JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LA
TANZANIA
________
KAMATI YA
KUDUMU YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI (PAC)
_________________
TAARIFA YA
KAMATI KUFUATIA MATOKEO YA UKAGUZI
MAALUM WA
MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA
SERIKALI
KATIKA AKAUNTI YA TEGETA ESCROW ILIYOKUWA
KATIKA BENKI
KUU YA TANZANIA
OFISI YA
BUNGE
S.L.P 941
DODOMA
NOVEMBA 20141
1.0
UTANGULIZI
1.1 Chimbuko
la Hoja ya Ukaguzi Maalum wa Akaunti ya
Tegeta
ESCROW kwa Upande wa Bunge
1.1.1
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za
Mashirika ya
Umma (POAC) kwa Mwaka wa Fedha
2009/2010
Mheshimiwa
Spika, kuwasilishwa kwa Hoja inayohusiana na
Akaunti ya
Tegeta ESCROW kwa mara ya kwanza ndani ya Bunge
lako Tukufu,
kulitokana na kuwasilishwa kwa Taarifa ya Mwaka ya
iliyokuwa
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma
(POAC) kwa
Mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2010.
Mheshimiwa
Spika, kuwasilishwa kwa hoja hiyo Bungeni
kulitokana
na Kamati ya POAC kuchambua na kujadili Taarifa ya
Hesabu
zilizokaguliwa za Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa Mwaka
wa fedha
ulioishia Juni 30, 2009. Mojawapo ya Hoja ya Ukaguzi
kwa mwaka
husika ilikuwa ni uendeshaji wa Akaunti ya Tegeta 2
ESCROW
ambapo Kamati ilifahamishwa kuwa Kampuni ya IPTL
ilikuwa
chini ya ufilisi na hivyo kulikuwa na uwezekano wa fedha
katika
Akaunti hiyo kutolewa na kulipa madeni ya IPTL wakati wa
ufilisi.
Mheshimiwa
Spika, kufuatia taarifa hiyo, Kamati ya POAC
iliwasilisha
Bungeni pendekezo la kuzuia utoaji wa fedha katika
Akaunti ya
Tegeta ESCROW hadi hapo migogoro yote kati ya
TANESCO na
IPTL itakapotatuoliwa kwa maslahi mapana ya Taifa
na baada ya
migogoro hiyo kupatiwa ufumbuzi fedha zilizokuwa
kwenye
Akaunti hiyo ndio pekee zitumike kulipa madeni ya IPTL.
1.1.2Kikao
cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za
Serikali
(PAC) na Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu
Mheshimiwa
Spika, tarehe 16 Machi, 2014 Kamati ya PAC
ilikutana na
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Katibu Mkuu wa
Wizara ya
Fedha pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
za Serikali
kwa ajili ya kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Agizo
lililotolewa
na iliyokuwa Kamati ya POAC mwaka 2009 kuhusu 3
matumizi ya
fedha zilizokuwemo kwenye Akaunti ya Tegeta
ESCROW
wakati wa kulipa madeni ya IPTL.
Mheshimiwa
Spika, katika kikao hicho pamoja na mambo
mengine,
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania aliiarifu Kamati kuwa
fedha
zilizokuwemo kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW
zimetolewa
na kulipwa IPTL. Kamati ilipohoji kama ulipaji huo
umezingatia
Azimio la Bunge lako Tukufu kwamba fedha hizo
zisitolewe
mpaka mgogoro baina ya TANESCO na IPTL
utakapotatuliwa,
haikupatiwa majibu. Hivyo, Kamati kwa
kuzingatia
umuhimu wa Azimio hilo la Bunge kutekelezwa ipasavyo
na
kuhakikisha utoaji wa fedha katika Akaunti hiyo umefanyika
kihalali na
aliyelipwa amelipwa kihalali, ilimuomba Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za Serikali kufanya Ukaguzi Maalum
kuhusu
miamala iliyofanyika katika Akaunti hiyo pamoja na umiliki
wa Kampuni
ya IPTL.
1.1.3 Agizo
la Kufanyika kwa Ukaguzi Maalum
Mheshimiwa
Spika, tarehe 20 Machi, 2014 Kamati ya PAC
iliwasilisha
Hadidu za Rejea kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa 4
Hesabu za
Serikali kwa ajili ya kufanya Ukaguzi Maalum kupitia
barua yenye
Kumbukumbu Namba CBC.155/188/01/31. Aidha,
Ofisi ya
Taifa ya Ukaguzi iliwasiliana na Katibu wa Bunge kupitia
barua
Kumbukumbu namba CA.27/442/01/53 ya tarehe 27 Aprili,
2014 ikiomba
Kamati ya PAC iweze kuridhia Hadidu za Rejea
zitakazoongoza
ukaguzi husika. Kamati iliridhia Hadidu za Rejea
husika kwa
barua Na. CBC. 155/188/01 ya tarehe 3 Mei, 2014.
1.1.4
Majadiliano Bungeni
Mheshimiwa
Spika, katika mijadala mbalimbali ambayo imekuwa
ikiendelea
katika Bunge lako Tukufu, Waheshimiwa Wabunge
mbalimbali
wamekuwa wakizungumzia kwa namna tofauti suala la
Akaunti ya
Tegeta ESCROW. Michango hiyo imekuwa ikijikita
katika mambo
makubwa mawili, kundi moja limekuwa likidai kuwa
fedha hizo
ni za umma na zimetolewa bila kufuata taratibu za
kisheria.
Kundi lingine limekuwa likisema fedha hizo siyo za umma
ni za IPTL
na zilitolewa kihalali. Baadhi ya Wabunge ambao
wamewahi
kuzungumzia suala hili ni pamoja na Mhe. David
Kafulila,
(Mb.) Mhe. John Mnyika, (Mb.), Mhe. Profesa Sospeter
Muhongo,
(Mb.) Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Stephen 5
Masele,
(Mb.) Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Jaji.
Fredrick
Mwita Werema, (Ex Official) Mwanasheria Mkuu wa
Serikali
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda, (Mb.)
Nukuu ya
baadhi ya yaliyosemwa na Wabunge hawa zimeainishwa
katika
uchambuzi wa Kamati ambao ni Sehemu ya Tatu ya Taarifa
hii.
1.2
Kuwasilishwa kwa Taarifa ya Ukaguzi Maalum
Mheshimiwa
Spika, tarehe 14 Novemba, 2014, Taarifa ya
Ukaguzi
Maalum wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali
kuhusiana na Miamala iliyofanyika katika Akaunti ya
Tegeta
ESCROW pamoja na Umiliki wa Kampuni ya IPTL
iliwasilishwa
kwenye Ofisi ya Spika na Katibu wa Bunge na tarehe
17 Novemba,
2014 ilikabidhiwa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Hesabu za
Serikali (PAC) ili ichambuliwe na kutolewa maoni na
mapendekezo.
Tarehe 18 Novemba, 2014, Kamati ya PAC ilianza
uchambuzi wa
Taarifa hiyo (Kiambatisho Na.1).
1.3 Kamati
ya PAC ilivyofanya kazi6
Mheshimiwa
Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 119 ya Kanuni za
Bunge, Toleo
la 2013 Spika anaweza kukabidhi jambo lingine
lolote kwa
Kamati yoyote kadri atakavyoona inafaa kwa ajili ya
kufanyiwa
kazi na Kamati hiyo. Hivyo, Kamati ya PAC katika
kutekeleza
jukumu la kuchambua Taarifa ya Ukaguzi Maalum
ilifanya
kazi kama “Kamati ya Uchunguzi” ikiongozwa na masharti
ya Sheria ya
Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge, Sura ya 296.
1
Mheshimiwa
Spika, Kanuni ya 117 imetoa pia mamlaka kwa
Kamati za
Kudumu kujiwekea utaratibu wake na kuweza
kuwaruhusu
Wabunge ambao sio Wajumbe wa Kamati husika
kuhudhuria
na kushiriki katika shughuli za Kamati. Kwa kutumia
Kanuni hiyo,
Kamati iliwaalika Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla (Mb),
Mhe. Luhaga
Joelson Mpina (Mb) na Mhe. Alphaxard Kangi Lugola
(Mb)
kuhudhuria na kushiriki vikao vya Kamati.
Mheshimiwa
Spika, pamoja na kupitia Taarifa ya Ukaguzi
Maalum
tarehe 19 Novemba, 2014 Kamati ilifanya mahojiano na
mashahidi
wawili hususan Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za
Serikali, Ndugu Francis Mwakapalila na Kamishna Mkuu
1
The Parliamentary Imunities, Powers and Privileges Act, Cap 2967
wa TRA Ndugu
Rished Bade. Pia Kamati ilimwandikia Mkurugenzi
Mkuu wa
TAKUKURU Dkt. Edward Hosea kama rafiki wa Kamati.
Aidha,
Kamati ilipitia Nyaraka na Sheria mbalimbali zilizoletwa na
mashahidi
pamoja na Kumbukumbu Rasmi (Hansard) za Vikao vya
Bunge na Kamati
za Kudumu za Bunge ambapo suala la Akaunti ya
Tegeta
ESCROW limewahi kujadiliwa.
Mheshimiwa
Spika, Wajumbe wa PAC na Wabunge waalikwa
walioshiriki
kazi hii ni hawa wafuatao:-
1. Mhe.
Zitto Zuberi Kabwe (Mb), - Mwenyekiti
2. Mhe. Deo
Haule Filikunjombe (Mb), - Makamu
Mwenyekiti
3. Mhe. Asha
Mshimba Jecha (Mb), - Mjumbe
4. Mhe.
Desderius John Mipata (Mb), - Mjumbe
5. Mhe.
Zaynab Matitu Vulu (Mb), - Mjumbe
6. Mhe.
Zainab Rashid Kawawa (Mb), - Mjumbe
7. Mhe.
Kheri Ali Khamis (Mb), - Mjumbe
8. Mhe.
Abdul Jabir Marombwa (Mb), - Mjumbe
9. Mhe.
Gaudence Cassian Kayombo(Mb), - Mjumbe8
10. Mhe.
Hezekiah Ndahani Chibulunje (Mb), - Mjumbe
11. Mhe.
Amina M. Mwidau(Mb), - Mjumbe
12. Mhe.
Lolesia M. Bukwimba (Mb), - Mjumbe
13. Mhe.
Lucy Fidelis Owenya (Mb), - Mjumbe
14. Mhe.
Esther Nicholas Matiko (Mb), - Mjumbe
15. Mhe.
Ally Keissy Mohamed (Mb), - Mjumbe
16. Mhe.
Faida Mohammed Bakar (Mb), - Mjumbe
17. Mhe.
Ismail Aden Rage (Mb), - Mjumbe
18. Mhe.
Modestus Dickon Kilufi (Mb), - Mjumbe
19. Mhe.
Kombo Khamis Kombo, (Mb) - Mjumbe
20. Mhe.
Catherine Valentine Magige (Mb), - Mjumbe
21. Mhe.
Dkt. Haji Mponda (Mb), - Mjumbe
22. Mhe.
Luhaga Joelson Mpina (Mb), - Mjumbe
Mwalikwa
23. Mhe.
Alphaxard Kangi Lugola (Mb), - Mjumbe
Mwalikwa
24. Mhe. Dkt.
Hamisi A. Kigwangalla (Mb), - Mjumbe
Mwalikwa
Kamati
ilisaidiwa na Sekretarieti iliyoongozwa na Katibu wa Bunge
Dkt. Thomas
D. Kashililah na Makatibu wengine ambao ni Ndg. 9
Nenelwa
Mwihambi Wankanga, Ndg. Mathew Nionzima Kileo, Ndg.
Mswige
Dickson Bisile na Ndg. Erick Sosteness Maseke.10
2.0
UCHAMBUZI WA KAMATI KUHUSU TAARIFA YA UKAGUZI
MAALUM NA
YALIYOJITOKEZA KWENYE MAHOJIANO YA
KAMATI NA
KAIMU MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA
HESABU ZA
SERIKALI, KAMISHNA MKUU WA TRA NA
MKURUGENZI
MKUU WA TAKUKURU
2.1 UTEKELEZAJI
WA MKATABA WA TANESCO NA IPTL
Mheshimiwa
Spika, katika kuchambua hadidu za rejea
zilizofanyiwa
kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali,
Kamati ilijielekeza kwanza kufanya uchambuzi kuhusiana
na
utekelezaji wa Mkataba wa kuzalisha umeme kati ya Kampuni
ya IPTL na
TANESCO, uchambuzi wa Kamati katika Taarifa ya
Ukaguzi
Maalum umebaini mambo mbalimbali. IPTL ilianzishwa
chini ya
Wanahisa wawili ambao ni Kampuni ya Mechmar Malaysia
Berhad
iliyosajiliwa nchini Malaysia ambayo ilikuwa inamiliki hisa 7
sawa na
asilimia 70 katika IPTL na Kampuni ya VIP Engineering
and
Marketing iliyosajiliwa hapa nchini ikiwa na hisa 3 sawa na
asilimia 30
ya hisa zote. Mwaka 1995 Serikali kupitia TANESCO
iliingia
Mkataba wa miaka 20 na IPTL kwa ajili ya kuzalisha na 11
kuuziana
umeme wa megawati 100 japokuwa makubaliano ya
awali (MOU)
yalionyesha kuwa mkataba ungekuwa wa miaka 15.
Mahitaji ya
umeme ilikuwa ni kwa dharura kutokana na ukame
uliosababisha
upungufu wa maji katika mabwawa ya kuzalisha
umeme.
Mheshimiwa
Spika, mwaka 1997 ujenzi wa mtambo wa
kuzalisha
umeme ulikamilika. Hata hivyo, TANESCO ilibaini
kwamba
gharama za ujenzi wa mtambo wa kuzalisha umeme
ambazo IPTL
iliwasilisha kwake zilikuwa kubwa tofauti na
makubaliano
ya kwenye Mkataba. IPTL ilikuwa imefunga injini
zenye
msukumo wa kati (medium speed) zenye gharama ndogo
na uwezo
mdogo badala ya injini za msukumo mdogo (low speed)
zenye nguvu
kubwa na bei kubwa. Wakati huo huo IPTL
waliendelea
kutoza kiasi kikubwa cha fedha kinacholingana na
gharama ya
ufungaji wa mtambo wenye msukumo mdogo (low
speed).
Katika utekelezaji wa Mkataba IPTL walitakiwa kufunga
jenereta 5
zenye uwezo wa kuzalisha megawati 20 kila moja lakini
badala yake
walifunga jenereta 10 zenye uwezo wa kuzalisha
megawati 10
kila moja jambo ambalo lilikuwa ni kinyume na
makubaliano
ya Mkataba.12
Mheshimiwa
Spika, kutokana na IPTL kukiuka makubaliano ya
Mkataba kama
ilivyoelezwa hapo juu, mwaka 1998 TANESCO
ilifungua
Shauri Na. ARB/98/8 katika Baraza la Kimataifa la
Usuluhishi
wa Migogoro ya Uwekezaji (The International Centre for
Settlement
of Investiment Disputes - ICSID) kupinga ukiukwaji
huo. Katika
Hukumu iliyotolewa na ICSID, IPTL iliagizwa
kupunguza
gharama za uwekezaji kutoka USD 163.531 milioni hadi
USD 127. 201
milioni kwa mwezi.2 (Kiambatisho Na. 2)
Mheshimiwa
Spika, ujenzi wa Mtambo ulikamilika mwaka 1997
lakini
uzalishaji na uuzaji wa umeme ulianza mwaka 2002. Kwa
mujibu wa
makubaliano ya kuzalisha umeme, TANESCO ina wajibu
wa kulipia
gharama za uwekezaji (capacity charges) kwa wastani
wa USD 2.6
milioni kila mwezi;3 gharama za kutumia umeme
(energy
charges) wakati uzalishaji halisi unapofanyika na
kugharamia
mafuta ya kuendeshea mitambo husika. Hivyo,
kuanzia
mwaka 2002 capacity charges ambayo ni gharama za
uwekezaji
kutokana na uwepo wa mtambo wa kuzalisha umeme,
2
Shauri hili
hurejewa kama ICSID-1
3 Baada ya utekelezaji wa ICSID 113
zilianza
kulipwa na TANESCO kwa IPTL. Ikumbukwe kuwa capacity
charges
huendelea kulipwa kwa muda wote ambao Mkataba
unaendelea
bila ya kujali kama mtambo unazalisha umeme au
hauzalishi.
