MAHAKAMA ya wilaya Nkasi mkoani Rukwa imemhukumu
kwenda jela miaka 30 Martin Misala (20) mkazi wa kijiji cha Katongolo kata ya
Kipili wilayani Nkasi kwa kosa la kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka (16) na
kumsababishia maumivu makali
Akitoa hukumu hiyo hakimu mfawidhi wa mahakama ya
wilaya Nkasi Ramadhan Rugemalila alisema kuwa anamtia hatiani mtuhumiwa baada
ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka pasipo kuacha shaka
yoyote na kuwa anamtia hatiani kwa kosa hilo la ubakaji chini ya kifungu cha
sheria No,130(1)(2)
Upande wa mashitaka ukiongozwa na mwendesha mashitaka
wa jeshi la polisi Hamimu Gwelo uliiambia mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa huyo
alitenda kosa hilo la kumbaka binti huyo oktoba (20) mwaka jana majira ya saa 6
usiku katika kijiji hicho cha Katongolo walipokua wametokea disko.
Katika kesi hiyo upande wa mashitaka uliitisha
mashahidi wanne ambao walitoa ushahidi wao huku mtuhumiwa akikosa watu wa
kumtetea na ndipo mahakama ilipoamua kumtia hatiani kwa kosa hilo baada ya
kuridhishwa na maelezo yaliyotolewa na upande wa mashitaka
Kutokana na kosa hilo upande wa mashitaka uliiomba
mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa huyo ili liwe ni fundisho na kwa
wengine baada ya vitendo kama hivyo kushamiri wilayani Nkasi katika siku za
hivi karibuni
Mtuhumiwa kwa upande wake aliiomba mahakama hiyo
kumpunguzia adhabu kwa sababu yeye hilo ni kosa lake la kwanza lakini pia
familia yake inamtegemea sana
Wakati huohuo mahakama hiyo imemhukumu kwenda jela
miaka 15 Masanja Lupinga mkazi wa kijiji cha Katani kwa kosa la uwizi wa
ng’ombe.
Upande wa mashitaka uliieleza mahakama hiyo kuwa
septemba 16 mwaka jana mtuhumiwa huyo aliiba ng’ombe 8 za Lauliano Kayoka mkazi
wa kijiji cha Ntemba
Alisema ngombe hao walikamatwa mjini Sumbawanga pamoja
mtuhumiwa huyo wakizipeleka machinjioni kwa ajiri ya kwenda kuwauza
Upande wa mashitaka uliita mashahidi 8 wakiwemo na
ng’ombe hao kama kielelezo mahakamani na kwa kuzingatia kuwa mtuhumiwa hili si
kosa lake la kwanza mahakama hiyo ilimtia hatiani kwenda kutumikia kifungo cha
miaka 15 jela chini ya kifungu No,168 na 165 ya kanuni ya adhabu sura ya 16.
Na Lumemo blog
Post a Comment
Post a Comment