GuidePedia

0

John Mwambigija mwenyekiti wa CHADEMA Mbeya mjini aliyevaa kofia ilyokuwa na mchanganyiko wa rangi nyekundu akisisitiza jambo fulani kwa waandishi wahabari.

Baraka Mwakyabula katibu mwenezi wa CHADEMA mbeya mjini akisoma maelezo fulani kwa waandishi wa habari.





Viongozi wa CHADEMA wakiwa na waandishi wa habari katika kikao chao ndani ya Hotel ya Mbeya peak.

 

Mjumbe wa baraza  la kuu la  taifa   kupitia chama cha   Chadema  John mwambigija   amewataka wanachi kuwa makini na baadhi ya  watu ambao wamekwa  wakizunguka  kwa   kueneza  kashifa mbaya  juu ya chama  hicho.

Hayo yamejili wakati wa  kikao maalumu  na waandishi  wa habari ambapo amesema kuna baadhi ya watu wamekuwa wakizunguka  katika  sehemu mbali mbali nchini  kwa  kutoa  kashifa  mbaya  kwa wananchi kwamba chama cha chadema kinamatumizi mabaya ya fedha jambo ambalo siyo la kweli.

Amesema mpaka sasa wamejipanga   kuzunguka katika maeneo tofauti mkoani hapa   kwakuwakamata watu hao kwa lengo la kuweza  kuwafisha katika vyombo  vya kisheria.

Amesema katika kuhakikisha  chama   hicho  kinasonga  mbele  wamefanikiwa  kununua magari na pikipi ambayo   mpaka  sasa  yanaendelea  kutumika  nchi nzima   kwa matumizi ya  chama  husika  na kusema  luzuku  imeendelea  kufanya kazi yake  vizuri  bila  kufanya  ubadhilifu wowote na  viongozi  husika.

Kwa upande katibu mwenezi wa chadema mbeya mjini Baraka Mwakyabula amesema kuhusu uchaguzi wa diwani katika kata ya Ntembela chadema imejipanga kuhakikisha chama chao kinashinda kwaasilimia mia.

Hata hivyo ametoa angalizo kwa chama cha mapindizi ccm kuacha vitendo vya kuchakachua matokeo kwani wao wamejipanga vyakutosho juu ya uchaguzi huo.

                                          Na, Lumemo blog


Post a Comment

 
Top