Mheshimiwa
Spika, gharama hizi zilikoma kulipwa moja kwa
moja kwa
IPTL mwaka 2007 baada ya TANESCO kubaini kuwa
IPTL
inakokotoa gharama hizo kwa msingi wa USD 38.16 milioni
(ambayo ni
sehemu ya mkopo wa USD 105 milioni uliochukuliwa
na wanahisa
kutoka Umoja wa Mabenki ya Malaysia (Consortium
of Malaysian
Banks) ambao baadaye ulinunuliwa na Standard
Chartered
Bank ya Hong Kong) badala ya mtaji wa uwekezaji wa
kiasi cha
Sh. 50,000 uliosajiliwa BRELA na hivyo kufanya tozo ya
capacity
charges kuwa kubwa. Endapo ungetumika mtaji wa
uwekezaji wa
Sh. 50,000/= katika kukokotoa capacity charges
TANESCO
ingekuwa inalipa tozo ndogo kuliko ilivyo sasa.
Mheshimiwa
Spika, kutokana na kutoridhishwa na kiwango cha
capacity
charges kilichokuwa kinatozwa na IPTL mnamo mwaka
2004,
TANESCO ilifungua Shauri la Pili ICSID kupinga kiasi kikubwa 14
cha tozo ya
capacity charges.
4 Uamuzi wa
Baraza ilikuwa ni
kwamba
Wanahisa waketi na Mteja wao (TANESCO) na
kukubaliana
kuhusu kanuni ya ukokotoaji wa tozo hiyo.
Mheshimiwa
Spika, mpaka tunapowasilisha Taarifa hii Bungeni,
Uamuzi wa
ICSID-2 kwamba IPTL ikae na TANESCO kwa ajili ya
kukokotoa
upya capacity charges haujatekelezwa, hivyo TANESCO
wanaendelea
kulipa USD. 2.6 milioni (sawasawa na shilingi
4,511,000,000/=
kwa mwezi)
5 kila mwezi
kama capacity charges
kwa IPTL
izalishe au isizalishe umeme. Hivyo, utekelezaji wa
Mkataba wa
uzalishaji wa umeme kati ya IPTL na TANESCO
umetawaliwa
na migogoro toka ulipoanza mpaka sasa.
2.2
UFUNGUAJI WA AKAUNTI YA TEGETA ESCROW
Mheshimiwa
Spika, Hadidu Rejea namba tatu ilimtaka Mdhibiti
na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali kuchunguza sababu za
Kufungua
Akaunti Maalumu ya ESCROW – Tegeta (TegetaESCROW
Account),
Pia kuchunguza Chanzo cha mgogoro kuhusu
4 Shauri hili hurejewa pia kama ICSID 2. 5
Kiwango cha kubadilishia fedha Dola 1 kwa wastani wa shilingi 1,735 (chanzo BOT tarehe 25/11/2014)15
Tozo baina
ya TANESCO na IPTL na kuthibitisha iwapo Mgogoro
uliamuliwa
kwa Masilahi ya pande zote mbili yaani (TANESCO na
IPTL).
2.2.1 Chanzo
cha kufunguliwa kwa Akaunti ya Tegeta ESCROW
Mheshimiwa
Spika, kwa mujibu wa Ukaguzi maalum wa Mdhibiti
na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali, sababu ya msingi ya
kufungua
Akaunti ya Tegeta ESCROW ni kipengele Na. 6.8 cha
Mkataba wa
kununua umeme, (Power Purchasing Agreement -
PPA) baina
ya TANESCO na IPTL ambacho kinaeleza kuwa iwapo
upande
wowote kati ya TANESCO au IPTL utapinga usahihi wa
tozo za
Ununuzi wa umeme, Washirika hao watalazimika kutumia
jitihada zao
kuhakikisha kuwa mgogoro juu ya Malipo husika
unamalizika
kwa mujibu wa kipengele Na. 18.1 cha PPA.
Mheshimiwa
Spika, kipengele husika (18.1 (a)) cha Mkataba wa
kununua
umeme kinaitaka TANESCO na IPTL kujadiliana iwapo
hawaafikiani
katika masuala ya Tozo na kinasomeka kama
ifuatavyo:16
“In the
event that a dispute arises, the Parties
shall
attempt in good faith to settle such Dispute
by mutual
discussion, which may include
referring
the Dispute to the Operations
Committee,
provided that any matters are
described in
Article 7.4 shall be referred to the
Operations
Committee for its review and
recommendations
or attempted resolution,
where
appropriate”
Mheshimiwa
Spika, Aidha, kwa kuzingatia kipengele Na 18.2
(Kiambatisho
Na. 3) wahusika katika mkataba wa PPA
wanalazimika
kutumia mtaalamu wa upatanishi (mediation by
expert)
katika utatuzi wa mgogoro kabla ya kutolewa fedha
zilizopo
kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW.
Mheshimiwa
Spika, kipengele cha 18.2 cha mkataba wa
ESCROW
kinaelekeza wahusika kama ifuatavyo:
“In the
event that Parties are unable to resolve a
Dispute in
accordance with Article 18.1, then 17
either
party, in accordance with this Article 18.2
may refer
the Dispute to an expert for
consideration
of the Dispute and obtain a
recommendation
from the expert as the resolution
to the
dispute”
Mheshimiwa
Spika, uchambuzi wa Kamati kuhusu Taarifa ya
Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali umethibitisha
kuwa kwa
muda wote wa Mkataba baina ya TANESCO na IPTL
hapakuwahi
kuanzishwa Kamati ya Uendeshaji (Operations
Committee).
Kinyume na Kipengele 8.3 (a) cha PPA. TANESCO na
IPTL
walipaswa kuunda Kamati ya Uendeshaji siku 180 kabla ya
kuanza
uzalishaji (Commercial Operation Date). Kamati hiyo
ilitakiwa
kuwa na Wajumbe sita ili kuratibu uendeshaji wa mtambo
na pia
ingehusika na usuluhishi wa migogoro ambayo ingejitokeza
kutokana na
Mkataba wa uzalishaji umeme.
Mheshimiwa
Spika, umuhimu wa kufanyika usuluhishi kwenye
masuala
ambayo TANESCO na IPTL wameshindwa kuelewana
umetiliwa
nguvu na Kipengele 8.6 cha makubaliano ya Akaunti ya 18
Tegeta
ESCROW. Kipengele hicho kinawaelekeza wahusika
kutumia
taratibu za usuluhishi na makubaliano kama
zilivyoanzishwa
na Azimio la Usuluhishi wa Mikataba baina ya
Mataifa na
Mataifa (ICSID Convetion). Hivyo basi ni dhahiri kuwa
baada ya
TANESCO na IPTL kutokukubaliana katika ngazi ya
Kamati ya
Uendeshaji (ambayo haikuwahi kuanzishwa)
wangekwenda
kwa Msuluhishi na kama ingeshindikana
wangechukua
hatua ya upatanishi (arbitration).
2.2.2 Chanzo
cha Mgogoro baina ya TANESCO na IPTL
Mheshimiwa
Spika, kwa mujibu wa uchambuzi wa Taarifa ya
Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, imebainika kuwa
chanzo cha
mgogoro kati ya TANESCO na IPTL ambacho ndio
kilisababisha
kufunguliwa kwa Akaunti ya Tegeta ESCROW, ni
taarifa
ziliyoifikia Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO mnamo tarehe
01 Aprili,
2004. Kaika Taarifa hiyo, pamoja na mambo mengine
walifahamishwa
na mmoja wa wanahisa wa IPTL, Kampuni ya VIP
Engineering,
kuwa kuna viashiria kuwa TANESCO wanailipa IPTL
capacity
charges kubwa.19
Mheshimiwa
Spika, baada ya kupokea taarifa hiyo, Bodi ya
Wakurugenzi
ya TANESCO iliiteua Kampuni ya Uwakili ya Mkono ili
kufuatilia
madai hayo na kutoa ushauri kwa Bodi. Aidha, Bodi
iliwateua
Ndg. Arnold Kileo, Dr. Enos Bukuku na Bw. Bashiri
Mrindoko
ambao walikuwa Wajumbe wa Bodi kufuatilia kwa karibu
usahihi wa
madai hayo.
Mheshimiwa
Spika, Kampuni ya Uwakili ya Mkono iliishauri Bodi
ya
wakurugenzi ya TANESCO kuwa, gharama za uwekezaji
zilizowasilishwa
na IPTL na ambazo zilitumika kukokotoa kiwango
cha capacity
charges hazikuwa sahihi. Ushauri huu ulitokana na
ukweli kuwa
kiwango cha ‘capacity charges’ kilichokuwa kinatozwa
kilizingatia
mtaji wa wanahisa (Owners’ Equity) ambao ni USD
milioni
38.16 badala ya Sh. za Kitanzania 50,000/= ambazo
wanahisa wa
IPTL wakati wa usajili wa Kampuni hiyo kwa Msajili
wa Makampuni
(BRELA) walikionyesha kuwa ndio mtaji (paid up
share
capital). Aidha, kiasi hicho kimeonyeshwa katika Hesabu
zilizokaguliwa
za IPTL kati ya mwaka 2002 na mwaka 2007.
(Kiambatisho
Na. 4).20
Mheshimiwa
Spika, kwa kuzingatia ushauri wa Kampuni ya
Uwakili ya
Mkono, Menejimenti ya TANESCO kupitia barua namba
DMDF&CS/02/05,
tarehe 17 Juni, 2004 walitoa Notisi kwa IPTL ya
kutoendelea
kulipa capacity charges kwa sababu kiwango
walichokuwa
wanatozwa ni kikubwa kuliko inavyostahili
(Kiambatisho
Na. 5).
Mheshimiwa
Spika, pamoja na kutoa Notisi hii Kamati imebaini
kuwa Bodi na
Menejimenti ya TANESCO kwa nyakati tofauti
walizitaarifu
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wizara ya
Nishati na
Madini, na Msajili wa Hazina kuomba zichukue hatua
stahiki
kutatua mgogoro uliokuwa unaendelea.6
Kamati ilifanikiwa
kuona barua
Na. NEM/740/05 ya tarehe 6 Desemba, 2005 kutoka
kwa Kampuni
ya Uwakili ya Mkono kwenda kwa aliyekuwa Katibu
Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini Bw. Patrick Rutabanzibwa
akirejea
mazungumzo yao ya tarehe 5 Desemba, 2005 ambapo
iliamuliwa
kuwa Kampuni ya Uwakili ya Mkono iandae Rasimu ya
Makubaliano
kwa ajili ya ufunguzi wa Akaunti ya Tegeta ESCROW.
6
Barua ya
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali yenye Kumb. Na.
SEC/247/07/04
ya tarehe 05 Julai 2004, Barua ya Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO kwenda kwa
Katibu Mkuu
Wizara ya
Nishati na Madini yenye Kumb. NaSEC.427/9/2004 ya tarehe 23 Septemba, 2004 na
Barua ya
Mkurugenzi
Mtendaji wa TANESCO kwenda kwa Msajili wa Hazina yenye Kumb. Na. SEC.247/8/2004
21
2.2.3
Kufunguliwa kwa Akaunti ya Tegeta ESCROW
Mheshimiwa
Spika, baada ya kukamilika kwa Rasimu ya
makubaliano
ya mchakato wa kufungua Akaunti ya Tegeta
ESCROW,
Mkataba wa kufunguliwa kwa Akaunti hiyo ulisainiwa na
washirika
wawili ambao ni Wizara ya Nishati na Madini kama
mdhamini wa
TANESCO katika ulipaji wa capacity charges na
energy
charges na Kampuni ya IPTL. Aidha, kwa mujibu wa
Mkataba huo
BOT ilikuwa ni wakala wa Uendeshaji wa Akaunti
husika.
Mheshimiwa
Spika, wakati mahojiano ya Kamati na Kaimu
Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Kamishna Mkuu
wa TRA
pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU tarehe 19
Novemba,
2014 waliithibitishia Kamati kuwa kutokana na
makubaliano
wa Akaunti ya Tegeta ESCROW, sehemu ya fedha au
fedha yote
katika Akaunti hiyo ilikuwa ni fedha ya umma. Katika
mahojiano
hayo, Maafisa hao walitamka yafuatayo kuhusiana na
umiliki wa
fedha za Akaunti ya Tegeta ESCROW:22
Kaimu
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
“… Kwa jinsi
tulivyopitia fedha hii, tungesema ipo katika
makundi
matatu. Kundi la kwanza hiyo fedha ilikuwa na
kodi ndani
yake kwa hiyo tungesema kulikuwemo na
fedha ya
Serikali kwa maana ya kodi. Kwa upande
mwingine,
kwa sababu mpaka ESCROW inafunguliwa
kulikuwa na
dispute, kulikuwa na kutokubaliana juu ya
charges, kwa
hiyo kuna fedha ambayo inaweza ikawa ni
ya TANESCO
na kuna fedha ambayo inaweza kuwa ni ya
IPTL …”7
Kamishna
Mkuu wa TRA
7
Hansard ya
mahojiano ya Kamati na Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
tarehe 19 Novemba
2014 uk.
19.23
“… TANESCO
walitudhihirishia na kwa evidence
kwamba
katika kufanya yale malipo kwenye
ESCROW
Account walilipa pamoja na pesa ambayo
ilitakiwa
kulipwa kwetu ya VAT. Kwa hiyo,
kulikuwa na
VAT Component ambayo haikutakiwa
kwenda kule
…”8
Mkurugenzi
Mkuu wa TAKUKURU
“…
ninachoweza tu kusema na baada ya kusoma
Taarifa ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali ni
wazi kwamba pesa zilivyotoka TANESCO
kwenda Benki
Kuu bado kwa maoni yetu ni fedha
za Serikali
kwa sababu ni fedha ya TANESCO. Huo
ndiyo
mtazamo ambao tunao kiuchunguzi hadi
wakati
huu.”9
Mheshimiwa
Spika, majibu haya yaliyotolewa na Kaimu
Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Kamishna
Mkuu wa TRA
na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU
8
Hansard ya
mahojiano ya Kamati na Kamishna Mkuu wa TRA tarehe 19 Novemba, 2014 uk. 61.
9
Hansard ya
mahojiano ya Kamati na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU tarehe 19 Septemba, 2014 uk.
