GuidePedia

0

Gabriel Mbwile akiwasilisha mrejesho wa kikao cha kwanza kabla hajachaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho.

Hapa baada ya  kufanya uchaguzi ambapo hapo viongozi wote wanne wamepatika aliyevaa shati jeupe ni katibu Fredy Jackson aliyevaa shati jekundu mwenyekiti Gabrieli Mbwile aliyejifunga kilemba mtunza azina na wapembeni yake amemuwakilisha mwenyekiti msaiduizi Fredy harbet.







Baadhi ya wanachama wakiwasikiliza viongozi wao wakipendekeza majina ya wajumbe ili yapigiwe kura.

 

Hatimae chama cha watangazaji wa radio na DJS mkoa wa mbeya chaanzishwa rasmi na kuhudhuriwa na watangazaji zaidi ya 35 katika uchaguzi wa viongozi watakaosimamia shughuli za chama hicho.

 
Chama hicho kimefanya uchaguzi mbali mbali leo katika ukumbi wa G12 ambapo zamani ulijulikana kama Nebana na kwamba katika uongozi huo ni pamoja na mwenyekiti, katibu mwenyekiti mzaidizi na wajumbe wane.

Aidha katika kuchagua nafasi ya uenyekiti aliyeibuka na kuwa mwenyekiti ni Gabriel Mbwile kutoka Bomba fm nafasi ya katibu ni Fredy Jackson kutoka Mbeya fm mwenyekiti msaidizi Fredy Harbet kutoka Bomba fm.

Kwaupande wa baadhi ya wajumbe wanne waliyochaguliwa ni pamoja na Stanslausi Lambati kutoka Mbeya fm, Rashidi Abdalah (Shibobo) kutoka Generation fm, na Sara Mande kutoka Generation fm.

 Nae mwenyekiti wa chama hicho  Gabriel Mbwile amesema amesema moja kati ya majukumu yake  atakayoyafanya ni kuhakikisha watangazaji wote wa mkpoa wa mbeya wanpata mkataba kutoka kwa bwajiri wao ili wawe na ajira ya kudumu  tofauti na ilivyo sasa.

Hata hivyo Mbwile amehairisha kikao hicho mpaka tarehe 1/08/ 2014 ili kutoa utaratibu wa chama pamoja na kutengeneza katiba ya itakayowaongoza katika chama.
               
                            Na, Lumemo blog.


 


Post a Comment

 
Top