ASKOFU wa TAG Jimbo la Mbeya Kaskazini, Dk. Donald Mwanjoka akiwakabidhi vyandarua 100 viongozi wa Hospitali ya mkoa Mbeya |
ASKOFU wa TAG Jimbo la Mbeya Kaskazini, Dk. Donald Mwanjoka akihutubia katika hospitali ya mkoa Mbeya |
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Dk Seif Mhina akimkaribisha mgeni rasmi |
Dr. Leonard Maboko Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii ya TAG ambae pia ni Mkurugenzi wa NIMR, akitoa neno kwa wageni |
Baadhi ya watumishi wa Hospitali ya mkoa Mbeya wakimsikiliza mgeni rasmi |
Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya Dk. Gloria Mbwile, Alilipongeza Kanisa kwa kutimiza miaka 75 tangu kuanzishwa kwake nchini Tanzania pamoja na kutambua umuhimu wa huduma za jamii. |
ASKOFU wa TAG Jimbo la Mbeya Kaskazini,
Dk. Donald Mwanjoka amekabidhi vyandarua 100 katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya
ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya jubilee ya miaka 75 ya kuanzishwa kwa kanisa
hilo.
Akizungumza wakati wa zoezi la
kukabidhi vyandarua hivyo, Askofu huyo alisema zoezi hilo linafanyika kutokana
na Kanisa hilo kitaifa kuanzishwa Mkoa wa Mbeya pamoja na sherehe kufanyika
kitaifa Mkoa wa Mbeya.
Awali akitoa utambulisho katika hafla
hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Mwenyekiti wa
Kamati ya Huduma za Jamii wa TAG, Dk. Leonard Maboko, ambaye pia ni Mkurugenzi
wa NMR, alisema mbali na askofu huyo kukabidhi vyandarua hivyo katika hospitali
hiyo pia Maaskofu wengine wametawanyika katika Hospitali za Jiji la Mbeya na Wilaya
ya Mbeya kwa ajili ya kukabidhi vyandarua hivyo.
Naye Mganga mfawidhi wa Hospitali ya
Mkoa wa Mbeya Dk. Gloria Mbwile, Alilipongeza Kanisa kwa kutimiza miaka 75
tangu kuanzishwa kwake nchini Tanzania pamoja na kutambua umuhimu wa huduma za
jamii.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa
Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Dk Seif Mhina aliwashukuru Kanisa kwa msaada na
kuongeza kuwa kitendo hicho ni kutekeleza mfumo wa serikali wa kuzishirikisha
sekta binafsi katika mfumo wa (PPP).
Aliongeza kuwa hivi sasa serikali inakabiliwa
na kutekeleza mpango wa mileniawa kupunguza vifo vya mama na mtoto kutokana na
Malaria hivyo kitendo cha Kanisa kutoa msaada huo ni kuisaidia Serikali kwa
kutoa vyandarua bure tofauti na serikali ya kutoa kwa mfumo wa hati Punguzo.
Post a Comment
Post a Comment