81.24
yanathibitisha
kuwa Waziri wa Nishati na Madini na Naibu
wake pamoja
na Mwanasheria Mkuu wa Serikali hawakuwa
sahihi
walipolieleza Bunge kwamba fedha za kwenye Akaunti
ya Tegeta
ESCROW siyo za Serikali. Wakijaribu kujibu hoja
mbalimbali
za Wabunge kuhusiana na suala hilo kwa nyakati
tofauti kila
mmoja wao kwa namna yake alitamka ifuatavyo:
Waziri wa
Nishati na Madini. Mhe. Prof. Sospeter
Muhongo (Mb)
“…fedha za
ESCROW hizi ni fedha zilizowekwa
baada ya
hawa wafanyabiashara wawili
kutokukubaliana
na zingeweza kuwekwa popote
… kwa hiyo
hizo pesa ni za IPTL, yaani ni kitu
ambacho ni
rahisi kabisa, lakini mtu anataka
kupotosha
hapa anasema fedha za walipa kodi,
fedha sijui
za wakulima, hakuna kitu kama
hicho,”10
10Hansard ya tarehe 30 Mei, 2014 ukurasa wa 41525
Naibu Waziri
wa Nishati na Madini, Mhe. Stephen
Masele (Mb)
“…
nilipokuwa namsikiliza Mheshimiwa David Kafulila,
nikawa
najiuliza maswali, Mheshimiwa David Kafulila
yumo humu
Bungeni kwa amri ya Mahakama, kama
Mahakama
inakupa amri ya kuwa Mbunge, halafu leo
ikiamua
kwamba fedha za IPTL zilipwe, unahoji na
unataka
umwingize Mheshimwa Muhongo wakati
Muhongo
hajaamua chochote, kwa kweli
inasikitisha.”11
Mwanasheria
Mkuu wa Serikali
“… kuhusu
hili la ESCROW, lazima niseme ukweli.
Suala la
ESCROW ni suala ambalo linatokana na
wanahisa wa
IPTL ambao ni wanahisa wawili.
Mwanahisa
mmoja ni VIP na mwingine ni
Mechmar,
hiyo ndiyo IPTL. Ugomvi huu wa
ESCROW siyo
pesa ya Serikali (Makofi) …”12
11Hansard ya tarehe 30 Mei, 2014 ukurasa wa 397
12Hansard ya
tarehe 25 Juni, 2014 uk. 72.26
Mheshimiwa
Spika, aidha Mheshimiwa Waziri Mkuu
alikuwa ni
miongoni mwa waliodai kuwa fedha zilizokuwa
kwenye
Akaunti ya Tegeta ESCROW siyo za umma. Akijibu
Mwongozo wa
Mheshimiwa Kafulila kwenye Kikao cha Nane,
Mkutano wa
15 Mheshimiwa Waziri Mkuu alisema:
“…fedha zile
ambazo zilikuwa zimewekwa
ESCROW
Account ni fedha za IPTL kwa maana ya
hiyo
Kampuni. Katika uamuzi wa Mahakama
uliotolewa
ikaamua kuwa fedha ile ipelekwe IPTL
kwa sababu
ni fedha ya IPTL. Tukasema ni
vyema,
kukawa na mvutano pale kidogo sasa
tupeleke au
tusipeleke, tukasema hapana, uamuzi
wa Mahakama
unasema pelekeni, fedha zile
zikapelekwa
kwa sababu ni za IPTL…”13
2.2.4
Kuibuka kwa madai ya IPTL Kutaka kulipwa fedha katika
Akaunti ya
Tegeta ESCROW
13Hansard ya tarehe 9 Aprili, 2014 uk. 50-5127
Mheshimiwa
Spika, uchambuzi wa Kamati umebainisha kuwa
baada ya
hukumu ya Mahakama Kuu ya Tanzania katika Shauri
Na. 49 la
2002 na Na. 254 la 2003 ya tarehe 05 Septemba, 2013,
Mwenyekiti
na Mtendaji Mkuu wa PAP ambaye sasa
anajitambulisha
kama Mmiliki wa IPTL, Bw. Harbinder Singh Sethi,
alimuandikia
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO barua yenye
Kumb. Na.
IPTL/TANESCO/2013/03 ya tarehe 13 Septemba, 2013
akimtaka
kulipa fedha zote zilizokuwa kwenye Akaunti ya Tegeta
ESCROW.
(Kiambatisho Na.6). barua hiyo ilinakiliwa kwa Waziri
wa Nishati
na Madini, na hapa ndipo upotoshaji wa amri ya
Mahakama
ulipoanzia.
Mheshimiwa
Spika, Amri ilikuwa inakabidhi ‘affairs’ za IPTL
lakini
haikutoa maelekezo kuwa fedha zilizokuwa kwenye Akaunti
ya Tegeta
ESCROW zitolewe bila kufuata utaratibu uliokuwa
umeainishwa
katika makubaliano ya Akaunti husika. Hukumu ya
Mheshimiwa
Jaji Oriyo ya tarehe 16 Desemba, 2008 iliyokabidhi
mali zote za
IPTL kwa RITA haikutafsriwa kuwa fedha za Akaunti
ya Tegeta
ESCROW zitoke bali ziliwekwa chini ya Mfilisi (RITA) 28
mpaka hapo
mgogoro wa capacity charges uishe.14 Ni ajabu
kwamba
Serikali nzima ilitafsiri Amri ya Mheshimiwa Jaji Utamwa
kwa matakwa
ya Bw. Harbinder Singh Sethi.
Mheshimiwa
Spika, Aidha tarehe 18 Septemba, 2013 Bw.
Harbinder
Sethi alimwandikia tena Mkurugenzi Mtendaji wa
TANESCO
akiendelea kusisitiza kuwa TANESCO wakubali kutoa
fedha zote
za ESCROW na kutoendelea kupinga ankara za madai.15
Mheshimiwa
Spika, kufuatia madai ya PAP kutaka kulipwa fedha
zilizokuwa
kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW, tarehe 16
Septemba,
2013 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,
Bwana
Eliakim Maswi, alimwandikia Mwanasheria Mkuu wa Serikali
barua Kumb.
Na CBD.88/147/29 akimwarifu kuwa PAP imepewa
umiliki wa
hisa za IPTL kwa uamuzi wa Mahakama wa tarehe 5
Septemba,
2013. Hata hivyo alimwarifu pia kuwa Akaunti ya
Tegeta
ESCROW ilifunguliwa kutokana na mgogoro wa capacity
charges kati
hiyo TANESCO na IPTL na hivyo umiliki wa fedha
zilizokuwemo
kwenye Akaunti ya utabainika baada ya wahusika
14 Shauri Na. 49 la mwaka 2002, Mahakama Kuu ya Tanzania (Dar Es Salaam)
15Barua ya
Bw. Harbinder Sethi kwenda kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO yenye Kumb. Na.
IPTL/TANESCO/2003
ya tarehe 18 Septemba, 201329
kukutana na
kujadiliana juu ya jambo hili. Kaatibu Mkuu aliomba
mwongozo wa
kisheria kuhusu masuala hayo na akaambatanisha
mapendekezo
ya makubaliano ya utolewaji wa fedha kwenye
Akaunti hiyo
yaliyokuwa yameandaliwa na Kampuni ya PAP.
Mheshimiwa
Spika, tarehe hiyo hiyo 16 Septemba, 2013
Mwanasheria
Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, alimjibu
Katibu Mkuu
wa Wizara ya Nishati na Madini kwa barua Namba
AGCC/E.80/6/58
akikubaliana na maoni ya Katibu Mkuu wa Wizara
ya Nishati
na Madini kuwa washirika wa Akaunti ya Tegeta
ESCROW
(TANESCO na IPTL) wakae pamoja kuchambua madai
yanayoihusu
TANESCO. Aidha Mwanasheria Mkuu wa Serikali
alielekeza
kuwa dhamana ya Serikali kwenye Mkataba wa
uzalishaji
umeme ipitiwe na kujadiliwa upya ili kukidhi mabadiliko
yaliyotokea
na athari ambazo zingeweza kuipata Serikali.
2.3 MAUZO YA
HISA ZA IPTL
Mheshimiwa
Spika, Hadidu za rejea Namba 4, 5 na 10 Mdhibiti
na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali kuchunguza kama wakati 30
wa kufungua
Akaunti ya BOT (Akaunti ya Tegeta ESCROW)
Mechmar
ilikuwa inamiliki IPTL. Pia, kuthibitisha kwamba kampuni
ya Mechmar
ilikuwa imehamishia umiliki wake kwa Kampuni ya
PAP kabla ya
kufilisiwa, na kwamba sasa PAP inamiliki IPTL.
Katika
Hadidu Rejea hizi masuala mawili makubwa yamejitokeza,
nayo ni
mchakato wa PAP kumiliki IPTL na suala la malipo ya kodi
ya ongezeko
la mtaji (capital gain) na ushuru wa stempu (stamp
duty). Kwa
upande wa umiliki wa IPTL, Taarifa ya Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za Serikali imeonyesha kuwa IPTL
ilikuwa
inamilikiwa na Kampuni mbili, Mechmar (hisa 7) na VIP
(hisa 3) kwa
mtaji wa Sh. 35,000 kutoka Mechmar na Sh. 15,000
kutoka VIP.
Baadaye Mechmar iliuza hisa zake 7 kwa Kampuni
iliyosajiliwa
British Virgin Islands (BVI) iitwayo Piper Link kwa USD
milioni 6.
Hata hivyo,
uuzaji huu wa hisa kutoka Mechmar kwenda Piper Link
ulipingwa
katika Mahakama Kuu ya British Virgin Islands kwa
Shauri
lililofunguliwa na Martha Renju (ambaye anawakilisha
masilahi ya
Benki ya Standard Chartered Hong Kong). Moja ya
maombi
yaliyotolewa Mahakamani ni kuwa Mahakama ishikilie Hati 31
ya hisa
husika mpaka shauri la msingi litakapomalizika.16 Siku hiyo
hiyo shauri
lilipofunguliwa, tarehe 8 Novemba, 2010 Mahakama
ilitoa amri
ya kusitisha uuzaji wa hisa hizo saba za Mechmar
kwenda Piper
Link na kuamuru Piper Link iwasilishe Mahakamani
hapo Hati ya
hisa 7 za IPTL zinazodaiwa kuuzwa kwake. Taarifa ya
Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali imebainisha pia
kuwa baada
ya uamuzi wa mwisho kutolewa, tarehe 11 Aprili,
2014
Mahakama ilimkabidhi Martha Renju Hati ya hisa saba (7) za
Mechmar kwa
17barua ya Msajili wa Mahakama Kuu ya BVI
inayosomeka:
“This is to
certify that the Share Certificate No. 01 with
07 shares as
defined in the Statement of Claim being
held in
Custody by The Court in the above matter be
returned to
Maples and Calder on behalf of the
Claimant.”18
16 BVIH COM 2010/147
18 Barua ya
tarehe 13 Aprili, 2011 kutoka kwa Msajili wa Mahakama Kuu ya BVI kwenda kwa
Mawakili
wa Martha
Rethu – Maples and Calder. Barua hii ni Kielelezo Namba 64 katika Taarifa ya
Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za Serikali.32
Katika
mahojiano ya Kamati na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za
Serikali, ilithibitishwa kuwa mpaka sasa Hati ya hisa
saba (7) za
Mechmar kwenye IPTL bado ziko mikononi mwa Benki
ya Standard
Chartered Hong Kong.19
Mheshimiwa
Spika, umiliki wa hisa unakamilika pale ambapo
muuzaji
anamkabidhi mnunuzi Hati ya hisa husika, vinginevyo
mnunuzi
anakuwa amenunua “hisa hewa”. Pamoja na ukweli huu
bado Piper
Links tarehe 21 Oktoba, 2011 ilimuuzia PAP hisa zile
saba kwa
gharama ya USD 20 milioni. Swali linalojitokeza hapa ni
kuwa
unawezaje kuuza kitu usichonacho? Ni wazi kuwa kwa kuwa
Piper Links
hakuwa mmiliki halali wa hisa saba (7) za Mechmar
kwenye
Kampuni ya IPTL alichonunua PAP ni “hisa hewa” na
kumiliki
Kampuni hewa.
Mheshimiwa
Spika, Mchakato huo umeifanya Kamati kuhoji
uhalali wa
PAP kuchukua fedha za ESCROW kwa madai kuwa yeye
ndiye
Mmiliki mpya wa IPTL. Kutokana na uchambuzi tuliofanya
hapo juu
kinachojitokeza ni kuwa hata kama kulikuwa na uhalali
19 Mahojiano ya Kamati na Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali tarehe 19 Novemba, 201433
kwa IPTL
kulipwa sehemu ya fedha zilizokuwa kwenye Akaunti ya
Tegeta
ESCROW bado PAP hakustahili kulipwa fedha hizo.
Mheshimiwa
Spika, Kutokana na mahojiano kati ya Kamati na
Kamishina
Mkuu wa TRA ilibainika kwamba Kampuni ya Piper Links
haijulikani
sio tu British Virgin Islands bali hata nchi nyingine.20
Kamati
haielewi ni jinsi gani taasisi kubwa kama Benki Kuu ya
Tanzania,
Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Fedha, Ofisi ya
Mwanasheria
Mkuu wa Serikali na nyingine zilizohusika katika suala
hili, na
ambazo tunaamini zimesheheni Watendaji wenye weledi,
zimewezaje
kushindwa kufanya uchunguzi wa kina (due diligence)
ambao
ungewezesha utata huu kugundulika na kuepuka
kudanganywa
na PAP.
Mheshimiwa
Spika, Kamati imejiridhisha kuwa kitendo cha
Kampuni ya
Piper Links kukiuka amri ya Mahakama ya British Virgin
Islands
ndiyo kilipelekea Bw. Harbinder Singh Sethi kufanya
udanganyifu
uliotokea. Kwa maana hiyo Piper Links ni chanzo
kikubwa cha
yaliyotokea. Ikumbukwe kuwa Piper Links na
Mechmar
walilipa kodi ya ongezeko la mtaji (capital gain tax) siku
20 Ndg. Rished Bade, tarehe 19 Novemba, 201434
moja (tarehe
6 Desemba, 2013) na kwenye tawi moja la Benki ya
CRDB na wote
waliwakilishwa na mtu mmoja aliyewasilisha nyaraka
za kughushi
na kukwepa kodi ya ongezeko la mtaji iliyopaswa
kulipwa.
2.3.1Kodi iliyopaswa
kukusanywa iwapo mauzo ya hisa 7 za
Mechmar
kwenda Piper Links na baadaye kwenda PAP
yangekuwa
halali
Mheshimiwa
Spika, uchambuzi wa kamati umeainisha dosari za
kisheria za
uhamishaji wa hisa za Mechmar kwenda Piper Links na
baadaye
Piper Links kwenda PAP. Dosari ambazo zinafanya
mchakato huo
mzima kukosa uhalali wa kisheria. Hata hivyo
endapo
mchakato huu ungekuwa halali ulipaswa kuzingatia sheria
za kodi
hususan Sheria ya Kodi ya Mapato kama ilivyorekebishwa
na Sheria ya
Fedha ya mwaka 2012.
Mheshimiwa
Spika, kama ilivyoelezwa hapo awali, katika
uchambuzi wa
Hadidu za Rejea 4, 5 na 10 masuala ya kodi nayo
yaliyojitokeza,
hususan kodi ya ongezeko la mtaji na ushuru wa
stempu.
Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
alifafanua
kuwa kodi ya ongezako la mtaji ni kodi ambayo hutozwa 35
kwenye faida
inayotokana na mauzo ya mali na uwekezaji na katika
faida
itokanayo na mauzo ya hisa.
Mheshimiwa
Spika, Kamati ilishangazwa na kusikitishwa na kiasi
kikubwa cha
kodi kilichopotea au kuibiwa kwa makusudi katika
mchakato
mzima wa ukusanyaji wa kodi husika. Kama ilivyoelezwa
hapo awali
kuwa, tarehe 9 Septemba, 2012 Kampuni ya Mechmar
iliuza hisa
saba (7) kwa Piper Links ilizokuwa inamiliki katika
Kampuni ya
IPTL kwa bei ya USD milioni 6.
Mheshimiwa
Spika, hata hivyo, taarifa zilizowasilishwa Mamlaka
ya Mapato
Tanzania (TRA) kwa ajili ya kukokotoa kiasi cha kodi ya
ongezeko la
mtaji ambacho Mechmar ilitakiwa kulipa, zinaonyesha
kuwa hisa
hizo zimeuzwa kwa Sh. milioni 6. Kwa kutumia taarifa
hizo, TRA
ilikokotoa kodi husika na hivyo Mechmar ilipaswa kulipa
kodi ya
ongezeko la mtaji Sh. 1,919,988,800 na siyo Tsh.596,500
ilizolipa.
