Muuguzi wa zahanati ya kijiji cha malangali kata ya totowe Wilaya ya chunya, Pili Ntongolo akiwa katika chumba cha kuhifadhia dawa.
hiki ni moja kati ya vyumba vya kupumzishwa wagonjwa na hiki ndo kitanda chake.
hiki ndio choo cha zahanati hiyo.
huyu ni moja ya wagonjwa katika zahanati hiyo.
hii ndo silingibodi ya zahanati hiyo ikiwa ni jengo zima.
.........................................................................................................................................
hiki ni moja kati ya vyumba vya kupumzishwa wagonjwa na hiki ndo kitanda chake.
hiki ndio choo cha zahanati hiyo.
huyu ni moja ya wagonjwa katika zahanati hiyo.
hii ndo silingibodi ya zahanati hiyo ikiwa ni jengo zima.
.........................................................................................................................................
Dawa
zinazosambazwa na Serikali katika zahanati ya kijiji cha Malangali kata ya
Totowe wilaya ya Chunya zipo hatarini kuharibika kutokana na utunzwaji mbovu.
Muuguzi wa
kituo hicho Pilly Ntongolo amekiri kuwepo kwa tatizo hilo kwa muda mrefu tangu zahanati
hiyo kuzinduliwa kwa mbio za mwenge miaka miwili iliyopita huku uongozi wa
kijiji na kata kushindwa kuchukua hatua madhubuti.
Ntongolo
amesema kuwa dawa hizo zimekuwa zikitunzwa hovyo kutokana na kutokuwepo kwa
shelfu za mbao ambazo zingewezesha kupangwa
kwa utaratibu unaoeleweka,lakini imekuwa tofauti baada ya uongozi wa kijiji
kushindwa kununua mbao za kutengenezea shelfu hizo.
Hali imekuwa
mbaya zaidi baada ya utaratibu mpya wa kusambaza dawa vijijini kupitia mpango
wa shirika la Bohari na usambazaji
dawa[MSD]kwa walengwa kuzambaza dawa katika zahanati hiyo kulundikwa
hovyo bila utaratibu hali ambayo ina hatarisha usalama wa dawa hizo.
Uchunguzi
umebaini kuwa kituo hicho chenye namba za MSD 105866 kuwa na tatizo pia na
tatizo kubwa la kuharibika dari baada ya mchwa na popo kuharibu dari na
kusababisha dawa hizo kumwagikiwa na vumbi pia na mikojo ya popo hali
inayohatarisha afya za watumiaji wa dawa hizo.
Pia zahanati
hiyo inakabiliwa na tatizo la kuwepo maji hali inayolazimu muuguzi huyo kulazimika
kuchota maji kutoka kwake wakati wa kutoa huduma ya kuzalisha kwa wajawazito
wanaofika kujifungua.
Aidha vyoo
vya zahanati hiyo vimeziba kutokana na ukosefu wa maji hali inayolazimu wagojwa
kujisaidia vichakani kutokana na kukosekana kwa maji hali inayohatarisha afya
kwa wagonjwa.
Changamoto
nyingine inayoikabili zahanati hiyo ni pamoja na mazingira machafu ambapo nyasi
zimeota hadi katika upenu wa zahanati,ambapo muuguzi hulazimika kuacha huduma
kwa wagonjwa ili kupunguza uchafu uliokithiri.
Mtendaji wa
kijiji hicho Yaledi Mwanguku hakuwa tayari kumpeleka mwandishi katika zahanati
hiyo akidai muuguzi hayupo ,lakini mwandishi alipokwenda alimkuta muuguzi hali
inayoonesha kutokuwa tayari kujibia kero hii.
Hivi sasa
zahanati hiyo haina Mwenyekiti wa Kamati ya Afya kutokana na Ahmed Ndauka
kujiuzuru kutokana na tofauti baina yake na muuguzi ambapo Kamati ya Afya ya
wilaya ilifika kutatua mgogoro huo.
Post a Comment
Post a Comment