
cha kuwaletea waalimu katika shule yao
ya msingi Lema.
Wakizungumza
na waandishi wa habari jana kwa nyakati tofauti kijijini humo wananchi hao walidai
kuwa kwa muda mrefu shule hiyo imekuwa haina waalimu huku idadi ya wanafunzi
ikizidi kuongezeka lakini Idara hiyo imeshindwa kupeleka waalimu katika shule
hiyo.
Walisema
shule hiyo inawaalimu wanne kati yao wavulana
wapo wawili na wanaume wawili huku wanafuzi wakifikia mia sita kitu ambacho ni
kinyume na utaratibu wa wizara huku wanafunzi wa shule hiyo wakikosa haki yao ya msingi katika
kupata elimu stahiki.
mwandishi wa habari hizi alifika katika shule hiyo na kujionea uhalisia wa kero hiyo ulioenda
sambamba na kuongea na viongozi wa kijiji hicho ambao ni mwenyekiti wa kijiji
Christopha Lukali na Mratibu wa elimu wa
kata Umbege Lugano ambao walikiri kuwepo na kero hiyo na kuwa tayari
wamelipeleka suala hilo kwenye idara usika.
Diwani
wa Kata hiyo Ezekia Msyani alisema kuwa ni kweli shule hiyo inawaalimu wanne
huku wanafunzi wakiwa 600 na kwamba walikwisha fanya mkutano mkuu wa kijiji
kulizungumzia suala hilo kuhusu uhitaji wa waalimu na muhtasari wa mkutano huo
waliupeleka kwenye ofisi ya elimu na hivi sasa wanasubiri utekelezaji wa ombi lao.
Aliongeza
kuwa shule hiyo imekamilika kila idara na haina tatizo lolote isipokuwa
upungufu wa waalimu kitu ambacho kinadidimiza elimu kwa wanafunzi wanaosoma
kwenye shule hiyo na kwamba aliiomba idara hiyo kuliangalia suala hilo kwa jicho la tatu
ili kunusuru hali hiyo itakayo didimiza elimu kwa wanafunzi wanaosoma kwenye
shule hiyo.
Afisa
elimu msingi wa wilaya hiyo Claud Bulle alipozungumza na gazeti hili ofisini
kwake alikiri kuwepo na upungufu huo na kudai kuwa hilo ni tatizo kubwa
ikichukulia waalimu wanne kwa wanafunzi mia sita ni hatari kubwa inayoweza
kushusha ufauru kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Aliongeza
kuwa kwa kuliona hilo idara yake ilipeleka maombi ya uhitaji wa waalimu kwa
wilaya nzima na watatoa kipaumbele cha kupeleka waalimu wengi katika shule hiyo
na kwamba katika sheria za wizara ni kuwa wanafunzi alobaini wanatakiwa
wafundishwe na mwalimu mmoja kwa wanafunzi mia sita waalimu wanne ni pengo
kubwa la waalimu lilipo katika shule hiyo.
Aliwataka
wananchi wa kijiji hicho kuwa wavumilivu kwani wao kama idara wanalifanyia kazi
tatizo hilo na
kuwa watapeleka waalimu wa kutosha katika shule hiyo pindi watakapoletewa
waalimu wapya mwaka huu.
(Habari na Ibrahim Yassin)
Post a Comment
Post a Comment