Aidha, kwa upande wa ushuru wa stempu Mechmar
ilipaswa
kulipa shilingi 96 milioni na siyo shilingi elfu 60 ilizolipa.
Hivyo jumla
ya kodi iliyopotea kwa maana ya kodi ya Ongezeko la
Mtaji na
ushuru wa stempu ni shilingi 2,015,988,800. 36
Mheshimiwa
Spika, hisa kutoka Piper Links kwenda PAP ziliuzwa
kwa gharama
ya USD milioni 20, lakini taarifa zilizopelekwa TRA
zilionyesha
kuwa hisa hizo zimeuzwa kwa USD 300,000. Kwa
mantiki hiyo
Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali
inaonyesha kuwa Piper Links ilitozwa na kulipa kodi ya
ongezeko la
mtaji kiasi cha Sh. 47,940,000 na Sh. 4,800,000 kama
ushuru wa
stempu (stamp duty)’. Katika mahojiano, Kamishna
Mkuu wa TRA
aliifahamisha Kamati kuwa kwa gharama ya USD
milioni 20
kiasi cha kodi ya ongezeko la mtaji kilichotakiwa kulipwa
ni Sh.
6,399,977,600 na sio Sh. 47,988,800, na kwa upande wa
ushuru wa
stempu ‘stamp duty’ kiasi kilichotakiwa kulipwa ni Sh.
320,000,000
na siyo Sh. 4,800,000. Kwa maana hiyo jumla ya kodi
iliyopotea
kwa maana ya kodi ya ongezeko la mtaji na ushuru wa
stempu
(stamp duty)’ ni Sh. 6,667,188,800.
Mheshimiwa
Spika, jumla ya kodi iliyopotea kutokana na uuzaji
wa hisa za
Mechmar kwenda Piper Links na za Piper Links kwenda
PAP ni jumla
ya shilingi 8,683,177,600.
Mheshimiwa
Spika, mahojiano ya Kamati na Kamishna Mkuu wa
TRA yalilenga,
pamoja na mambo mengine, kufahamu jitihada 37
zilizofanywa
na watendaji wa TRA kuthibitisha uhalali wa taarifa
zilizowasilishwa
kwao (due diligence) kabla ya kukokotoa kiasi cha
kodi ya
ongezeko la mtaji kwa miamala yote miwili yaani Mechmar
– Piper
Links na Piper Links – PAP. Kamati ilipotaka kufahamu ni
hatua gani
zimechukuliwa kwa watumishi waliohusika na zoezi hilo,
hatua
zinazochukuliwa na TRA ili kukusanya kodi iliyopotea na
kufuta Tax
Clearance Certificate, ilijulishwa kuwa kwanza TRA
ilishtushwa
na taarifa kuwa kulikuwa na mikataba miwili yenye bei
tofauti
ambayo iliandaliwa na wahusika ili iwawezeshe kukwepa
kodi, na
kwamba Kampuni ya VIP imeuza hisa zake 3 ilizokuwa
ikizimiliki
kwenye kampuni ya IPTL kwa bei ya USD milioni 75
wakati PAP
hiyo hiyo iliuziwa na Piper Links hisa 7 kwa USD
300,000.
Hivyo, TRA ilifanya uchunguzi wake ikiwa ni pamoja na
kuhoji watu
mbalimbali akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa PAP Bw.
Harbinder
Singh Sethi (Kiambatisho Na. 7).
Mheshimiwa
Spika, Kamati ilipokea taarifa ya uchunguzi wa
ndani
iliyofanywa na TRA ambao ulithibitisha ukwepaji mkubwa wa
kodi na
udanganyifu wa mikataba. Kamati imekubaliana na uamuzi
wa TRA
kuondoa hati za kodi kwa IPTL na hivyo kuna uwezekano
kuwa kuanzia
tarehe 24 Novemba, 2014 PAP haitokuwa tena 38
mmiliki wa
IPTL mpaka hapo watakapofuata upya tararibu za
kisheria na
TRA kukusanya kodi stahiki.
2.4 KIASI
CHA FEDHA KILICHOKUWEMO NA KILICHOLIPWA
KUTOKA
AKAUNTI YA TEGETA ESCROW
Mheshimiwa
Spika, Hadidu rejea ya 7 ilimtaka Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za Serikali kuchunguza kiwango cha
fedha
kilichokuwepo kwenye Akaunti Maalumu ya ESCROW, wakati
BOT
inahamisha fedha zilizokuwepo katika akaunti hiyo kwenda
IPTL,
kiwango cha cha fedha kilichopaswa kuwemo katika akaunti
hiyo maalumu
ya BOT pamoja na kiwango cha fedha
kinachopaswa
kulipwa zaidi kutoka TANESCO. Hii ilihusisha pia
kuchunguza
na kutoa taarifa kuhusu Kiasi cha fedha kilichowekwa
na kila
mhusika hadi uamuzi wa mahakama Kuu ya Tanzania
ulipotolewa.
Mheshimiwa
Spika, hadi kukamilika kwa Ukaguzi wa Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za Serikali, Kamati imebaini kuwa kiasi
kilichokuwepo
kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW ni Sh. 39
167,251.892.330
na USD 22,198,544. Baada ya Uhakiki wa
Akaunti ya
Tegeta ESCROW hadi tarehe 05 Novemba, 2013 ilikuwa
na Kiasi cha
Sh. 8,020,522,330 na USD 22,198,544. Aidha,
kulikuwa na
Kiasi cha Sh. 159,231,370,000 kilichojumuisha fedha
zilizowekezwa
kwenye hati fungani (Treasury Bills) Sh.
148,071,081,052
zenye riba ya Sh. 11,160,288,948.21
Mheshimiwa
Spika, malipo yote ya Sh. 167,251,892,330 na USD
22,198,544
zililipwa kwa Kampuni ya PAP kupitia Akaunti Na.
912000012534
ya USD na Akaunti Na. 9120000125294 ya Shilingi
za
kitanzania katika Benki ya Stanbic zilizofunguliwa tarehe 27
Novemba, 2013
maalum kwa ajili ya kupokea fedha hizo. Hivyo
jumla ya
fedha iliyotolewa kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW na
kulipwa kwa
PAP ni shilingi 203,102,540,890.22
Mheshimiwa
Spika, uchunguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za
Serikali umebainisha kuwa hadi kufikia tarehe 05 Juni,
2007 kiasi
kilichokuwa kwenye akaunti ni jumla ya Sh. 118,
291,827,820
japokuwa TANESCO walipinga gharama za tozo, lakini
21 Taarifa ya CAG kuhusu Akaunti ya Tegeta ESCROW ukurasa wa 35
22 Kiwango cha kubadilishia fedha Dola 1 kwa wastani wa shilingi 1,615 (chanzo BOT tarehe 28/11/2013)40
waliendelea
kulipa gharama hizo kati ya mwaka 2004 na 2007.
Aidha,
uhakiki wa Ankara za IPTL za hadi tarehe 01 Juni, 2014
zilizopatikana
TANESCO zilibainisha kuwa Akaunti ya Tegeta
ESCROW
ilitakiwa kuwa na Sh. 306,675,081,939.
Mheshimiwa
Spika, kuhusu suala la fedha zilizowekwa katika
Akaunti ya
Tegeta ESCROW, uhakiki wa wakaguzi ulibainisha kuwa
kulikuwa na
jumla ya Sh. 182,771,388,687, kati ya hizo TANESCO
iliweka
Kiasi cha Sh. 142,008,357,587 na Wizara iliweka Kiasi cha
Sh.
40,763,031,100.
Mheshimiwa
Spika, kwa mujibu wa ankara zilizotolewa na IPTL
inaonekana
TANESCO ilipaswa kuweka Kiasi cha Sh.
123,903,693,252
zaidi ya fedha ilizoziweka katika Akaunti ya
Tegeta
ESCROW ikiwa ni tofauti kati ya Kiasi ilichotakiwa kuweka
cha Sh.
306,675,081,939 na Kiasi kilichowekwa cha Sh.
182,771,388,687.
Mheshimiwa
Spika, pamoja na riba ya Sh. 11,160,288,948
iliyopatikana
katika uendeshaji wa Akaunti ya Tegeta ESCROW,
fedha hizo
zote zililipwa kwa Kampuni ya PAP, huku wakala wa 41
uendeshaji
wa Akaunti husika (BOT) hakupewa kiasi chochote
japokuwa
walitumia gharama kubwa katika kesi zilizofunguliwa
dhidi ya Akaunti
hiyo na gharama za kawaida za uendeshaji.
2.5 USHIRIKI
WA TAASISI ZA SERIKALI NA WATU BINAFSI
KATIKA
UTOAJI FEDHA KATIKA AKAUNTI YA TEGETA
ESCROW
2.5.1 Benki
Kuu ya Tanzania (BOT)
Mheshimiwa
Spika, Hadidu ya Rejea ya Pili ilihusu wajibu wa
Benki Kuu ya
Tanzania kama ulitekelezwa ipasavyo katika
mchakato wa
kutoa fedha kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW.
Miongoni mwa
maswali muhimu kwa Kamati ilikuwa ni kwanza
kufahamu
kwamba katika suala la Akaunti ya Tegeta ESCROW
Benki Kuu
ilikuwa na Wajibu gani na iliutimizaje? Ama je, ilikuwa
sahihi namna
Wajibu huo ulivyotimizwa?
Uchambuzi wa
Kamati katika Taarifa ya Ukaguzi Maalum na
Makubaliano
ya Uendeshaji wa Akaunti ya Tegeta ESCROW42
yaliyokuwepo
kati ya Serikali na IPTL umebainisha kwamba Benki
Kuu ya
Tanzania ilikuwa na wajibu ufuatao:
a) Kufungua
na kuhifadhi Akaunti ya Tegeta ESCROW katika
sarafu
mbili, yaani Shilingi ya Tanzania na USD.
b) Kupokea,
kuhifadhi na kuwekeza fedha za Akaunti ya Tegeta
ESCROW;
c)
Kushughulikia kutolewa kwa fedha hizo kwa kuzingatia masharti
yaliyopo
katika Sehemu ya Nne ya Makubaliano ya Akaunti ya
Tegeta
ESCROW (Kiambatisho Na. 3) ambayo ni kujiridhisha
kwamba
mgogoro kuhusu capacity charges kati ya IPTL na
TANESCO
umetatuliwa, na kwamba Makubaliano yanayohusiana
na utatuzi
wa mgogoro huo yanakuwepo katika Hati iliyosainiwa
na
kuwasilishwa kwake kwa ajili ya mchakato wa utoaji wa
fedha hizo.
d) Kutoa
taarifa za kila robo Mwaka kwa IPTL na TANESCO kuhusu
hali ya
Akaunti.23
23Kipengele Na. 2 cha Makubaliano ya Uendeshaji wa Akaunti ya Tegeta ESCROW43
Mheshimiwa
Spika, kabla ya kuchambua namna Benki Kuu
ilivyotimiza
wajibu wake kama ulivyoelezewa hapo juu tujielekeze
kidogo
kwenye ufahamu wa dhana nzima ya Akaunti ya Tegeta
ESCROW.
Akaunti ya aina hii hutumika kuhifadhi kiasi cha fedha
pale
washirika wa mkataba wa kibiashara wanapokuwa kwenye
mgogoro na
hivyo kuhitaji kutunza fedha zinazotokana na
utekelezaji
wa mkataba husika kwenye jambo linalobishaniwa ili
kusubiri
uamuzi wa msuluhishi au maridhiano ya washirika.
Mheshimiwa
Spika, baada ya kuyafahamu majukumu ya msingi
ya Benki Kuu
ya Tanzania katika Akaunti ya Tegeta ESCROW,
Kamati
ilijielekeza katika kufahamu namna Benki Kuu ya Tanzania
ilivyotimiza
wajibu huo. Uchambuzi wa Kamati umebaini kwamba
ili
kutekeleza wajibu ambao Benki Kuu ya Tanzania ilikuwa nao
katika
Akaunti ya Tegeta ESCROW, iliishauri Serikali kujiridhisha
zaidi kabla
ya kutoa fedha kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW juu
ya mambo
yafuatayo:
(a) Kuwepo
kwa ushahidi kwamba hisa zilizokuwa zinamilikiwa
na Mechmar
zimenunuliwa na PAP na manunuzi husika
yamesajiliwa
na BRELA;44
(b) Kuwepo
na ushahidi kuwa mgogoro uliokuwepo kati ya IPTL
na TANESCO
kuhusu capacity charges umepatiwa suluhu, na
imeafikiwa
kwamba IPTL ilipwe fedha husika;
(c)Wizara ya
fedha ilete ushauri kuhusiana na uwepo wa Kodi ya
Ongezeko la
thamani katika fedha zilizopo katika Akaunti ya
Tegeta
ESCROW.
(d) Serikali
kupatiwa kinga ya IPTL ili kujiepusha na uwezekano
wa kushitakiwa
na IPTL hapo baadaye kutokana na Benki Kuu
kutoa fedha
za IPTL.24
Mheshimiwa
Spika, baada ya uchunguzi wa Kamati kuhusiana
na ushauri
uliotolewa na BOT kwa Serikali yafuatayo yalibainika:
(i) Kuhusu
kuwepo ushahidi kwamba hisa zilizokuwa
zinamilikiwa
na MECHMAR zimenunuliwa na PAP na
manunuzi
husika yamesajiliwa na BRELA,
24Ushauri wa Benki Kuu ulitolewa kwenye Kikao
cha maridhiano kilichoitishwa kwa dharura na Katibu Mkuu wa
Wizara ya
Nishati na Madini Bw. Eliakim Maswi kupitia barua yake yenye kumbu Na. CBD.
88/417/31 ya tarehe
23 Septemba,
2013 kwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Servacius Likwelile.45
kilichowasilishwa
kwa Gavana wa Benki Kuu ni Deed of
Assignment
of Shares na Mkataba wa kuuza hisa kati ya PAP na
Piper Link
(Kiambatisho Na. 8) na siyo hati halisi ya umiliki
wa hisa.
(ii)Kuhusu
ushahidi kuwa mgogoro uliokuwepo kati ya
IPTL na
TANESCO kuhusiana na overcapacity charges
umepatiwa
suluhu na imeafikiwa kwamba IPTL ilipwe
fedha
husika, Kamati yangu, imethibitisha kwamba hakukuwa
na
makubaliano kati ya TANESCO na IPTL ambao ndiyo
washirika wa
Akaunti ya Tegeta ESCROW. Uthibitisho huu
unatokana na
maelezo ya kipengele Na. 3.2 na 7.1 cha Taarifa
ya Kamati ya
Wataalam iliyokutana tarehe 24 Septemba, 2013
kuhusu
utoaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta ESCROW.
Taarifa hiyo
ya Wataalam ndiyo iliyotumika kama kielelezo cha
ushahidi
kuwa mgogoro uliokuwepo kati ya IPTL na TANESCO
kuhusiana na
capacity charges umepatiwa suluhu jambo
ambalo ni
kinyume na yaliyomo katika kipengele 3.2 na 7.1 cha
Taarifa
husika (Kiambatisho Na. 9). Vipengele hivyo
vinasomeka
kama ifuatavyo:-46
“3.2
Discussions between TANESCO and IPTL on
disputed
capacity charges are ongoing, therefore,
the team
could not make concrete observation on
this issue.”
“7.1 TANESCO
and IPTL should conclude the
ongoing
verification of the outstanding capacity
charges
invoices and issues relating to it and
submit a
joint resolution to PS-MEM as soon as
possible to
enable other process to take off.”
