GuidePedia

0


Meza kuu ya viongozi wa Jumuiya ya Ahmadiyya pamoja na Afisa maendeleo ya jamii kabla ya kukabidhi msaada katika kituo cha Yatima Songwe
Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Mbeya, Bevarine Mgoda akizungumza na watoto kabla ya kukabidhi msaada 
Kiongozi wa wazee wa Jumuiya ya Ahmadiyya Mkoa wa Mbeya, Hafidhu Mgagi akimkaribisha Shehe mkuu kuzungumza na watoto kabla ya kukabidhi misaada
Shehe Mkuu wa Kanda ya Mbeya wa Jumuiya ya Kiislamu ya Ahmadiyya akizungumza jambo na watoto wanaolelewa  katika kituo hicho
Watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto yatima kilichopo Songwe wakisikiliza kwa makini 
Viongozi wa Jumuiya ya Kiislamu ya Ahmadiyya wakikabidhi misaada mbali mbali kwa walezi wa kituo cha Yatima Songwe Mbeya
Watoto wakiwa pamoja na baadhi ya vitu walivyokabidhiwa na jumuiya ya Ahmadiyya Mbeya
KATIKA kuhitimisha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya, Mkoa wa Mbeya imefanya ziara ya kutembelea vituo vya watoto Yatima na watoto wi moja wenye mahitaji maalumu.
Ziara hiyo ilifanyika juzi ambapo viongozi wa Jumuiya hiyo wakifuatana na Shehe mkuu wa Kanda ya Mbeya, Karim-Ud-Din Shams walitembelea kituo cha Malezi na Mafunzo ya Watoto Yatima Good Samaritan Orphanage Trust kilichopo Songwe Wilaya ya Mbeya mkoani hapa na kutoa msaada wa bidhaa mbali mbali.
Akimkaribisha Shehe Mkuu kukabidhi zawadi hizo, Kiongozi wa baraza la Wazee wa Jumuiya ya Ahmadiyya Mkoa wa Mbeya, Hafidhu Mgagi, alisema Waumini wa dini ya Kiislamu duniani kote wako kwenye mfungo wa mwezi wa Ramadhani ambao uko ukingoni kuisha, hivyo Jumuiya hiyo imeona ni vema ikashiriki na Yatima katika sikukuu ya Idi.
Kwa upande wake Shehe Mkuu wa Kanda ya Mbeya inayounda mikoa wa Mbeya, Rukwa na Katavi, Karim Shams alisema kutembelea Yatima ni moja ya maandiko matakatifu ya Mungu yanayomtaka kila mwislamu kuwajali watoto Yatima na wasiojiweza ili waweze kupata thawabu.
Alisema lengo la kutembelea kituo hicho ni kusherekea na watoto sikukuu ya Idd itakayofanyika hivi karibuni baada ya kumaliza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani na kuongeza kuwa hayo ni moja ya matakwa ya maagizo ya dini ya kushirikiana na yatima ili kupata thawabu siku ya kiama.
Katika hafla hiyo Jumuiya hiyo ili kabidhi bidhaa mbali mbali zikiwemo Sukari, Mchele, mafuta ya kupikia na sabuni za kufulia ambazo thamani yake haikujulikana mara moja kutokana na kugawanywa katika sehemu zingine zenye mahitaji.
Kwa upande wake Mlezi wa Kituo hicho, Yusufu Salali, alitoa shukrani kwa Jumuiya hiyo kwa kuwajali watoto wanaolelewa katika kituo hicho licha ya kumulikiwa na dini ya kikristu lakini Waislamu hawakufanya ubaguzi na kutoa misaada bila kujali udini.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya jamii Wilaya ya Mbeya,Bevarine Mgoda, alisema sula la watoto yatima katika Wilaya yake linakabiliwa na changamoto nyingi hivyo alitoa shukrani kwa wadau kuendelea kuwajali zikiwemo taasisi za serikali na sio kuiachia Serikali pekee.
Alizitaja baadhi ya Changamoto hizo kuwa ni pamoja na ufinyu wa usafiri wa kuweza kuwatembelea watoto yatima popote walipo hatan kushughulikia maswala yao yanapojitokeza kwa ghafla hususani vijijini ambako vitendo vya ukatili dhidi ya watoto ni vingi.
Aliongeza kuwa changamoto nyingine ni ukosefu wa elimu kwa wanajamii ambao kutokana na hali hiyo wamekosa uzalendo wa kuona kila mtu anaweza kuhudumia mtoto yatima bila kujali katika katika familia ya aina gani.

Post a Comment

 
Top