MAITI 6 kati ya 8 waliofia majini katika ziwa Tanganyika
baada ya boti mbili kugongana julai 7 mwaka huu katika kata ya Korongwe
wilayani Nkasi mkoani Rukwa zimepatikana huku jitihada za kutafuta miili
mingine ikiendelea.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake katibu tawala wa wilaya Nkasi mkoani Rukwa
(DAS)Festo Chonya amesema toka boti hizo zigongane julai 7 kati ya boti
ya abiria na ile ya wavuvi na kupelekea boti ya abiria kuzama watu nane
walifia majini na jitihada zilifanywa za kuanza kuitafuta miili hiyo ambapo
mpaka hivi sasa ni miili 6 ndiyo iliyopatikanika.
Alisema
kutokana na kuwa miili ya watu hao ilikua imeharibika sana serikali ilikataa
kusafirisha maiti na badala yake serikali imetenga eneo maalumu katika kijiji
cha Korongwe ambapo miili yote iliyopatikana imezikwa katika kijiji hicho
cha Korongwe.
Katibu
tawala huyo wa wilaya ametaja majina ya maiti ambao wamepatikana hadi hivi sasa
kuwa ni ya Fatuma Masud (46) mkazi wa Mwanza ambaye alikua ni
mfanyabiashara,Cleophas Mwanandenje (47) mkazi wa Kijiji cha Korongwe na
mtoto Edward Kangeme (8) mkazi wa kijiji hicho cha Korongwe wilayani Nkasi.
Wengine
ni Anastazia Alex (7) wa Korongwe,Emmanuel Manyika (28) mkazi wa Mpege na
Beneth Kasomo (54) wa mkazi wa Challa na kuwa jitihada za kuitafuta miili ya
watu wawili waliokufa katika ajali hiyo inaendelea.
Chonya
alifafanua kuwa ajali hiyo ilitokea usiku wa tarehe 7 mwezi huu majira ya saa 3
usiku ambapo boti ya abiria iliyokua imetokea katika kata ya kirando
walipogongana na boti la wavuvi iliyopelekea boti la abiria kupasuka na kuzama
na kupelekea vifo hivyo vya watu 8.
Na, Lumemo blog
Post a Comment
Post a Comment