Mheshimiwa
Spika, Kamati imethibitisha kuwa uthibitisho na
vielelezo
alivyopata Gavana wa Benki Kuu katika kufikia
maamuzi ni
Taarifa ya Kamati ya Wataalam kama ilivyotajwa
hapo juu. Hata
hivyo Kamati imefanikiwa kuona nyaraka
iliyosainiwa
na Ndugu John Kabadi kwa niaba ya TANESCO na
Mwakilishi
wa Kampuni ya IPTL ya tarehe 8 Oktoba, 2013
kwamba
wamekubaliana kuwa fedha zote za ESCROW zilipwe
kwa IPTL
mara moja. Uamuzi huu uliwasilishwa na Mwenyekiti
wa Bodi ya
TANESCO kwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na 47
Madini
tarehe 9 Oktoba, 2013.25 Makubaliano haya hayaonekani
katika
mawasiliano yoyote ya Kiserikali na badala yake Kamati
iliona
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini akiingia
makubaliano
na IPTL ya utoaji wa fedha katika Akaunti ya
Tegeta
ESCROW (Kiambatisho Na. 10).
(iii)Kuhusu
Wizara ya fedha kupeleka ushauri kuhusiana na
uwepo wa
Kodi ya Ongezeko la thamani katika fedha
zilizopo
katika Akaunti ya Tegeta ESCROW, Kamati
haikupata
ushahidi kwamba Wizara ya Fedha ilishauri kuhusu
masuala ya
kodi ya ongezeko la thamani katika fedha
zilizokuwepo
kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW pamoja na
kushauriwa
na TRA kwa barua Na. 100-221-969/214 ya tarehe
29 Oktoba,
2013 iliyonakiliwa pia kwa Gavana wa Benki Kuu.
Katika barua
hiyo TRA waliainisha uwepo wa kodi ya ongezeko
la thamani
ya Sh. 26,946,487,420.80 kwenye Akaunti ya
Tegeta
ESCROW (Kiambatisho Na. 11). Hata hivyo, barua
ya TRA Kumb.
Na. TRA/CG/L.3 ya tarehe 4 Februari, 2014 kwa
Katibu Mkuu
wa Wizara ya Fedha ilionesha kuwa kiasi cha kodi
25barua yenye Kumb. Na. SEC.427/IPTL/10/201348
kinachodaiwa
ni Sh. 21,713,935,720.75. (Kiambatisho Na.
12).
Mheshimiwa
Spika, Kamati imebaini kuwa Mwanasheria Mkuu
wa Serikali
kwa barua yenye Kumb Na. AGCC/E.080/6/70 ya
tarehe 18
Novemba, 2013 alimthibitishia Gavana kuwa hakukuwa
na kodi ya
Serikali katika fedha zilizokuwa kwenye Akaunti ya
Tegeta
ESCROW na kwamba fedha hizo zihamishiwe IPTL ili
Serikali
ijinasue na mashauri yasiyo na tija kwake.
Mheshimiwa
Spika, Kamati inaona ushauri wa Mwanasheria
Mkuu wa
Serikali ulimpotosha Gavana kwa sababu kwa mujibu wa
kifungu 5(4)
cha Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, 2006
capacity
charges hukatwa kodi.
(iv)Kuhusu
Serikali kupatiwa kinga kutoka IPTL dhidi ya
madai
yanayoweza kujitokeza baada ya fedha katika
Akaunti ya
Tegeta ESCROW kulipwa.49
Mheshimiwa
Spika, kuhusiana na kinga hii, Harbinder Singh
Sethi ambaye
ni Mkurugenzi Mtendaji wa PAP alitoa Kinga kwa
hati
iliyotolewa tarehe 27 Oktoba, 2013. Hata hivyo, kwa
mujibu wa
taarifa za TRA zilizowasilishwa kwa Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za Serikali uhalali wa PAP kumiliki
hisa 7 za
Piper Links investiment ulitiliwa mashaka na TRA kwa
kuwa PAP
haikuwa na Tax Clearance Certificate ambayo ndiyo
hutumika kwa
Kampuni kusajiliwa BRELA na hatimaye
kutambuliwa
na Wizara ya Nishati na Madini. Kwa maana hiyo
PAP
haikutimiza masharti ya Kifungu cha 90(2) cha Sheria ya
Kodi ya
Mapato ambacho kinasomeka kama ifuatavyo:
“The
installment referred to in subsection 1 shall be
paid before
the title to an investment asset is
transferred,
and appropriate authorities for
registration,
transfer or approval shall not register
such
transfer or change of name without the
production
of a certificate of the Commissioner
certifying
that the installment has been paid or that
no
installment is payable.”50
Mheshimiwa
Spika, Kifungu hiki ambacho kilifanyiwa
marekebisho
kwa Sheria ya Fedha ya mwaka 2012 (Sheria Na
8 ya 2012)
kimeweka utaratibu wa kuwezesha Serikali kutoza
kodi pale
makampuni yanapouziana Hisa nje ya nchi. Sheria hii
inataka
kwanza kupata hati ya TRA (Tax Clearance Certificate)
kabla ya
BRELA kusajili hisa hizo na kabla ya mamlaka za
uthibitisho
kuthibitisha. Wakati Wizara inaingia makubaliano ya
kutoa fedha
za Akauti ya Tegeta ESCROW kwa PAP na wakati
PAP
wanalipwa fedha hizo, Kampuni hiyo haikuwa na uhalali
wa kumiliki
IPTL. Hivyo BRELA, Wizara ya Nishati na Madini,
TANESCO na
BOT walikiuka Sheria ambazo kama zingefuatwa
pengine leo
tusingekuwa tunajadili suala hili.
Mheshimiwa
Spika, Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana
kutoka TRA,
imebainika kuwa mpaka malipo ya kwanza katika
Akaunti ya
Tegeta ESCROW yanafanyika tarehe 28 Novemba,
2013 PAP
haikuwa na Tax Clearance Certificate ambayo
ingeiwezesha
kumiliki hisa 7 za IPTL. Taarifa hizo zinaeleza
kwamba
tarehe 23 Desemba,2013 kwa kutumia mikataba ya
kughushi PAP
ilipata Tax Clearance Certificate No. 004965651
(Mechmar
kwenda Piper Links) na 0049657 (Piper Links
kwenda PAP).
Hata hivyo
pamoja na kutokuwa na Tax Clearance Certificate
bado Kampuni
ya PAP ilitambuliwa na Wizara ya Nishati na
Madini
pamoja na uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania wa
tarehe 5
Septemba, 2013 kupitia Hukumu ya Mheshimiwa Jaji
J.H.K.
Utamwa iliyokabidhi shughuli zote za IPTL kwa PAP na
kuiwezesha
kulipwa fedha zote zilizokuwa katika Akaunti ya
Tegeta
ESCROW.
Mheshimiwa
Spika, Kamati imethibitisha juhudi kubwa
aliyofanya
Gavana wa Benki Kuu kutaka kujiridhisha vya kutosha
kabla ya
kuruhusu fedha hizo kutolewa. Hata hivyo, alipata
maagizo
kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwamba fedha
hizo zitoke
(Kiambatisho Na.17).
2.5.2 Bodi
ya Wakurugenzi ya TANESCO
Mheshimiwa
Spika, katika suala la utoaji wa fedha katika
Akaunti ya
Tegeta ESCROW, Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO
ilikutana
katika Kikao cha52
dharura
mnamo tarehe 19 Septemba, 2013 ili Kujadili suala la
utolewaji wa
fedha katika Akaunti ya Tegeta ESCROW. Katika
Kikao hicho,
Menejimenti ya TANESCO iliwasilisha taarifa Na. 447
ambapo
ilitahadharisha juu ya utolewaji wa fedha katika Akaunti
hiyo kabla
ya kuhitimishwa kwa Shauri la madai ya msingi ya
TANESCO juu
ya capacity charges (Kiambatisho Na. 13).
Mheshimiwa
Spika, siku hiyo hiyo ya tarehe 16 Septemba, 2013
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO Jenerali
Mstaaafu
Robert Mboma, alimwandikia Katibu Mkuu Wizara ya
Nishati na
Madini akimwarifu kuwa TANESCO itafuata maelekezo
ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwamba washirika wa Akaunti
ya Tegeta
ESCROW wakae pamoja kutatua mgogoro wa capacity
charges ili
kubaini kiasi kinachostahili kulipwa IPTL na
kinachotakiwa
kurejeshwa TANESCO.
Mheshimiwa
Spika, Kamati imepata shaka kubwa juu ya uamuzi
wa haraka
bila kufanya uchunguzi wa kina, kwa Bodi ya
Wakurugenzi
ya TANESCO kufanya vikao viwili mfululizo ili
kuruhusu
uchotwaji wa fedha za ESCROW. Kikao cha kwanza
kilifanyika
mnamo tarehe 16 Septemba, 2013 ambapo Bodi ilikuwa 53
na msimamo
sawa na wa Menejimenti kuwa fedha za ESCROW
zisitoke,
Kikao cha pili cha dharura kikafanyika tarehe 19
Septemba,
2013 ambapo Bodi iliazimia pia kuwa fedha zisitoke.
Mheshimiwa
Spika, kati ya tarehe 14 hadi 20 Septemba, 2013
TANESCO
ilimuagiza Mwanasheria wake Bw. Godwin Ngwilimi
aende nchini
Malaysia kufanya “due diligence” kuhusu uhalali wa
Kampuni ya
PAP kumiliki IPTL. Wakati huo Bodi ya TANESCO
ilikuwa na
vikao vya haraka haraka “supersonic speed” ambavyo
vilikubali
haraka bila hata kusubiri ushauri wa Mtumishi wao
kwamba fedha
za ESCROW wapewe PAP.
Mheshimiwa
Spika, katika barua ya Mkuu huyo wa Sheria wa
TANESCO
kwenda kwa Mkurugenzi Mtendaji yenye Kumbukumbu
Na.
SEC.427/IPTL/11/2013 ya tarehe 7 Novemba, 2013 alisema:
“Nilishuhudia
nyaraka kwamba Piper Link ilinunua
hisa za
Mechmar na katika mauziano hayo Kampuni
hiyo
iliwakilishwa na Bw. Harbinder Singh Sethi hivyo
huyu bwana
ndiye Piper Link na ndiye PAP”54
Hata hivyo,
Bodi ya TANESCO haikukubaliana na ushauri huo na
hatimaye
kumwachisha kazi Bwana Godwin Ngwilimi. Kosa lake
kubwa ni
kutahadharisha kuwa nchi inatapeliwa. Kama ushauri
huu
ungefuatwa tusingefika hapa tulipo leo kwa sababu hadi hapa
fedha katika
Akaunti ya Tegeta ESCROW zilikuwa hazijatolewa.
Mheshimiwa Spika,
Hata hivyo, mnamo tarehe 9 Oktoba 2013
Mwenyekiti
wa Bodi ya TANESCO alimuandikia barua Katibu Mkuu
Wizara ya
Nishati na Madini yenye Kumbukumbu Na.
SEC.427/IPTL/10/2013
akimuarifu mambo yafuatayo;
a) Bodi
ilipokea kutoka IPTL madai ya kiasi cha ziada cha dola
za
kimarekani 45,485,719.97 pamoja na riba na tozo ya
jumla ya
dola za kimarekani 33,564,004.53 na hivyo kufanya
jumla ya
madai za ziada ya kilichopaswa kulipwa kwenye
akaunti ya
Tegeta ESCROW kuwa USD 79,049,724.50. Hivyo,
kuiagiza
Menenjimenti ya TANESCO kufanya uhakiki wa kiasi
hicho.
b) Baada ya
Menejimenti kuwa imehakiki madai hayo, Bodi
imejiridhisha
kuwa IPTL sio tu inastahili kulipwa fedha 55
zilizokuwa
kwenye akaunti ya Tegeta ESCROW bali pia
wanastahili
kulipwa kiasi cha tozo na riba kilichotajwa hapo
juu.
Mheshimiwa
Spika, huku ikieleweka kuwa Bodi ya TANESCO
haikuwa
imefanya maridhiano na IPTL kuhusiana na mgogoro wa
‘over
capacity charges’ unaohusu fedha zilizokuwa kwenye akaunti
ya Tegeta
ESCROW, Bodi ilimuarifu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati
na Madini
kuhusu makubaliano mapya yaliyofikiwa baina yake na
IPTL kuhusu
kulipa ziada husika kwenye Akaunti ya Tegeta
ESCROW kwa
njia mbadala zifuatazo:
a) Kulipa
fedha za ziada dola za kimarekani 45,485,719.97 iwapo
TRA
itakubali kusamehe kodi ya USD 33,564,004.53 ambayo ni
sawa na
kiasi cha tozo na riba ambacho TANESCO anadaiwa na
IPTL. Au,
b) Kulipa
USD 79,049,724.50 iwapo TRA haitosamehe kodi ya USD
33,564,004.53
ambayo ni sawa na kiasi cha tozo na riba
ambacho
TANESCO anadaiwa na IPTL (Kiambatisho Na. 14
na 15).56
Mheshimiwa
Spika, Kamati imeshangazwa na makubaliano hayo
yaliyofikiwa
kati ya Bodi ya TANESCO na IPTL, ikizingatiwa kuwa
mgogoro wa
msingi uliohusu madai ya TANESCO kutozwa capacity
charges
kubwa na IPTL haukupatiwa ufumbuzi kama ilivyoelekezwa
na ICSID.
Kamati imefanikiwa kuona muhtasari wa kikao cha
Menejimenti
ya TANESCO na IPTL kilichofanyika tarehe 8 Oktoba,
2013 katika
Hoteli ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam ambapo
imebaini
kuwa walizungumzia mambo yafuatayo:
a) Hukumu ya
Mahakama Kuu ya Tanzania chini ya Mhe. Jaji
Utamwa, J
iliyotolewa tarehe 5 Septemba 2013
b)
Uhamishaji wa mali za IPTL ikijumuishwa Mitambo ya kufua
Umeme na
madai ya fedha za IPTL kwa TANESCO yaliyowekwa
kwenye
Akaunti ya Tegeta ESCROW kwenda kwa PAP.
c) Madai ya
ziada ya IPTL kwa TANESCO kama yalivyoainishwa
hapo juu.57
Mheshimiwa
Spika, hakukuwa na uthibitisho kuwa walizungumzia
suala la
kutafuta maridhiano kuhusu madai ya TANESCO kutozwa
capacity
charges kubwa ili kuwezesha kutolewa kwa fedha
zilizokuwemo
kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW ingawa inaonyesha
kwenye
mawasiliano mbalimbali yaliyofanyika kati ya Serikali,
TANESCO na
IPTL walikuwa wanajua kuwa wanapaswa kufanya
maridhiano
katika suala husika.
Mheshimiwa
Spika, ni dhahiri kutokana na Bodi ya TANESCO
kukubali
kulipa madai ya ziada wakati madai ya msingi ya IPTL na
TANESCO
(Fedha iliyowekwa kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW)
hayajapatiwa
ufumbuzi, inaonyesha udhaifu wa kiuongozi na
kutanguliza
maslahi binafsi mbele kabla ya maslahi ya Umma. Kamati
inahofu
iwapo makubaliano hayo yatakubaliwa na kutekelezwa,
Serikali
itapoteza fedha nyingi bila manufaa kwa kuendelea kuilipa
IPTL madai
hayo ya ziada.
