Mwenyekiti wa usalama barabarani Mkoa wa Mbeya Allan Mwaigaga Alipokuwa aikongea na waandishi wa habari kuhusu ajali zinazoendelea kutokea Mkoani Mbeya.
Hapa Mwenyekiti akisisitiza kuhusu uvaaji wa kofia za pikipiki kwa waendesha bodaboda.
Hapa akitolea mfano kwa baadhi ya waendesha bodaboda wanapokuwa wakiendesha huku wakiongea na simu.
Mwenyekiti wa usalama barabarani Mkoa wa Mbeya Allan Mwaigaga amewataka madereva magari na Pikipiki kuacha tabia ya kunywa pombe pindi wanapokuwa barabarani na kuongea na simu, akiongea na waandishi wa habari jana ofisini kwake Mwaigaga amesema ajali nyingi zinatokana na uzembe wa madereva. Aidha amewashauri wamiliki wa vyombo hivyo ambao ni watumishi wa Serikali kuacha kutumia maadaraka yao vibaya kwani madereva wengi wamekuwa wakikiuka sheria kwakutegemea waajiri wao ni watumishi wa Serikali. pia ameahidi kuwa katika kipindi chake cha uongozi atahakikisha anasimamia usalama wa barabarani kiukamilifu na kwamba mtu yeyote atakaekiuka sheria za barabarani atamchukulia hatua za kisheria kwa mujibu wa sheria zilizowekwa.

Post a Comment
Post a Comment