Baadhi ya mizigo ya anayetuhumiwa imani za kishirikina ikitokewa nje na wafanyakazi wenzie.
Wafanyakazi
wa kiwanda cha chai
chivanje katika kijiji cha
Itula kata ya itula
Wilayani rungwe mkoani
mbeya wamemtuhumu mfanyakazi
mwenzao kwa imani za kishirikina Faustina Sakogo na kumfukuza katika kambi wanayoishi na kudai ameleta
ugonjwa wa kuhara katika kambi yao.
Wakiongea
na waandishi wa habari katika mkutano wa
hadhara kijiji hapo wamesema chanzo
cha tukio hilo ni baada ya mama huyo
kuleta ugonjwa wa kuhara kambini
hapo na kwamba katika
siku za hivi karibuni mama huyo alileta mchele
ambao alikuwa akiwakopesha
wafanyakazi wenzake lakini watu wote ambao walikuwa wakitumia mchele huo walikuwa wakihara.
Baada
ya mama huyo kuonyesha ubishi juu ya suala
hilo ambapo bila kujua aliweza kuingia katika wakati mgumu baada
ya wafanyakazi hao kuandamana
hadi katika kambi ambalo alikuwa akishi na kwa kutoa mizigo yake huku wakimtaka
aondoke
Aidha
baada ya tukio hilo Faustina Sakogo aliamua
kutoa taarifa kwa kiongozi wa
kiwanda hicho Daniel Mwang’ombola ambaye alifika
kambini hapo kwa kuwataka
wafanyakazi hao kuachana na
vitendo vya kujichukulia sheria
mkononi.
Baada
ya kiongozi huyo kuondoka katika
eneo la tukio wafanyakazi hao waliamua kuanzisha suala hilo
upya kwa kumtaka Faustina kuondoka
mara moja kiwandani hapo kabla
ya jua kuzama ikiwa ni pamoja na kutoa mizigo yake nje.
Na, lumemo blog
Post a Comment
Post a Comment