MKAZI
wa kijiji cha Kandete kata ya Kandete katika halmashauri ya Busokelo
wilayani.Rungwe Mbeya Suzana Osea (25) amejikuta katika wakati mgumu baada ya
kuolewa na wanaume wawili na kuzua tafrani kijijini humo.
Akizungumza
na kituo hiki jana Omari Njela mbaye ndiye anayedaiwa kuwa ni mume halali
wa mwanamke huyo alisema alimuoa mwanamke huyo miaka miwili iliyopita na tayari
amezaa naye mtoto mwenye umri wa miezi mitatu.
Alisema
wiki iliyopita binti huyo alimtelekeza mtoto ndani kwa siku mzima na kufunga
mlango kwa nje kasha kuchukua uamuzi mgumu wa kuolewa na mwanaume mungine huku
akijua kuwa yeye ni mke wa mtu na kuwa wakati kitendo hicho kinafanyika yeye
alikuwa safarini.
Alisema
baada ya mtoto kufungiwa mlango alianza kulia kwa uchungu na ndipo majirani
waliposhituka na kulazimika kuvunja mlango na kuingia ndani kasha kumkabidhi
mtoto huyo kwenye serikali ya kijiji hicho kupitia kwa afisa mtendaji wa kata.
Afisa
mtendaji wa kata ya Kandete Huruma Mwakyusa mbali na kukiri ofisi yake kumpokea
mtoto huyo alidai kuwa aliamuru wanaume wote pamoja na mwanamke wakamatwe na
baada ya kukamatwa serikali ya kijiji hicho kiliketi na kutafuta ufumbuzi wa
suala hilo.
Aliongeza
kuwa katika shauri hilo
mwanamke huyo alishindwa kumtambua mwenye uhalali na mtoto huyo na kuwa
ilionekena alikuwa akijivinjari na wanaume wote kwa nyakati tofauti hivyo kuto
tambua baba halali wa mtoto.
Kwa
upande wake mwanamke huyo alisema alichukua maamuzi ya kuolewa na mume mungine
baada ya kuona mumewe amekuwa akichepuka na mwanamke mungine na kufikia hatua
kumpangia chumba na kuwa aliamua kufanya hivyo ili kumkomoa.
“mume
wangu alipo pata mchepuko huo alianza kunidharau na kuniambia kuwa mimi sina
hadhi ya kuwa naye huku akipunguza penzi kwangu ndipo nikachukua maamuzi magumu
ya kuamua kuchepuka na hatimaye kuolewa”alisema mwanamke huyo.
Serikali
ya kijiji hicho kilishindwa kufikia tamati ya suala hilo baada ya mwanamke huyo kuwa na msimamo
wa kuwa atawamudu wanaume wote wawili alidai ananguvu za kutosha na kuahidi
kuwa mwaminifu kwa wanaume hao hadi siku ya kufa.
Kwa
upande wao wanaume hao waliafikiana kushea penzi na mwanamke huyo ambapo
walipangiana zamu na kutokomea katika kikao hicho huku mamia waliokuwepo kwenye
shauri hilo
wakishikwa na butwaa kutokana na maamuzi ya wanaume hao kuoa mke mmoja.
Na, Baraka Lusajo Rungwe
Post a Comment
Post a Comment