KAMANDA wa
Jeshi la Polisi mkoani Mbeya(RPC) Ahmed Msangi amewataka wananchi wa wilaya ya Rungwe
mkoani hapa kudumisha amani, utulivu na mshuikamano uliopo nchini kwa kufanya
kazi kwa kushirikiana hasa katika kipindi hiki cha kuelekea katika chaguzi za
Selikari za mitaa ambako ndiko uvunjifu wa amani unapo tokea.
Msangi
aliyasema hayo jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya
Polisi Tukuyu ambapo mbali na kuwataka wananchi kudumisha amani pia aliwataka
wananchi kushirikiana na polisi jamii katika suala la ulinzi shirikishi ili
kuwalinda wananchi pamoja na mali zao.
Alisema Jeshi
la polisi lipo kwa ajili ya kuwatumikia wana nchi na kwamba aliwataka wananchi
kushirikiana na jeshi hilo kwa kuwafichua waalifu pale wanapo wabaini pomoja na
kuona kama kunaviashiria vya uvunjifu wa amani huku akiwataka askari wa jeshi
hilo kuto toa siri za wananchi pindi wanapowafichua waharifu.
Diwani kata
ya Kawetele ambaye pia ni mwenyekiti wa NCCR Mageuzi wilayani humo Anyimike
Mwasakilali mbali na kumpongeza mkuu huyo Polisi pia alizitaja changamoto
zilizopo katika kata hiyo ambayo ndiyo makao makuu ya wilaya kuwa ni kutokuwa
na ofisi yan kata hali inayowalazimu kufanya kazi katika mazingira magumu.
Alisema kuwa
walikwisha toa taarifa ya maandishi kwa mkurugenzi wa halmashauri nakala
waliipeleka kwa mkuu wa wilaya wakiomba kupatiwa jingo kwa ajili ya ofisi
lakini hadi leo hawajapatiwa ofisi kitu ambacho kinawapa wakati mgumu katika
utendaji wao wa kazi kwa kuwa ofisi ya kata ina tumiwa na maafisa
kilimo,afya,katibu kata,mratibu elimu na afisa mtendaji mwenyewe hivyo
kukosekana kwa ofisi hiyo ni changamoto kubwa kwao.
Antoni
Kasokera alitoa changamoto inayowakabili wananchi ni kuwa
baadhi
ya polisi wasiokuwa waaminifu wamekuwa wakitoa siri na kuwataja wananchi pindi
wanapowapelekea taarifa za kuwepo kwa uharifu au viashiria vya uvunjifu wa amani
Akiijibu
Changamoto hiyo mkuu huyo wa polisi alisema kuwa yeye analijua tatizo hilo na
tayari amekwisha fanya mikutano kadhaa kwa lengo la kukusanya kero kwa raia na
tayari amekwisha waagiza wakuu wa polisi katika wilaya zote kuwa endapo
matatizo hayo yataendelea basi hatakuwa na msamaha kwa afisa yeyote atakaye
bainika kufanya hivyo.
Katika
mkutano huo pia vikundi mbalimbali vilikuwepo kama Polisi jamii kata ya
kawetele,Msasani,kikundi cha Sakosi Uwadi kata ya Igogwe,Kikundi cha waendesha
Bodaboda Tukuyu mjini ambapo Rpc ameahidi kuwachangia endapo wataanzisha Sakosi
yao kwa lengo la kujiimarisha kiuchumi na kukuza mitaji mara dufu.
Post a Comment
Post a Comment