MGOGOLO mkubwa kati ya wavuvi wa forodha ya kafyofyo
na wananchi wa kitongoji cha Njisi Kijiji cha Kirwa Kata ya Kajunjumele
wilayani Kyela mkoani Mbeya umeibuka na kupelekea hali ya uvunjifu wa amani na
umwagaji damu kutaka kutopkea baada ya kutoelewana baina ya watu hao.
Akizungumza
na waandishi wa habari kwenye forodha hiyo,Mwenyekiti wa forodha John Ndewele
alisema kuwa mgogoro huo ulianza miezi kadhaa iliyopita kwa viongozi wa kijiji
cha kilwa kutowatambua huku wakidai kuwa wavuvi hao hawatoi michango ya ujenzi
wa miradi ya maendeleo pamoja na kutoshiriki katika shughuri za maendeleo.
Alisema
asilimia 80 ya wavuvi katika forodha hiyo ambayo ni kubwa kuliko zote wilayani
humo ni kutoka tarafa ya mwambao wilayani Ludewa ambao wapo zaidi ya 50
wanaofanya shughuri za uvuvi katika forodha hiyo iliyopo katika kitongojin cha
njisi kijiji cha Kirwa kwa kufuata taratibu zote za idara ya maliasili na uvuvi.
Alisema
kuwa baadhi ya wananchi pamoja na viongozi wa kijiji hicho wamekuwa na wivu wa
kimasilahi na wavuvi kutokana na wavuvi kutoka wilaya ya Ludewa kuwazidi wazawa
kipato cha majini hadi kufikia hatua ya kuwatafutia tuhuma za kuwatuhumu kuwa
hawashiriki katika shughuri za maendeleo,wanatembea na wake zao na kutoa
lugha za matusi wa wazawa kitu ambacho si kweli.
Ndewele
aliongeza kuwa kitu kitu kinachowauma zaidi ni kutokana na wao kuchukua ubia na
halmashauri ya wilaya hiyo kutoza ushuru ambapo kila nyavu ikiingia kuvua
inatozwa Tsh,1000 huku mnunuzi utozwa Tsh,500 kila mmoja huku idadi ya nyavu
zikiwa 53 na wanunuzi wanaofika kununua samaki ni zaidi ya 200.
Alisema
kuwa wao kama wavuvi wapo kisheria na wamekuwa wakilipa zaidi ya mil,6 kwa
ajili ya leseni za nyavu pamoja na mitunbwi,ambapo nyavu moja inakuwa na wavuvi
5 mitumbwi 3 katika usajili hutoa Tsh,120,000,yaani nyavu 80,000 mtumbwi mmoja
32,000 mvuvi mmoja 7500 mbali na ushuru wa mtu mmoja mmoja na adhabu mbalimbali
huku kijiji kikipewa 150.000 kwa mwaka kama ruzuku.
Baada ya
kutokea kwa mgogoro huo viongozi wa forodha walipeleka malalamiko kwa mkuu wa
wilaya Magret Marenga ambaye naye alimtuma Afisa Tarafa wa unyakyusa Hery
William ambaye tar,8/5/2014 alifika kijijini humo na kufanya mkutano wa pamoja
na kusikiliza pande zote mbili huku kijiji kikitaka wavuvi hao wavunje makambi
uwepo mwalo na wao waishi uraiani ili waweze kushirikiana katika shughuri za
maendeleo.
Alisema afisa huyo aliwaeleza wananchi kuwa wawape
mwezi mmoja siku ya tar,8/6/2014 ili wavuvi hao waweze kujipanga zaidi kuliko
kutoa amri ya kuwaondoa maeneo hao kighafra wakati hawana maeneo mengine ya
kuishi zaidi ya kambini,na kuwa siku hiyo muafaka wa jambo hilo haukufikiwa
huku wao wakiendelea kuishi katika makambi hayo na kupokea vitisho kutoka kwa
wanakijiji hao.
Mwenyekiti wa kitongoji hicho cha njisi Ndenge
Mwakilasa alikiri kuwepo na mgogoro huo na kudai kuwa wavuvi hao wamekuwa
hawashiriki katika shughuri za maendeleo huku wakidai kuwa wao wapo chini ya
maliasili na si Kijiji kitu ambacho kimeleta utata na kuwa walifanya mikutano
ya kuwataka waishi vijijini huku ziwani wawe wanaenda kuvua na kurudi na si
kweka makambi kitu ambacho wao wanakipinga.
Mwenye
kiti wa kijiji cha Kilwa Padon Mwangwala kwa upande wake alidai kuwa uongozi wa
kijiji chake ulipokea muhtasari wa kikao cha kitongoji kikitaka wavuvi hao
wahamie vijijini na kuvunja makambi na wao kupeleka kwenye kata na kukaa vikao
vya (WDC) na kupeleka muhtasari kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ambayo ilitoa
tamko katika mkutano kuwa ifikapo tar.8/6/2014 wavuvi wawe wamehamia vijijini.
Alisema wao wakiwa wanasubiri tarehe hiyo walishangaa
kuona mkuu wa wilaya ya Kyela Magreti malenga siku ya tar,6/6/2014 akienda kwa
wavuvi na kuwaeleza kuwa wasiondoke badara ya kuitisha mkutano wa pande zote
mbili ili atatue mgogoro yeye ndiyo kachochea mgogoro na kutuzarau sisi ambao
ndiyo viongozi wa sehemu husika.
Aliongeza
kuwa ilipofika tar,7/6/2014 jeshi la polisi wilayani lilifika kijijini humo na
kumkamata Nickson Mwakasonda kwa madai kuwa amefunga barabara ya kutoka kwake
kwenda ziwani wakati njia hiyo imepita katikati ya mji wake nay eye aliamua
kuifunga ili apande migomba,na hadi sasa kijana huyo yupo lumande.
Kutokana na hali hiyo viongozi wa kijiji hicho
wametishia kujiuzuru nyadhifa zao kwa madai kuwa hawatendewi haki,na katika
sekeseke hilo zaidi ya wavuvi 100 kutoka wilayani Ludewa wameondoka maeneo hayo
wakihofia usalama wao.
Afisa
maliasili uvuvi na utalii wilayani Kyela Fedinand Mwaseba aligoma
kulizungumzia sakata hilo na kudai kuwa lipo chini ya mkuu wa wilaya,huku mkuu
wa wilaya Magret malenga hakuweza kupatikana ofisini kwake kutokana na kuwa
katika mapumziko mafupi na alipo pigiwa simu yake haikupatikana.
Na, Lumemo blog
Post a Comment
Post a Comment