Katibu wa madrasa ya swalihina Bi, Fatuma Almasi aliyesimama.
Mwalimu wa madrasa (USTADHATI) Bi, Zaituni Hamza aliyekaa katika kochi akipokea simu.
Wanawake wa kiislam mkoa wa mbeya wametakiwa kuwa waadilifu na kuacha vitendo viovu visivyo mpendeza mungu hasa katika mfungo mtukufu wa ramadhani
Hayo yamesemwa na katibu wa kikundi cha kiislam Bi, Fatuma Almasi kilichopo ilomba jijini mbeya wakati wa hafla ya kuukaribisha mwenzi wa ramadhani iliyofanyika nyumbani kwa Bi, Zaituni Hamza ambaye pia ni mwalimu wa madrasa hiyo.
Aidha Bi, Fatuma amesema kumekuwa na tabia za baadhi ya wanawake kufanya vitendo am,bavyo havimpendezi mungu na kwamba vitendo hivyo vinapelekea hata kuharibu jamii
Bi, Fatuma amevitaja baadhi ya vitendo hivyo ni pamoja na kupaka wanja, kuweka rasta na kuvaa vimini wakati wa mwezi wa ramadhani.
Kwa upande wake mwalimu wa madrasa hiyo Bi. Zaituni Hamza amesema lengo la kuanzisha madarasa ni kutoa elimu inayomuhusu mungu kwa wanawake wa kiislam na watoto.
Hata hivyo Bi, Zaituni amewataka wanawake wa kiislam kujitokeza bkwa wingi kwaajili ya kuwapeleka watoto wao pamoja na wao wenyewe ili kupata elimu ya mungu na kuishi katika maadili ya kimungu.
Post a Comment
Post a Comment