2.5.3
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya VIP Engineering
Ndg. James
Rugemalira58
Mheshimiwa
Spika, katika suala zima la IPTL, Ndg. James
Rugemalira
anatajwa kama Mkurugenzi Mtendaji wa VIP
Engineering
ambaye alikuwa na hisa 3 kati ya hisa 10 kwenye
IPTL. Kwa
mujibu wa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za
Serikali, mwaka 2004, Ndg. Rugemalira aliufahamisha
uongozi wa
TANESCO kuwa gharama za ‘capacity charges’
wanazotozwa
na IPTL ni za juu tofauti na makubaliano. Taarifa hizi
baadaye
zilithibitishwa na Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO na
kusababisha
Akaunti ya Tegeta ESCROW kufunguliwa kama
tulivyoeleza
hapo awali.
Mheshimiwa
Spika, Bw. James Rugemalira ameonekana
kuhusika
tena na suala la IPTL pale alipofungua Shauri
mahakamani
kuomba kuiondoa IPTL kwenye ufilisi na kisha kuuza
hisa zake
kwa Kampuni ya PAP. Ni baada ya uamuzi wa Mahakama
Kuu kuhusu
shauri hili uliotolewa tarehe 5 Septemba, 2013 ndipo
fedha za
Akaunti ya Tegeta ESCROW zilipotolewa kwa uharaka.
Mheshimiwa
Spika, Kamati imepitia Mkataba wa mauzo ya Hisa
kati ya Kampuni
ya PAP na VIP na kuthibitisha kuwa Waziri wa
Nishati na
Madini Mheshimiwa Prof. Sospeter Muhongo (Mb) ndiye 59
alikuwa
kiungo kati ya Bw. Harbinder Singh Sethi wa IPTL na Ndg.
Rugemalira
wa VIP (Kiambatisho Na. 16). Katika mkataba huo
wa tarehe 19
Agosti, 2013. Ndg. James Rugemalila alithibitisha
kuwa Waziri
wa Nishati na Madini Mhe. Prof. Sospeter Muhongo
alimwomba
kuwasilisha kiasi cha fedha ambacho angependa
kulipwa na
IPTL ili kumaliza Shauri lililokuwepo mahakamani.
Aidha, Bw.
Sethi aliwasilisha kwa Bw. Rugemalira ushahidi
kwamba PAP
imenunua Hisa 7 za Mechmar katika IPTL.
“On 11th
July 2013, the Minister of Energy and
Minerals,
Hon. Dr. Prof. Sospeter Muhongo invited VIP
to submit to
him the amount of money if paid VIP
would
conclusively settle VIP claims against IPTL”.
Mheshimiwa
Spika, mchakato wote wa kutoa fedha katika
Akaunti ya
Tegeta ESCROW ndipo ulipoanza na mauzo ya hisa za
VIP kwenda
PAP na baadaye kuhitimishwa na maamuzi ya
Mahakama Kuu
ya tarehe 5 Septemba, 2013 ambayo ndiyo
yaliyotumika
kuhalalisha utoaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta
ESCROW
tarehe 28 Novemba hadi 5 Desemba, 2013.60
Mheshimiwa
Spika, Baada ya fedha kutolewa kwenye Akaunti
ya Tegeta
ESCROW Ndg. Rugemalira alipata mgao wake wa USD
million 75,
ambazo ndani yake kulikuwa na kodi ya Serikali ambayo
haikukusanywa
na gharama za uendeshaji wa Akaunti ya
ESCROW,
fedha hizo zote zilipelekwa katika Benki ya Mkombozi.
Huko
zilianza kugawiwa kwa watu binafsi. Kamati imearifiwa kuwa
Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amepeleka suala
hilo
TAKUKURU na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU amekiri
kuendelea na
uchunguzi. Kamati pia imekabidhiwa taarifa ya
Benki za
Stanbic na Mkombozi ambazo zimeonyesha namna
ambavyo
fedha zilichukuliwa na watu na makampuni mbalimbali.
Mheshimiwa
Spika, baada ya kupokea taarifa za benki (bank
statements)
kutoka Benki ya Stanbic na Benki ya Mkombozi,
Kamati
ilibaini yafuatayo: -
a) Kuwepo
kwa fedha zilizohamishwa kutoka Akaunti ya PAP
iliyoko
Benki ya Stanbic kwenda Akaunti ya VIP iliyoko katika
Benki ya
Mkombozi.61
b) Kuwepo
kwa fedha taslimu zilizolipwa kwa watu binafsi ambao
majina yao
hayaonekani lakini walifanya miamala mikubwa
kinyume cha
Sheria ya Benki Kuu na Taasisi za Fedha ya
mwaka 2006.
c) Kuwepo
kwa fedha walizohamishiwa watu mbalimbali katika
Akaunti zao
binafsi.
d) Katika
fedha ambazo zimelipwa kwa watu binafsi katika Benki
hizi yapo
majina ya viongozi wa kisiasa, viongozi wa
madhehebu ya
dini, Majaji na watumishi wengine wa Serikali.
Mheshimiwa
Spika, Kamati inajiuliza ni nini mahusiano ya moja
kwa moja
kati ya Viongozi hawa na malipo yaliyotokana na Akaunti
ya Tegeta
ESCROW. Mfano kwa upande wa viongozi wa kisiasa
ambao
waliingiziwa fedha katika akaunti zao binafsi ni; Mhe.
Andrew
Chenge (Mb), ambaye alikuwa Mwanasheria Mkuu wa
Serikali na
sasa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Bajeti,
shilingi bilioni 1.6; Mhe. Anna Tibaijuka (Mb) na Waziri wa 62
Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi shilingi bilioni 1.6; Mhe.
William
Ngeleja (Mb) na ambaye alikuwa Waziri wa Nishati na
Madini
shilingi milioni 40.4 na Ndg. Daniel N. Yona ambaye alikuwa
pia Waziri
wa Nishati na Madini shilingi milioni 40.4; Ndg. Paul
Kimiti
ambaye ni Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Sumbawanga
shilingi milioni
40.4 na Dr. Enos S. Bukuku ambaye alikuwa
Mjumbe wa
Bodi ya TANESCO aliingiziwa shilingi milioni 161.7.
Mheshimiwa
Spika, kwa upande wa Majaji Prof. Eudes
Ruhangisa,
aliingiziwa milioni 404.25 na Mhe. J.A.K Mujulizi
aliingiziwa
shilingi milioni 40.4.
Mheshimiwa
Spika, pia kwa upande wa Watumishi wa umma,
Ndg. Philip
Saliboko ambaye alikuwa mtumishi wa RITA aliingiziwa
shilingi
milioni 40.4, Ndg. Emmanuel Daniel Ole Naiko ambaye
alikuwa
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)
aliingiziwa
shilingi milioni 40.4 na Ndg. Lucy L. Appollo ambaye ni
Mtumishi wa
TRA aliingiziwa shilingi milioni 80.8.
Mheshimiwa
Spika, kwa upande wa Viongozi wa Madhehebu ya
Dini
walioingiziwa fedha na Benki ya Mkombozi ni Askofu 63
Methodius
Kilaini shilingi 80.9, Askofu Eusebius Nzigirwa shilingi
milioni 40.4
na Mchungaji Alphonce Twimann Ye Simon shilingi
milioni
40.4.
Mheshimwa
Spika, Kamati ilithibitishiwa na Mkurugenzi Mkuu
wa TAKUKURU
kuwa baadhi ya watu walienda kugawana fedha
kwenye Benki
tajwa wakiwa na mifuko ya rambo, sandarusi,
mabox,
magunia na lumbesa. Kutokana na muamala uliofanyika
tarehe 6
Februari, 2014 katika Benki ya Mkombozi kiasi cha shilingi
bilioni 3.3
na muamala wa Benki ya Stanbic wa tarehe 23 Januari
2014 ambapo
fedha taslimu (cash) kiasi cha shilingi bilioni 73.5
zilitolewa
na kugawanywa kwa watu mbalimbali kinyume cha
Sheria ya
Benki Kuu na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006. Taarifa
ya benki
(bank statements) yenye majina na akaunti zote
zilizoingiziwa
fedha zimeambatishwa pamoja na taarifa hii
(Kiambatisho
Na. 23).
2.5.4 Ofisi
ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG)64
Mheshimiwa
Spika, Kwa mujibu wa Ibara ya 59(3) ya Katiba ya
Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mwanasheria Mkuu wa Serikali
ndiye
mshauri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya mambo
ya sheria na
anawajibika kutoa ushauri kwa Serikali kuhusu
mambo yote
ya kisheria na ushauri wake ni wa mwisho.
Kamati
imebaini mawasiliano mbalimbali kutoka kwa Katibu Mkuu
wa Wizara ya
Nishati na Madini na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
kwa nyakati
tofauti wakiomba Ushauri kwa Mwanasheria Mkuu wa
Serikali
kuhusiana na njia bora za kushughulikia suala la Akaunti
ya Tegeta
ESCROW. Kwa kuzingatia uchambuzi wa Taarifa ya
Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na mahojiano,
uhusika wa
Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika suala la utoaji
wa fedha za
ESCROW ni kama ifuatavyo:
a) Kuruhusu
ulipwaji wa fedha za Akaunti ya Tegeta
ESCROW kabla
ya kujiridhisha na mgogoro uliokuwepo
kati ya
TANESCO na IPTL
Mheshimiwa
Spika, kufuatia hukumu iliyotolewa na Mheshimiwa
Jaji Utamwa
mnamo tarehe 05 Septemba, 2013 na baada ya 65
kupokea
barua Na. CAC/184/211/01/23 ya tarehe 30 Septemba,
2013 ya
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dr. Servacius Likwelile
akiwasilisha
taarifa ya Wataalam iliyojumuisha Wataalam kutoka
BOT, Wizara
ya Fedha, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na
Wizara ya
Nishati na Madini kuhusu utolewaji wa fedha kwenye
Akaunti ya
Tegeta ESCROW, Mheshimiwa Jaji Fredrick Werema
kupitia
barua Kumb. Na. AGCC/E.80/6/65 ya tarehe 02 Oktoba,
2013
alimuarifu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, kuwa ameipitia
Ripoti ya
wataalamu kuhusu utoaji wa fedha za Akaunti ya Tegeta
ESCROW na
kwa Maoni yake alisema jambo linaloweza kuleta
tatizo
katika utoaji wa fedha hizo ni hati fungani zilizowekezwa na
Benki Kuu.
(Kiambatisho Na. 17).
Mheshimiwa
Spika, inashangaza kuwa bila ya kufanya
uchunguzi wa
kina wa mgogoro wa uhamishaji wa hisa za
Kampuni ya
Mechmar kwenda Piper Links, na kisha kutoka Piper
Links kwenda
PAP, na ilhali akijua fika kuwa kulikuwa na shauri
lililohusu
mgogoro wa capacity charges kwenye Kituo cha
Kimataifa
cha Usuluhishi wa migogoro ya Uwekezaji (ICSID 2),
Mwanasheria
Mkuu badala ya kushauri kupata suluhu ya shauri 66
lililoamuliwa
na ICSID 2 alitumia mamlaka yake kuelekeza fedha za
Akaunti ya
Tegeta ESCROW kutolewa kwenda IPTL.
Mheshimiwa
Spika, ni kwa maelekezo hayo ya mwisho ya
Mwanasheria
Mkuu wa Serikali, Makubaliano ya kutolewa fedha
baina ya
Wizara ya Nishati na Madini na IPTL yaliafikiwa.
b) Kusamehe
Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ya
thamani ya
Shilingi 23 bilioni.
Mheshimiwa
Spika, kuhusiana na suala la Mwanasheria Mkuu
wa Serikali
kusamehe kodi ya Serikali iliyokuwepo katika akaunti
ya Tegeta
ESCROW, Kamati imebaini kwamba mnamo tarehe 18
Novemba,
2013, Mwanasheria Mkuu wa Serikali alimwandikia
Gavana wa
Benki Kuu ya Tanzania barua yenye Kumb. Na.
AGCC/E.080/6/70
akimfahamisha kwamba hapakuwa na kodi ya
Serikali
iliyopaswa kukusanywa kutoka kwenye Akaunti hiyo.
Sehemu ya
barua hiyo inaeleza kama ifuatavyo (Kiambatisho
Na. 18):67
“… hata
hivyo, katika suala hili la ESCROW Account
hakuna kodi
inayotakiwa kukusanywa … kwa sababu
fedha
iliyopelekwa kwenye kwenye Account haikuwa na
VAT
iliyolipwa kwa ajili ya capacity charges”
Mheshimiwa
Spika, kutokana na ukweli huo, Kamati imebaini
kwamba
maelekezo ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa Gavana
wa Benki
Kuu, kuwa hapakuwa na kodi ya Serikali iliyopaswa
kukusanywa
kutoka kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW,
yalimsababisha
Gavana wa Benki Kuu na hivyo kubariki utoaji wa
fedha hizo
kabla ya kukata kodi ya Serikali. Aidha maelekezo hayo
yalikiuka
masharti ya kifungu cha 5(4) cha Sheria ya Kodi ya
Ongezeko la
Thamani ya Mwaka 2006.
Mheshimiwa
Spika, kitendo cha Mwanasheria Mkuu wa Serikali
kutofanya
mawasiliano na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA)
pamoja na
kwamba ana mamlaka ya kutafsiri sheria alipaswa
kujiridhisha
kwamba hapakuwa na kodi iliyopaswa kukatwa kutoka
kwenye fedha
zilizokuwa kwenye Akaunti hiyo. Aidha, angeweza
kujiridhisha
kutoka TANESCO iwapo fedha zilizokuwa zinapelekwa 68
kwenye
Akaunti ya Tegeta ESCROW hazikuwa na kodi ya
ongezeko la
thamani. Kwa kutotimiza wajibu huo Ofisi yake ilifanya
uzembe wa
kutokufanya uchunguzi wa kina wa suala hili (due
diligence)
kabla ya kutoa maelekezo kwa Benki Kuu ya Tanzania.
Mheshimiwa
Spika, maelekezo ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali kwa
Gavana yaliikosesha Serikali kodi ya ongezeko la
thamani
(VAT) kwa kiasi cha shilingi 23,154,003,077.
c) Kutoishauri
ipasavyo BOT, Wizara ya Fedha na Wizara
ya Nishati
na Madini kuhusu kinga kwa Serikali
iliyotolewa
na PAP
Mheshimiwa
Spika, mnamo tarehe 27 Oktoba, 2013, IPTL ilitoa
hati ya
kinga dhidi ya madai yoyote yanayoweza kujitokeza kwa
Serikali na
Benki Kuu kuhusiana na fedha zilizokuwa katika Akaunti
ya Tegeta
ESCROW mara baada ya fedha hizo kulipwa kwa IPTL.
Hati hiyo
ilisainiwa na Bw. Harbinder Singh Sethi Mwenyekiti na
Mtendaji
Mkuu wa IPTL na kushuhudiwa na Ndg. Joseph
Makandege
Katibu na Wakili Mkuu wa Kampuni ya IPTL.69
Mheshimiwa
Spika, kama ilivyobainishwa katika Ukaguzi
Maalumu wa
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, ni
dhahiri kuwa
hisa za Mechmar zilizonunuliwa na PAP kutoka
Kampuni ya
Piper Links ambazo Mahakama Kuu iliziweka chini ya
uangalizi wa
Martha Renju (Receiver) zina mashaka. Hivyo ilikuwa
ni jukumu la
Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na mambo
mengine
kutafsiri vema Hukumu ya Mheshimiwa Jaji Utamwa na
kisha
kufanya uchunguzi wa kina kujiridhisha juu ya uhalali wa PAP
kumiliki
hisa za Piper Links zilizohamishwa kutoka Kampuni ya
Mechmar.
Mheshimiwa
Spika, kutokana na sababu tajwa hapo juu ni
dhahiri kuwa
uhalali wa kinga ya PAP kwa Serikali na BOT kuhusu
hatma ya
utolewaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta ESCROW
una mashaka,
na hivyo kuna uwezekano wa Serikali kushtakiwa na
Mechmar muda
wowote kwa madai kuwa yenyewe haikuuza hisa
zake kwa
Piper Links.
