Kikundi cha wazee wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa mbeya
wamekemea vikali na kulaani tabia ya baadhi ya wabunge wabunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania
wanaotoa kauli za matusi na kuwakashifu waasisi wa nchi pindi wanapokuwa
bungeni.
Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti mstaafu wa chama cha
mapinduzi CCM mkoa wa mbeya ambapo kwasasa ni mwenyekiti wa kikundi cha wazee wa
CCM mkoa wa mbeya Isakwisa Santony Mwambulukutu mbele ya waandishi wa habari
katika Hotel ya Mbeya Peack.
Wazee hao wamesema kama wabunge wanauhitaji wa kuendelea na
kazi ya ubunge ni vyema waacha mara moja lugha ya cahfu za kejeli na kashfa kwa
waasisi wa letu kwani uhuru wanaotumia unakikomo chake.
Aidha wamesema hasa kauli
hizo zimekuwa zikitolewa katika bunge maalum la katiba ambapo mara nyingi wamekuwa
wakimkashifu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Sheik Abeid Karume, pasipo
kufikiri kuwa hao ndio chimbuko la utaifa huu tunaojivunia.
Wazee hao wameongeza kuwa wanaunga mkono mfumo wa serikali
mbili hivyo hawahitaji kuwasaliti waasisi wa taifa hili isipokuwa zifanyike
jitihada za kuondoa kasoro ndogo ndogo zilizopo ndani ya muungano.
Pia wameishauri serikali iliyopo madarakani kama inawezekana isisite
kuwashughulikia wote wanaowachafua waasisi wa Taifa hili kwa lengo la kudumisha
amani iliyopo katika nchi yetu.
Hata hivyo wazee hao wametoa wito kwa wazee wote wa Tanzania
wawaunge mkono katika kukemea na kulaani vitendo hivyo vinavyofanywa na baadhi
ya wabunge.
Na, Lumemo bolg
Post a Comment
Post a Comment