Mkuu wa mkoa wa mbeya Mh, Abas Kandoro akiongea na waandishi wa hbari ofisini kwake.
Baadhi ya watalaam waliyoandaa maadhimisho ya siku ya kupinga madawa ya kulevya.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa mbeya Mh, Abas Kandoro.
MAadhimisho ya kilele cha kudhibiti na
kupambana na madawa ya kulevya yanatarajiwa kufanyika kitaifa mkoani Mbeya
ambapo Makamu wa Raisi, Dk. Mohamed Gharib Bilal atakuwa mgeni rasmi.
Maadhimisho hayo yatafanyika katika
viwanya vya Shule ya Msingi RuandaNzovwe Ilomba jijini Mbeya Juni 26, Mwaka
huu.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa Habari,
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, amesema lengo la maadhimisho hayo ni kuiasa
jamii na kuikumbusha kuhusu athari za matumizi ya madawa ya kulevya kwa kukataa
kuuza wala kuingiza nchini.
Amesema Mkoa wa Mbeya umepata nafasi ya
kuandaa sherehe hizo kutokana na kuwa Mkoa unaopakana na nchi jirani hivyo
kuwepo kwa mwingiliano mkubwa na upishaji wa madawa ya kulevya kutoka nchi za
Nje ambazo zinapakana na Mkoa wa Mbeya.
Kandoro amesema kauli mbiu ya Mwaka huu
ni “Uteja wa dawa za kulevya unazuilika na kutibika chukua hatua”.
Aliongeza kuwa maadhimisho hayo yalianza
Juni 24, Mwaka huu na kufikia kilele Juni 26, Mwaka huu ambapo shughuli mbali
mbali zimaenza kufanyika zikiwemo za upimaji, utoaji elimu na kutoa matibabu
kwa waathirika wa madawa ya kulevya.
Aidha amezitaja baadhi ya taasisi
zinazoendelea na zoezi hilo kuwa ni pamoja na Mkemia mkuu wa Serikali, Mamlaka
ya chakula na dawa(TFDA),Hospitali ya Mkoa wa Mbeya,Hospitali ya Rufaa ya Mbeya,Mashirika
binafsi na Jeshi la Polisi.
Na, Lumemo blog
Post a Comment
Post a Comment