2.5.5 Wizara
ya fedha70
Mheshimiwa
Spika, Wizara ya Fedha ilikuwa ndio mratibu wa
vikao vya
Kamati ya Wataalam ya Serikali iliyokuwa ikishughulikia
suala la
utoaji wa fedha za ESCROW. Uchambuzi wa Kamati
umethibitisha
kuwa kulikuwa na mawasiliano mbali mbali
yaliyokuwa
yakifanywa na Katibu Mkuu Wizara ya fedha Ndg.
Servacius
Likwelile kwenda kwa Gavana wa Benki Kuu na kwa
Katibu Mkuu
wa Wizara ya Nishati na Madini kuhusiana na jambo
hilo.
Mheshimiwa
Spika, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha ndiye
aliyekuwa
kiungo katika kulipatia jawabu suala la utoaji wa fedha
katika
Akaunti ya Tegeta ESCROW. Hilo limejidhihirisha pale
alipopokea
taarifa ya Wataalam na kuiwasilisha kwa Katibu Mkuu
wa Wizara ya
Nishati na Madini na kunakiliwa kwa Gavana wa
Benki Kuu
naMwanasheria Mkuu wa Serikali kwa barua yenye
Kumb.
Na.CAC/184/211/01/23 ya tarehe 30 Septemba, 2013 kwa
maamuzi.
Mheshimiwa
Spika, uhusika wa Wizara ya Fedha hususan Katibu
Mkuu Ndg.
Servacius Likwelile unaishia katika kuwasilisha taarifa 71
ya wataalamu
ambayo baadaye inafanyiwa kazi na Mwanasheria
Mkuu wa
Serikali na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini.
2.5.6 Bw.
Harbinder Singh Sethi
Mheshimiwa
Spika, miongoni mwa wahusika wakuu wa suala
zima la IPTL
hususan Akaunti ya Tegeta ESCROW ni Bw. Harbinder
Singh Sethi,
ambaye anafahamika kama Mwenyekiti na Mtendaji
Mkuu wa IPTL
na wakati huohuo kama Mkurugenzi Mtendaji na
Mmiliki wa
PAP. Uhusika wake unaanzia katika ununuzi wa hisa
saba (7) za
Mechmar kwenda Piper Links Investments na kisha
kutoka Piper
Links Investiments kwenda PAP na hatimaye hisa 3
za VIP
kwenda PAP na hivyo kumpa umiliki wa IPTL na PAP kwa
asilimia mia
moja.
Mheshimiwa
Spika, kama ilivyokwishafafanuliwa hapo awali na
kwa mujibu72
wa matokeo
ya Ukaguzi Maalumu, ni dhahiri kuwa Bw. Harbinder
Singh Sethi
hajawahi kuwasilisha hati halisi za uhamisho wa hisa za
Mechmar
kwenda Piperlinks na kisha PAP. Kwa ushahidi huo ambao
unathibitishwa
na Maelezo ya Maofisa wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania
(TRA) na kwa nyaraka alizopeleka BRELA kwa usajili wa
Kampuni, ni
dhahiri kuwa PAP sio Mmiliki halali wa IPTL na
wamejipatia
fedha za kwenye akaunti ya Tegeta ESCROW kwa njia
ya
udanganyifu.
2.5.7
MSAJILI WA MAKAMPUNI (BRELA)
Mheshimiwa
Spika, uhusika wa BRELA katika suala zima la
utoaji wa
Fedha
katika
Akaunti ya Tegeta ESCROW, unatokana na ushahidi kuwa
Kamati imeshindwa
kuthibitisha kama Hisa za Piper Links toka
Kampuni ya
Mechmar na Hisa za PAP toka Piper Links ziliwahi
kusajiliwa
BRELA kabla Fedha hazijatolewa. Katika uchunguzi wake
Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali alitilia mashaka
mauzo ya
hisa hizo baada ya kupata uthibitisho wa uwepo wa hisa
7 za Mechmar
kutoka kwa Msimamizi Martha Renju. BRELA ilisajili 73
umiliki wa
hisa za PAP kwa IPTL bila kujali matakwa ya Sheria ya
Kodi ya
Mapato kama ilivyofafanuliwa hapo awali.
2.5.8 Wizara
ya Nishati na Madini
Mheshimiwa
Spika, Hadidu ya rejea ya tisa ilimtaka Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za Serikali kuchunguza iwapo Wizara ya
Nishati na
Madini ambayo iliingia Mkataba na IPTL wa kufungua
akaunti
Maalumu ya ESCROW ilifanya uadilifu na kuweka
uangalifu wa
kutosha kabla ya kuingia makubaliano na IPTL ya
kutoa fedha
zilizokuwepo kwenye Akaunti hiyo na kuilipa IPTL.
Mheshimiwa
Spika, Wizara ya Nishati na Madini ilikuwa mmoja
wa washirika
wakati wa ufunguzi na uendeshaji wa Akaunti ya
Tegeta
ESCROW. Aidha, lilikuwa ni jukumu la Wizara hii
kuhakikisha
kuwa Maslahi ya Taifa na TANESCO yanalindwa
ipasavyo
kabla ya kutolewa kwa fedha katika Akaunti husika.
Mheshimiwa
Spika, kwa kuzingatia Taarifa ya Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za Serikali kuhusu Ukaguzi maalumu wa 74
miamala ya
Akaunti ya Tegeta ESCROW, Kamati imebaini
yafuatayo
kuhusu ushiriki na uadilifu wa Wizara ya Nishati na
Madini
katika suala zima la utoaji wa fedha za ESCROW:
a) Viongozi
wa Wizara kutotambua Umiliki wa Fedha za
ESCROW
Mheshimiwa
Spika, kwa mujibu wa Mkataba wa ufunguaji wa
Akaunti ya
Tegeta ESCROW, washirika wawili katika akaunti hiyo
walikuwa ni
Wizara ya Nishati na Madini kwa niaba ya TANESCO
na IPTL na
Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ilikuwa ni Wakala wa
Akaunti
husika kwa ajili ya utunzaji wa fedha na uwekezaji.
Mheshimiwa
Spika, uthibitisho wa matamshi ya Viongozi wa
Wizara ya
Nishati na Madini ya mara kwa mara kuwa umiliki wa
fedha za
ESCROW ni wa watu binafsi yanatia shaka juu ya uadilifu
wao katika
kulinda maslahi ya TANESCO na Taifa katika mgogoro
uliokuwapo
baina ya TANESCO na IPTL.
Kamati
imebani kuwa uongozi wa Wizara kwa namna moja au
nyingine
umefanikisha utoaji wa fedha kwenye akaunti ya 75
ESCROW
Kinyume na kipengele 2.1 cha Mkataba wa ESCROW
ambacho
kinabainisha kuwa washirika wa Akaunti ya Tegeta
ESCROW ni
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Kampuni ya
IPTL na sio vinginevyo, kama kinavyonukuliwa hapo
chini:
“The ESCROW
Agent shall establish and maintain an
account, to
be held in trust for the benefit of
Government
of Tanzania and IPTL, and to be
designated
as the “Tegeta ESCROW Account”
Mheshimiwa
Spika, ni kwa msingi huo hapo juu na kwa
kuzingatia
kuwa Makubaliano ya kufungua Akaunti ya Tegeta
ESCROW
yalibainisha kuwa wadau wa fedha za kwenye akaunti
husika ni
Serikali na IPTL, Wizara ya Nishati na Madini haikutimiza
wajibu wake
ipasavyo ili kuhakikisha haki za TANESCO zinalindwa
kabla ya
utoaji wa fedha husika hasa kwa dhana iliyokuwa
imejengeka
miongoni mwao kuwa fedha hizo ni za wanahisa wa
IPTL na sio
za Serikali au sehemu ya fedha hizo si ya Serikali.76
Mheshimiwa
Spika, Kamati ilipowahoji Mkurugenzi Mkuu wa
TAKUKURU,
Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali
pamoja na Kamishna Mkuu wa TRA walithibitisha kuwa
sehemu ya
fedha zilizokuwemo kwenye Akaunti ya Tegeta
ESCROW
ilikuwa ni ya Serikali kwa maana kwamba kwa vyovyote
vile
palikuwa na fedha za umma katika Akaunti husika.
b) Katibu
Mkuu Wizara ya Nishati na Madini kubadili
msimamo wake
kuhusu umiliki wa Fedha za kwenye
Akaunti ya
Tegeta ESCROW
Mheshimiwa
Spika, mnamo tarehe 16 Septemba, 2013, Katibu
Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini Bw. Eliakim Maswi
alimwandikia
barua Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na
mambo
mengine kuomba ushauri wa kisheria kuhusu Akaunti ya
Tegeta
ESCROW huku akimfahamisha kuwa wamepokea jalada la
hukumu ya
mahakama kuu kuhusu uamuzi wake wa tarehe 05
Septemba,
2013 uliokuwa ukiiondoa IPTL kuwa kwenye ufilisi.77
Mheshimiwa
Spika, katika barua hiyo Katibu Mkuu, Wizara ya
Nishati na
Madini anamfahamisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali
kuwa:
“The ESCROW
Account was established as a
result of
tariff dispute between TANESCO and
IPTL on the
power generated by IPTL, therefore
the
ownership of the money in the ESCROW
Account will
only be established after the tariff
dispute is
resolved…. We are of the opinion that
PAP will be
entitled to the amount which belongs
to the IPTL
after the dispute is resolved and not
the entire
amount in the ESCROW Account”
Mheshimiwa
Spika, pamoja na msimamo huo wa Katibu Mkuu
wa Wizara ya
Nishati na Madini kuwa umiliki wa fedha za ESCROW
au sehemu ya
fedha hizo ni ya Umma, tarehe 20 Septemba, 2013
siku nne
baada ya kuwa na mtizamo kuwa fedha za ESCROW ni za
Umma au
kiasi chake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini
alimjulisha
Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa IPTL Bw. Harbinder 78
Singh Sethi
ambaye pia ni Mmiliki wa PAP kupitia barua yenye
Kumb. Na.
SBD.88/147/01/4 (Kiambatisho Na. 19) kuwa Wizara
haikuwa na
pingamizi dhidi ya kutolewa kwa fedha za ESCROW
kama bwana
Sethi angewasilisha ushahidi wa kuuzwa kwa hisa
asilimia 70
za Mechmar katika IPTL na kutoa kinga kwa Serikali na
TANESCO
baada ya utoaji wa fedha hizo.
Mheshimiwa
Spika, Kamati imepata mashaka makubwa juu ya
sababu
iliyomshawishi Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini
kubadili
msimamo na kuondoa masharti yake ya awali kwa
Mwenyekiti
na Mtendaji Mkuu wa IPTL ndani ya siku nne na
kuamua kuwa
Wizara haioni tena kikwazo cha kuruhusu utoaji wa
fedha ikiwa
ni Kinyume kabisa na mkataba wa ESCROW uliohitaji
kukamilika
kwa mgogoro baina ya TANESCO iliyokuwa ikisimamiwa
na Wizara na
IPTL.
c) Wizara ya
Nishati na Madini kutojiridhisha ipasavyo na
Uhamishaji
wa Hisa za
Mechmar kwenda Piper Links na baadaye
kwenda PAP79
Mheshimiwa
Spika, kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na
Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na kisha
kuthibitishwa
na ushahidi katika mahojiano ya Kamati, imebainika
kuwa kuna
utata mkubwa kuhusu uhamisho wa hisa za Mechmar
kwenda
Piperlink na baadaye kwa PAP. Ushahidi uliopatikana hadi
Akaunti ya
Tegeta ESCROW inafunguliwa ulionyesha kuwa
Mechmar
ilikuwa mmiliki halali wa IPTL (Kiambatisho Na. 3).
Aidha,
uchunguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali
ulibainisha kuwa Mechmar waliuza hisa zao saba kwa Piper
Link
Investment mnamo mwaka 2010 kwa USD milioni 6,
japokuwa
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali alibaini
kuwa hati
halisi ya umiliki wa hisa hizo bado inashikiliwa na Martha
Renju huko
BVI, hii inathibitisha kuwa hapakuwa na uhalali wa
PAP kumiliki
IPTL na kisha kulipwa fedha zilizokuwa kwenye
Akaunti ya
Tegeta ESCROW.
Mheshimiwa
Spika, Kamati iliendelea kubaini kuwa makubaliano
ya uuzwaji
wa hisa za Mechmar kwenda kwa Piper Links
Investment
yamejaa utata mkubwa kutokana na uchunguzi wa
Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kubaini kuwa
watia saini
katika makubaliano husika hawakuainisha majina yao 80
dhidi ya
sahihi walizoweka, hivyo kutoa tafsiri kuwa kuna jambo
lilikuwa
linafichwa kwa makusudi. (Kiambatisho Na. 8).
Mheshimiwa
Spika, ni dhahiri kuwa Wizara ya Nishati na Madini
kupitia kwa
Katibu Mkuu wa Wizara, haikufanya jitihada za
kutosha
kuhakiki mauziano hayo ya hisa kama alivyokuwa
ameomba hapo
awali. Katibu Mkuu, Nishati na Madini Ndg. Eliakim
Maswi
kupokea makubaliano ya uuzaji wa hisa za Piper Links
Investment
kwenda PAP bila kujiridhisha na kufahamu kuwa hisa
hizo
zimeshikiliwa na mtu binafsi inathibitisha mashaka ya Kamati
kuwa Katibu
Mkuu huyo kwa uzembe au kwa makusudi amehusika
katika
kufanikisha utoaji wa fedha za Akaunti ya Tegeta ESCROW
bila
kuzingatia taratibu husika.
Mheshimiwa
Spika, Waziri wa Nishati na Madini ndiyo mamlaka
ya
kuthibitisha uhamishaji wa umiliki wa Kampuni katika sekta
yake. Sheria
ya Kodi ya Mapato Kifungu cha 90 (2) kinaitaka
mamlaka hii
kutotambua uhamisho wa umiliki mpaka kwanza
itakapopatikana
hati ya kodi kutoka TRA. Kamati iliona Wizara
ikiitambua
PAP kwa barua zake tu bila kujali matakwa ya kisheria.81
d) Wizara ya
Nishati na Madini kuingia makubaliano ya
utoaji wa
fedha za ESCROW bila kupata ufumbuzi wa
masuala
yenye utata.
Mheshimiwa
Spika, pamoja na mapungufu yaliokwishaonekana
hapo awali
mnamo tarehe 21 Oktoba, 2013 Katibu Mkuu Wizara ya
Nishati na
Madini Bw. Eliakim Maswi pamoja na Mwanasheria wa
Wizara hiyo
Bi. Salome Makange kwa niaba ya Serikali waliingia
makubaliano
na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa IPTL, Bw.
Harbinder
Singh Sethi na Mwanasheria wa IPTL Bw. Joseph
Makandege
juu ya utoaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta
ESCROW
(Agreement for delivery of funds to Independent Power
Tanzania
Limited (IPTL) (Kiambatisho Na. 10).
Mheshimiwa
Spika, kwa kuzingatia uchunguzi wa Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za Serikali na uchambuzi wa Kamati
ambao
ulibainisha dosari nyingi zilizotakiwa kufanyiwa kazi na
Wizara ya
Nishati na Madini kabla ya kusaini makubaliano ya kutoa
fedha
zilizokuwemo kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW, ni dhahiri
kuwa uharaka
wa mawasiliano kati ya Wizara ya Nishati na Madini
na Kampuni
ya PAP hadi kutolewa kwa fedha yanatia mashaka na 82
ni muhimu
kujiuliza uharaka huo ulisababishwa na jambo gani.
