JAMII
imetakiwa kujitolea kujenga majengo ya mahakama sambamba na nyumba za kuishi
mahakimu na watumishi wengine wa mahakama ili waweze kufanya kazi zao kwa amani
na utulivu kitu kitakachowafanya wao kutenda haki
Wito huo umetolewa
na hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya Nkasi Ramadhani Rugemalila
kwenye maadhimisho ya siku ya sheria nchini ambayo uambatana na dua za viongozi
wa dini mbalimbali kama isharra ya kuanza kwa kazi za mahakama kwa mwaka huu wa
2014
Alisema kuwa
ufike wakati jamii kama ndiyo wadau wakuu wa mahakama wakajenga utamaduni wa
kuanza kujitolea kujenga majengo ya mahakama na nyumba za watumishi kama
ambavyo wanavyofanya kwenye ujenzi wa zahanati,shule,nyumba za walimu na mambo
mengine kwani hiyo ndiyo njia rahisi ya jamii kupata huduma za kimahakama
karibu
Alisema kuwa
kama wananchi wataonyesha moyo wa kujitolea kufanya kazi hiyo serikali
haitawaacha bali ni lazima itaunga mkono jitihada za wananchi katika
kufanikisha lengo lao la kuwa na mahakama nzuri nay a kisasa
Rugemalila
alisema kuwa siku ya sheria kwa mwaka huu imebeba ujumbe kuwa utendaji haki kwa
wakati,umuhimu wa ushiriki wa wadau ambapo alisema kuwa ujumbe huo umekuja kwa
wakati hususani wilayani Nkasi kwani utendaji haki unategemea zaidi wadau
wengine kama polisi,jamii yenyewe kutoa ushahidi na wengineo,hivyo kila mmoja
anatakiwa kuwajibika
Pia alisema
kuwa mahakama yake moja ya changamoto kubwa inayokumbana nayo ni kukosekana kwa
gereza la mahabusu kitu kinachowapa shida polisi na kuwaingiza gharama na
wakati mwingine watuhumiwa kushindwa kufika kwa wakati mahakamani kutokana na
kukosekana kwa usafiri wa uhakika na kuwanyima haki wanayostahili kuipata kwa
wakati
Wakiri wa
kujitegemea kutoka chama cha wanasheria Tanganyika tawi la Rukwa na Katavi
Ileth Mawala alisema kuwa wadau wana nafasi kubwa ya kuhakikisha kesi
zinakwisha kwa wakati endapo kila mmoja atawajibika ipasavyo
Alisema kuwa
haki iliyocheleweshwa ni sawa na haki iliyokataliwa hivyo ipo haja kwa wadau
wote wakiwemo mawakili kuhakikisha kuwa kesi zote nikwisha kwa wakati na kudai
kuwa ozoefu unaonyesha kuwa kesi nyingi zilizo na mawakili uchukua muda mrefu
na kuwataka sasa wawajibike na kuacha kuziairisha kesi kila wakati bila ya
sababu za msingi,ambapo hata wakiri wa serikali mkoani Rukwa Fadhiri Mwandoloma
naye alikazia hoja hiyo huku akisisitiza kuwa kucheleshwa kwa haki ni sawa
kabisa na haki hiyo kuwa imekataliwa
Mkuu wa
wilaya Nkasi Idd Hassan kimanta ambaye aliwakilishwa na katibu tawala wa wilaya
Festo Chonya alisema kuwa haki inayopatikanika kwa wakati huondoa shaka kwa
mahakama na kuwa hilo ni lazima lisimamiwe na kuwa serikali kama mdau mkubwa
itahakikisha inafanya mchakato wa haraka wilayani Nkasi kunapatikanika gereza
la mahabusu ili watu waweze kufika mahakamani kwa wakati
Na alimtaka
kila mmoja kuitafuta haki yake mahakamani na kuwa kama akiona kuwa hajatendewa
haki na vizuri kwenda mahakama ya juu zaidi ya ile ya awali na kuwa hiyo ndiyo
njia pekee na siyo kukimbilia mahakamani pale anapoona ameonewa na mahakama
Post a Comment
Post a Comment