SERIKALI ya Kijiji cha Ndaga kata ya Isongole wilayani
Rungwe mkoani Mbeya imetumia zaidi ya milioni 90 kujenga miradi ya maendeleo ya
kijiji hicho ikiwemo Shule ya msingi,ofisi ya kijiji na vyoo katika soko la
kijiji kwa kutumia fedha zao zilizotokana na vyanzo viwili vya mapato vilivyopo
kijijini humo.
Akizungumza
kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana kwenye viwanja vya ofisi ya
kijiji hicho mwenyekiti wa kijiji hicho Paulos Zambi alisema kuwa kijiji chake
kinategemea ushuru unaotokana na zao la viazi mviringo na mahindi na katika
makusanyo hayo wameamua kujenga miradi ya maendeleo kwa faida ya kijiji na
wilaya kwa ujumla ili kuondoa changamoto zilizopo.
Alisema
kuwa kwa upande wa shule ya msingi Goye yenye vyuimba sita vya madarasa
wametumia Tsh,60.000,000/- kwa mchanganuo ufuatao,Tsh,9,000,000/- zilitokana na
harambee,Tsh,7,000,000/-michango ya wanakijiji,Tsh,30,000,000/-miradi ya kijiji
na Tsh,14,000,000/-kutoka miradi isiyorasmi ikiwemo adhabu ndogondogo kwa wale
walinaokiuka taratibu zilizowekwa na kijiji hicho.
Zambi
aliyechaguliwa uenyekiti kwa tiketi ya CUF aliendelea kusema kuwa idadi hiyo ya
ujenzi iliyotajwa imejumuishwa pamoja na Tsh,20,000.000/-zilitumika kulipa fidia
kwa mtu mwenye eneo palipojengwa shule hiyo na kufikia idadi hiyo ya Mil,60 na
kuwa kilichobaki ni kujenga vyoo pamoja na kupiga plasta jingo zima jitihada
ambazo tayari wamezianza.
Kwa upande wa ofisi ya Kijiji Mwanyekiti huyo alisema
kuwa kijiji hicho kilianza kujenga ofisi hiyo tarehe 2/11/2011 ambapo wametumia
Tsh,32,000,000/-ambapo Tsh,11,000,000/-zilitokana na miradi rasmi ya kijiji na
Tsh,21,000,000/- zilitokana na miradi isiyorasmi ikiwamo ya adhabu ndogo ndogo
kwa wale waliokuwa wakikiuka taratibu zilizowekwa na kijiji.
Aidha mwenyekiti huyo aliongeza kuwa serikali yake
ilitumia Tsh,4,500,000/- kujenga choo katika maeneo yanayotumika katika
shughuri za kijamii ikiwemo soko la kijiji na Tsh,4,50,000 zimetumika kujenga
choo kwenye makao makuu ya kijiji hicho ili kupungunza adha waliyokuwa
wakiipata wananchi wa kijiji hicho na jumla ya ujenzi wa vyoo hivyo ni
Tsh,9,000,000/- na kuondoa kero zilizokuwepo kijijini hapo kwa fedha zao bila
kupata msaada serikalini.
Afisa mtendaji wa kata hiyo Laiponia Mwakisambwe
alisema kuwa viongozi wa kijiji hicho kwa kushirikiana na wananchi wameweza
kufanya mambo makubwa ya kukamirisha miradi hiyo kwa nguvu zao na kuwa baada ya
ujenzi wa shule ya msingi kukamilika wanampango wa kujenga shule ya sekondari ya
kijiji siku za usoni ili kuondoa usumbufu wanaoupata wanafunzi wa kutembea
umbali mrefu kwenda shule na kuongeza kiwango cha elimu kijijini hapo na kata
kwa ujumla.
Afisa
elimu msingi wa wilaya ya Rungwe Enock Kyando mbali na kupongeza juhudi hizo
zilizofanywa na kijiji hicho alisema kuwa atapeleka waalimu wa kutosha pindi tu
viongozi wa kijiji hicho watakapojenga vyoo na kuwa hatua waliyoifanya inapaswa
kuigwa na vijiji vingine ambavyo vimekuwa nyuma kufanya maendeleo yakiisubiri
serikali ifanye.
Mkuu wa
wilaya hiyo Chripin Meela kwa upande wake alimuagiza afisa elimu kuwa ifikapo
tarehe 1/1/2015 shule hiyo iweimeanza kupokea wanafunzi na kuwa serikali
itaangalia mahali walipokwama ili iweze kusaidia katika harakati hizo za kijiji
za kukamirisha miradi hiyo.
Katika
mkutano huo ulioambatana na ufunguzi wa miradi hiyo pamoja na sherehe watu
mbalimbali na wageni waalikwa walipata nafasi ya kusema ikiwa ni pamoja na
kutoa kile walichokuwa nacho ili kusaidia jitihada hizo ambapo fedha taslim
Tsh,9,26,400 zilipatikana pamoja na mifuko 79 ya saruji yenye thamani ya
Tsh,mil 1,3,43,000/-.
Na, Lumemo blog
Post a Comment
Post a Comment