hapo juu katika picha ni makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Busokelo Salome mwakalinga wakati akiongea na wananchi wa kata ya kandete. |
hapo juu katika picha ni mmoja wa wenyeviti wa vijiji wakati wakitoa maelezo juu uwepo wa kituo hicho. |
Na baraka lusajo.
HALMASHAURI ya Busokelo, wilayani
Rungwe mkoani Mbeya imesaini mkataba wa ujenzi wa kituo cha wakulima
kinachotarajiwa kujengwa katika eneo la Kandete wilayani humo, utakaogharimu
kiasi cha sh. milioni 194,370,000.
Akisaini mkataba huo
katika halmashauri ya Busokelo na
kampuni ya Mlogela Company Investment iliyopewa zabuni ya ujenzi wa kituo
hicho, mwenyekiti wa halmsahauri hiyo Mossesi Mwakipunga alisema kuwa
ujenzi huo utasaidia kuongeza jitihada za uzalisaji wa mazao mbalimbali
katika halmashauri hiyo.
‘’Katika kuongeza kiwango cha
uzalishaji wa mazao serikali kupitia halmashauri
imeamua kuchukua hatua ya kuwasaidia wananchi
wake kwa kuwapatia msaada wa kuwajengea kituo cha
wakulima ambacho kitasaidia katika kujikwamua na
hali ya kiuchumi’’ alisema
Alisema fedha hizo
zimetolewa na Serikali na kwamba halmashauri imetoa miezi mitano
kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho tayari kuanza matumizi.
Kwa upande wake kaimu
Mwenyekiti wa Halimashauri hiyo Salome Mwakalinga
aliwataka wananchi kutoa ushirikiano wakati wa ujenzi wa
kituo hicho ambacho kitakuwa na manufaa kwa wananchi wote.
Aidha mwakalinga aliwataka
viongozi wa serikali mkoani hapa kujijengea tabia ya
kusaini mikataba ya maendeleo mbele ya wananchi
kwa lengo la kuondoa maswali kwa
wananchi juu ya matumizi ya fedha zao.
Na lumemo, blog
Post a Comment
Post a Comment