waliosimama mbele kushoto ni mkuu wa shule Eckson Mwakalikamo akibadilishana mawazo na mkurugenzi wa vanessa, Bi, Shukran Gidion.
kulia mkuu wa shule ku;lia Mwakalikamo kushoto mgeni rasmi Mkurugenzi wa Vanessa Bi Shukran Gidion akihutubia katika ukumbi wa shule. Moja kati ya walimu waliyotunukiwa zawadi siku hiyo. Diwani wa kata ya Isyese Sanke Sesoakihutubia.
.................................................................................
kulia mkuu wa shule ku;lia Mwakalikamo kushoto mgeni rasmi Mkurugenzi wa Vanessa Bi Shukran Gidion akihutubia katika ukumbi wa shule. Moja kati ya walimu waliyotunukiwa zawadi siku hiyo. Diwani wa kata ya Isyese Sanke Sesoakihutubia.
.................................................................................
Mkurugenzi
wa TEHLAH FOUNDATION Bi. Shukurani
Gidion ambayo inamiliki shule ya sekondari ya Vanessa iliyopo Kata ya Isyesye
Jijini Mbeya ametoa tuzo kwa Walimu na wanafunzi wa shule hiyo baada ya kufanya
vizuri mtihani wa kidato cha pili kimkoa na kitaifa.
Hafla ya
kutunuku tuzo hizo imefanyika katika ukumbi wa shule hiyo Januari 31 mwaka huu
ambapo walimu 15 na wanafunzi 55 walitunukiwa na mgeni rasmi Pascal Obed Busigo
ambaye ni Afisa Elimu Taaluma Msaidizi Sekondari Jiji la Mbeya.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa Tehlah Foundation anatimiza ahadi yake aliyoitoa mwaka jana katika
mahafali ya kidato cha nne,endapo wanafunzi na walimu watafanikisha kupatikana
matokeo mazuri na ndiyo dhamira yake kuona shule yake inafanya vizuri.
Shule hiyo
yenye usajili namba S.3572 ambayo ina ushirikiano na Shirika la Gateway la
Ujerumani ambapo katika matokeo hayo
shule imeshika nafasi ya kumi na tatu kiwilaya
kati ya shule 47,na hamsini na nane kimkoa kati ya shule 265,na imekuwa shule ya 59 kikanda kati ya shule 464
katika matokeo hayo wanafunzi 127 waliofanya mtihani wote wamefaulu kuingia
kidato cha tatu.
Mkuu wa shule hiyo Eckson Mwakalikamo amesema
mwaka uliyopita shule iliweka mikakati mbalimbali kama vile kuanzisha mitihani
ya udahili kabla ya mwanafunzi kupokelewa shuleni ,nakufanya mitihani mara kwa
mara,nakuanzisha masomo ya jioni ili walimu kumaliza mitaala mapema kabla ya
mitihahani ya Taifa.
Kwa upande
mgeni rasmi Pascal Busigo aliupongeza mpango wa shule hiyo wa kutoa tunu kwa
walimu na wanafunzi kwani kufanya hivyo kutaifanya serikali kufikia mpango wake
wa matokeo makubwa sasa maarufu kama BRN[Big Result Now].
Aidha Busigo
aliwataka walimu,wazazi na wanafunzi kufanya kazi kwa ushirikiano kila mmoja
kwa nafasi yake yaani walimu kufundisha vema,wazazi kulipa ada kwa wakati na
wanafunzi kuzingatia masomo kufanya hivyo kutaleta tija huku nidhamu kwa walimu
na wanafunzi ikipewa kipaumbele Mungu atabariki.
Alimaliza
kwa kuwataka kuwa mabalozi wazuri wanafunzi wanaosoma shule hiyo kwani Taifa
litajengwa na wasomi ambao watazingatia uzalendo badala ya kufanya vitendo
viovu wawapo shuleni ambavyo vitapelekea kufanya vibaya katika mtihani wa
kumaliza kidato cha nne hivyo kupoteza mwelekeo wa maisha kwa ujumla.
Hata hivyo
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo Askofu Eliezery Kamwela aliwataka
wanafunzi kumtegemea Mungu wakati wote wa masomo huku nidhamu ikipewa kipau
mbele zaidi na kuwataka wazazi kusaidiana na walimu kuboresha ufaulu wa
wanafunzi shuleni hapo.
Post a Comment
Post a Comment