Mbunge wa jimbo la songwe Philipo Mulugo iliyesimama akiongea na washiriki wa mafunzo hayo.
Mbunge wa viti maalumu Dr, Mery Mwanjelwa na Mbunge wa jimbo la songwe Philipo Mulugo wakicheza wimbo uliyoimbwa na washiriki wa semina katika ukumbi OTTU.
Mery Mwanjelwa na Philipo Mulugo wakibadilishana mawazo mara baada ya kuingia katika ukumbi huo
Washiriki wa mafunzo wakimsikiliza mgeni rasmi katika ukumbi huo mara baada ya wasili.
Moja kati ya washiriki wa mafunzo Bi, Mery Malema akisoma risala waliyoiandaa kwa mgeni rasmi
Mkufunzi wa mafunzo hayo Bw, Israel Ilundu akiwaelekeza jambo washiriki kabla ya kuwasili mgeni rasmi.
Mgeni rasmi Philipo Mulugo akikabidhi zawadi zilizoandaliwa na washiriki kama shukrani kwa baadhi ya viongozi akiwemo mkufunzi na Mery Mwanjelwa.
Hii ni meza iliyoandaliwa kwaajili ya vyakula mara baada ya kumaliza kufunga mafunzo hayo.
Viongozi wanawake wa nyanja mbali mbali katika chama cha
Mapinduzi CCM mkoani mbeya wamepatiwa mafunzo yanayohusu mbinu za kukabiliana
na changamoto za uongozi pindi wawapo marakani.
Mafunzo hayo yaliyoendeshwa kwa muda wa siku tatu katika
ukumbi wa OTTU kabwe jijini mbeya yaliandaliwa na mbunge wa viti maalumu mkoa
wa mbeya Dr. Mery Mwanjelwa ambapo jana ndiyo kilele chake.
Katika kufunga mafunzo hayo mgeni rasmi aliyealikwa kwaajili
ya kufunga ni Mbunge wa jimbo la songwe Mh, Philipo Mulugo ambapo katika kujibu
risala iliyoandaliwa na washiriki wa mafunzo hayo aliwataka washiriki kutumia vyema
elimu waliyoipata na kuacha kurubuniwa na baadhi ya wanasiasa wenzao wasio aminifu.
Aidha Mulugo amesema kumekuwa na tabia kwa baadhi ya
wanachama wa chama cha CCM kukubali kununuliwa na viongozi ambao siyo
waadilifu, hivyo kupitia madfunzo hayo anaamini kuwa kutakuwa na mabadiliko
makubwa kufuatia uchaguzi mkuu ujao.
Mulugo alimpongeza Mbenge wa viti maalumu Mh, Mery Mwanjelwa
kwakuwaandilia wanawake hao mafunzo hayo kwani endapo watayafanyia kazi ipasavyo
yataleta tija kwao na jamii kwa ujula.
Awali washiriki wa mafunzo katika risala yao waliyoiandaa
walimshukuru Mbunge Mwanjelwa kwakuwaandalia mafunzo na kuahidi kupitia mafunzo
hayo hawatarubuniwa na viongozi wasio adilifu na kumtaka mbunge Mwanjelwa
kuendelea na moyo huo wa kujitolea kwani mafunzo kama hayo mara nyingi yamekuwa
yakitolewa kwa malipo lakini kwakupitia Mbunge huyo wameyapata bure.
Kwaupande wake Mbunge wa viti maalumu Mh, Dr Mery Mwanujelwa amesema
amefurahishwa sana na washiriki hao namna walivyoweza kupokea kwa haraka kitu
ambacho walichokuwa wanafundishwa pamoja na wakufunzi waliyokuwa wakiwafundisha
washiriki hao kutoka katika shirika la FACE la Ujerman linalojihusisha na
mafunzo ya utawala bora kwa viongozi.
Na, Lumemo blog
Post a Comment
Post a Comment