Huyu bibi ni mmoja kati ya wakazi ambao nyumba zao zipo karibu na dampo hilo pamoja na huyo mzee aliyesimama pia huyo mzee alikuwa akifanya biashara ya bucha.
Diwani wa kata ya Igurusi Mh, Keneth Ndingo
Wakazi wa kitongoji cha Zahanati kijiji cha Igurusi wilaya ya
mbarali mkoani Mbeya wameulalamikia uongozi wa serikali ya kijiji hicho kwa
kushindwa kuondoa kwa wakatitaka
zilizopo katika dampo ambalo limejengwa karibu na makazi ya watu.
Wakiongea na blog hii wakazi hao wamesema tangu kujengwa kwa
dampo hilo yapata zaidi ya miaka nne sasa serikali haijawahi kuondoa taka hizo
na kuzimaliza isipokuwa imekuwa ikiziondoa na kuzibakiza.
Kufuatia hali hiyo ndio imekuwa chanzo kikubwa cha kujaa kwa
haraka kwa dampo hilo hivyo kusababisha taka kuzagaa mpaka katika makazi yao
ambapo huwapa kero kubwa katika kufanya kazi zao kutokana na harufu mbaya
inayotoka katika dampo hilo.
Aidha wamesema eneo hilo miaka ya nyuma walikuwa wakifanya
biashara mbali mbali ikiwemo chakula na mabucha ya nyama ya ng’ombe hivyo tangu
kujengwa kwa dampo hilo ufanyaji wa biashara umekuwa ni mgumu kutokana na taka
zinazotupwa katika dampo hilo hivyo wafanya wafanyabishara hao kuamua kuondoka
na kwenda kutafuta sehemu nyingine za kufanyia bishara zao.
Hata hivyo wakazi hao wameiomba serikali kuondoa dampo hilo kutokana
na kushindwa kuondoa taka hizo ili wao waendelee na shughuli zao za kujitafutia
kipato.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho Mussa Mwanjejele amekiri
kuwepo kwa hali hiyo na kusema sababu ya kuchelewa kwa uondoaji wa taka hizo ni
halmashauri kuchelewa kutoa fedha kwaajili ya kuondolea taka hizo.
Amesema mpaka kufikia kuondoa taka hizo ni lazima wakapigekelele halmashauri ndipo wapewe fedha za
kuondola taka lakini bado fedha wanazopewa hazikidhi uondoaji wa taka zote
hivyo kusababisha taka zingine kubaki katika dampo hilo.
Hata hivyo Blog hii ilimtafuta Diwani wa kata ya Igurusi
Keneth Ndingo kwa njia ya simu ili kupata ufafanuzi kuhusu jambo hilo Diwani
huyo alipotafutwa amesema ni kweli tatizo hilo lipo na kusema yeye yuko
safarini kikazi na kwamba akirudi atalifuatilia kwa ukalibu ili kumaliza kwani limekuwa
la muda mrefua sasa.
Post a Comment
Post a Comment