Suala hili
linatia shaka uadilifu wa Viongozi wa Wizara ya Nishati
na Madini
kwa jinsi walivyoshughulikia.
2.6 MADENI
YA IPTL
2.6.1
Uhalali wa Madai ya Benki ya Standard Chartered ya Hong
Kong kwa
IPTL (USD. 125,970,570.57)
Mheshimiwa
Spika, Kamati imebaini kuwa madai ya Benki ya
Standard
Chartered ya Hong Kong kwa IPTL ni halali. Madai hayo
yanatokana
na Benki hiyo kununua deni la IPTL kwa Umoja wa
Mabenki ya
Malaysia (Consortium of Malaysian Banks) Mwezi
Agosti 2005.
Kimsingi baada ya TANESCO kuingia Mkataba wa
kununua
umeme wa IPTL, Kampuni ya IPTL iliingia pia Mkataba na
Umoja huo wa
mabenki tarehe 28 Juni 1997 kwa ajili ya mkopo wa
jumla ya
USD. 105,000,000 ili kuwezesha Ujenzi wa mradi wa
ufuaji wa
umeme uliopo Tegeta. Ingawa, ni kiasi cha USD
85,862,022
tu kati ya USD. 105,000,000 ndicho pekee 83
kilichopokelewa
na IPTL katika ya Mwezi Agosti 1997 hadi
Desemba
1999.
Mheshimiwa
Spika, pamoja na kwamba kumekuwa na mvutano
juu ya
uhalali wa madai ya SCB-HK ikielezwa kuwa matakwa ya
kifungu Na.
79 (1) na Kifungu Na. 172 vya Sheria ya Makampuni
CAP 212
(iliyorekebishwa mwaka 2002) hayakutimizwa kwa IPTL
kutowasilisha
makubaliano yaliyoingiwa kuhusu deni hili na
dhamana
zake26, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
amethibitisha
uhalali wa madai ya SCB-HK kwa kuzingatia
yafuatayo:
a) Uamuzi wa
Shauri Na. ARB/10/20 lililofunguliwa ICSID ulioeleza
kuwa
kutosajiliwa kwa makubaliano yenye maslahi ya dhamana
‘Security
Interest’ haiondoi uhalali wa deni dhidi ya Kampuni
husika.
b) IPTL
ilikuwa ikifanya marejesho hata baada ya deni hilo
kununuliwa
na SCB-HK, ambapo hadi kufikia mwaka 2007
26 Kifungu cha 79(1) cha Sheria hiyo
kinaelekeza kuwa makubaliano yeyote yanayoingiwa na kampuni
iliyosajiliwa
Tanzania yanayogusa maslahi katika mali na biashara zake, yanatakiwa
yawasilishwe pamoja na
nyaraka
zinazoshuhudia kwa Msajili wa Makampuni Tanzania ndani ya Siku 42 baada ya
tarehe ya makubaliano
hayo.84
ilikuwa
imelipa jumla ya USD 58.69 milioni na kati ya hizo USD
20 milioni
zililipwa kwa SCB-HK.
c) Hukumu ya
tarehe 5 Septemba, 2013 ya Mahakama Kuu ya
Tanzania
ilirejesha IPTL kuwa Kampuni hai.
Mheshimiwa
Spika, ikumbukwe kwamba capacity charges
humwezesha
mwekezaji kulipia mtaji wake (Return on Equity) na
kulipia
mkopo. Kati ya mwaka 2002 hadi 2006 TANESCO ilikuwa
inalipa
capacity charges katika kiwango kamili na hivyo IPTL
walipaswa
kuwa wamekamilisha kulipa mikopo yao. Aidha, katika
kipindi
hicho TANESCO iliilipa IPTL ziada ya shilingi bilioni 152
ambazo
zingepaswa kumaliza deni hilo. Hivyo, deni la USD
125,970,570.57
ambalo Standard Chartered Bank Hong Kong
inaidai IPTL
linapaswa kulipwa na Mechmar na siyo TANESCO.
2.6.2
Uhalali wa Madai ya TANESCO kwa IPTL (Sh.
321,041,364,000)
Mheshimiwa
Spika, Kamati imejiridhisha kuwa madai ya
TANESCO kwa
IPTL ni ya msingi na yana uhalali ingawa usahihi 85
wa madai
(kiasi cha deni) hayo utapatikana tu baada ya kufanyika
kwa mambo
yafuatayo;
a)
Kutekelezwa kwa uamuzi uliotolewa na Kituo cha Usuluhishi wa
Migogoro ya
Uwekezaji cha Kimataifa (ICSID) mwezi Februari
2004 (ICSID
2). Aidha, ICSID 2 ilielekeza TANESCO na IPTL
kukokotoa
upya kiwango cha capacity charges.
b) TANESCO
na IPTL kukubaliana kuhusu usahihi wa madai ya
TANESCO
baada ya washirika hao kukubaliana kuhusu kiwango
sahihi cha
Capacity charges.
2.6.3
Uhalali wa madai ya Watsila Tanzania Ltd (USD.
7,730,018.16)
Watsila Netherlands B.V
(USD.11,908,195.70
na GBP. 1,439,836.50 ) kwa IPTL
Mheshimiwa
Spika, Kamati imebaini kuwa Madai ya Watsila
Tanzania Ltd
USD 7,730,018.16 yanayotokana na utekelezaji wa
Mkataba wa
uendeshaji na ukarabati wa Mitambo ya IPTL na
Madai ya
Watsila Netherlands B.V ya USD 11,908,195.70 na Pauni
za
Kiingereza 1,439,836.50 yanayotokana na utekelezaji wa 86
Mkataba wa
Ujenzi wa Mitambo ya IPTL ni madai halali. Aidha,
Kamati imepata
uthibitisho kuwa wadeni hao wawili wanaendelea
kulipwa na
IPTL katika utaratibu waliokubaliana.
2.6.4 Wadai
wa IPTL walioainishwa katika Taarifa ya Mfilisi hadi
kufikia
tarehe 5 Septemba, 2013
Mheshimiwa
Spika, kwa sababu zisizoeleweka Taarifa ya Mfilisi
wa muda
(RITA) iliyotolewa tarehe 5 Septemba, 2013 wakati wa
makabidhiano
ya IPTL kutoka kwake kwenda kwa PAP, madeni
yaliyoorodheshwa
yalikuwa ya USD 14,623,062.02 tu bila
kujumuisha
madai ya Benki ya Standard Chartered ya Hong Kong,
TANESCO,
Watsila Tanzania Ltd na Watsila Netherlands B.V
yaliyoainishwa
hapo juu.
2.6.5
Tahadhari iliyochukuliwa na Serikali dhidi ya Madai
yanayoweza
kujitokeza
Mheshimiwa
Spika, Kamati imebaini kuwa Serikali haikuchukua
tahadhari ya
kutosha dhidi ya madai mengine yanayoweza
kujitokeza
kabla ya kutolewa kwa fedha katika Akaunti ya Tegeta 87
ESCROW.
Licha ya kwamba IPTL kupitia barua Na. IPTL/GEN/010-
2013 ya
tarehe 28 Oktoba, 2013 (Kiambatisho Na. 20)
iliwasilisha
kinga yake kwa Serikali na Benki Kuu dhidi ya madai
yanayoweza
kujitokeza.
Mheshimiwa
Spika, Serikali ilitakiwa kujiridhisha kuhusu uhalali
wa PAP
kumiliki IPTL na hivyo uhalali wa kinga inayotolewa na
IPTL
ikizingatiwa kwamba kwa mujibu wa Kamishna Mkuu wa TRA
na
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU mchakato wa Piper Links
kununua hisa
za Mechmar na kisha PAP kununua hisa za Piper
Links
haukuwa halali na TAKUKURU wanaendelea na uchunguzi
zaidi kuhusu
mauziano ya hisa husika. Kwa sababu hizo, Kamati
ina wasiwasi
na uhalali wa kinga hiyo suala ambalo linaweza
kusababisha
hasara kwa Serikali endapo Mechmar itathibitisha
kutouza hisa
zake kwa kuwa bado zinashikiliwa na mtu binafsi.
2.7 HATUA
ZILIZOCHUKULIWA BAADA YA UAMUZI WA
MAHAKAMA KUU
Mheshimiwa
Spika, Kamati haikuridhishwa na jinsi Serikali
ilivyotafsiri
hukumu ya Mahakama Kuu ya Tanzania chini ya Mhe. 88
Jaji J.H.K
Utamwa iliyotolewa tarehe 5 Septemba 2013 ambayo
ikielekeza
utekelezaji wa masuala yote matano (5) kama
yalivyoombwa
na VIP Engineering & Marketing (Kiambatisho Na.
21).
Mheshimiwa
Spika, Hukumu husika ilihusu utatuaji wa mgogoro
wa wanahisa
ambapo, pamoja na mambo mengine ilimuamuru
Mfilisi wa
muda kukabidhi mali zote za IPTL, ikiwa ni pamoja na
mtambo wa
kuzalisha umeme kwa Kampuni ya PAP ambayo
ilidhamiria
kuwalipa wadai wote halali wa IPTL na kuongeza uwezo
wa mtambo
hadi kufikia MW 500 na kuuza umeme kwa TANESCO
kwa bei ya
kati ya USD 0.6 hadi 0.8 kwa uniti moja ya umeme.
Mheshimiwa
Spika, hukumu hii haikuhalalisha PAP kulipwa
fedha
zilizokuwa kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW kwa sababu
fedha hizo
ziliwekwa chini ya makubaliano kati ya Serikali na IPTL
kutokana na
madai kuwa TANESCO wamekuwa wakitozwa
capacity
charges kubwa. Hivyo, utoaji wa fedha hizo ungefanyika
tu kama
TANESCO na IPTL wangepata suluhisho la mgogoro huo
na kisha kwa
pamoja kusaini hati ya makubaliano na kuomba
kutolewa kwa
fedha hizo wakionyesha kiasi ambacho kinatakiwa 89
kulipwa kwa
mshirika anayestahili kulipwa (Kiambatisho Na. 3).
Hivyo, kwa
Serikali kutumia hukumu hiyo ya Mahakama kama
kigezo
mahsusi cha kutoa fedha kwenye Akaunti ya Tegeta
ESCROW
haikuwa sahihi.
Mheshimiwa
Spika, Kamati haikuridhishwa pia na jinsi Serikali
ilivyojipanga
kutekeleza uamuzi huo wa mahakama ikizingatiwa
kuwa uamuzi
huo unaitaka IPTL kuongeza uzalishaji wa umeme
kufikia
megawati 500 wakati Mkataba wa kununua umeme (PPA)
baina ya
TANESCO na IPTL wa mwaka 1995 ulikuwa wa uzalishaji
wa megawati
100 tu. Serikali hadi sasa haijapitia na kujadili upya
utekelezaji
wa Mkataba husika hivyo kuna hatari ya Serikali kupitia
TANESCO
kuingia katika migogoro mipya.
Mheshimiwa
Spika, Kamati ilishangazwa kuona kwamba katika
hali isiyo
ya kawaida, Mahakama katika Shauri hilo tajwa ilikwenda
mbali zaidi
hadi kupanga kiwango cha bei ya umeme kuwa USD
0.6 hadi 0.8
kwa uniti moja ya umeme, ikizingatiwa kuwa bei ya
umeme
hupangwa katika mkataba wa mauziano ya umeme au
mwenendo wa
soko.90
3.0 MAONI NA
MAPENDEKEZO YA KAMATI
3.1 MAONI YA
KAMATI
Mheshimiwa
Spika, baada ya kupitia hadidu rejea kumi
zilizochambuliwa
hapo juu na kuzipatia majibu yote kwa mujibu wa
Taarifa ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu
ukaguzi
maalum katika akaunti ya Tegeta ESCROW, Kamati
inapaswa
kutoa mapendekezo ya njia sahihi za kisheria zinazoweza
kutumika kwa
ajili ya kulinda Serikali isipate hasara tena katika
utekelezaji
wa Mkataba wa Uzalishaji umeme kati ya TANESCO na
IPTL.
Vilevile Kamati inatoa mapendekezo juu ya hatua stahiki
ambazo
zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya wahusika kulingana na
matokeo ya
ukaguzi maalumu. 91
Mheshimiwa
Spika, Kamati imethibitisha bila chembe ya
mashaka
kwamba mchakato mzima wa kutoa fedha katika akaunti
ya Tegeta
ESCROW uligubikwa na mchezo mchafu na haramu
wenye harufu
ya kifisadi ulioambatana na udanganyifu wa hali ya
juu ambao
kwa kufuata sheria tu ungeweza kugundulika na
kuzuiwa.
Hata hivyo, Mheshimiwa Spika, mfumo mzima wa Serikali
ni kama
ulipata ganzi au uliganzishwa ili kuwezesha zaidi ya
shilingi
bilioni 306 kuporwa kutoka Benki Kuu ya Tanzania na
kutakatishwa
kupitia Benki mbili hapa Nchini na baadhi ya mabenki
ughaibuni.
Mheshimiwa
Spika, Kamati imethibitisha kuwa hukumu ya Jaji
Utamwa ya
kukabidhi masuala yote ya IPTL kwa Kampuni ya PAP,
ilitafsiriwa
vibaya kwanza na Bwana Harbinder Singh Sethi
mwenyewe na
baadaye ikatafsiriwa vibaya pia na viongozi wa
Wizara ya
Nishati na Madini, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na
hata baadhi
ya viongozi wakuu wa Serikali akiwemo Mheshimiwa
Waziri Mkuu.
Tafsiri hii potofu ilirudiwa rudiwa na kuimbwa na
viongozi wa
Wizara kiasi cha kuliaminisha Bunge na Umma
kwamba ndio
ilikuwa tafsiri sahihi. Baada ya kupata ushahidi usio
na mashaka
kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za 92
Serikali na
Mamlaka ya Mapato Tanzania, ni dhahiri Kampuni ya
PAP haikuwa
na uhalali wowote wa umiliki wa IPTL wakati inalipwa
fedha za
kutoka Akaunti ya Tegeta ESCROW.
Mamlaka ya
Mapato Tanzania kupitia uchunguzi wake imebaini
kukiukwa kwa
Sheria ya Kodi ya Mapato Sura ya 333, kifungu cha
90 (2) kama
ilivyofanyiwa marekebisho na sheria ya Fedha, sheria
namba 8 ya
mwaka 2012 kuhusiana na mabadiliko ya umiliki wa
hisa kutoka
Kampuni moja kwenda nyingine zilizoko nje ya
Tanzania na
zenye mali hapa Tanzania. Vile vile uchunguzi
umeonyesha
ukwepaji mkubwa wa kodi uliotokana na kuwasilisha
nyaraka za
kughushi kulikofanywa na mawakala wa Kampuni ya
PAP ambapo
hata kama wangekuwa wamefuata sheria hiyo hapo
juu bado
wangekuwa wamesababisha ukwepaji kodi wa shilingi
8.7 bilioni.
Mheshimiwa
Spika, mnamo tarehe 19 mwezi Novemba 2014,
Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania alimwandikia
barua
Msajili wa Makampuni (BRELA) akionesha kusudio la
kuondoa
uhalali wa hati za malipo ya kodi ya ongezeko la mtaji
(capital
gains tax certificates) zilizolipwa kuthibitisha mauzo ya hisa 93
za Mechmar
kwenda Piperlink na baadaye PAP akitoa siku 6. Barua
hiii
iliwasilishwa mbele ya Kamati. Hivi sasa tunavyowasilisha
taarifa hii
siku sita zilikamilika jana bila Kampuni ya PAP kuchukua
hatua zozote
za kufanya malipo halisi na halali kama Kamishna
Mkuu wa
Mamlaka ya Mapato alivyoelekeza.
Mheshimiwa
Spika, CAG amebainisha pia kuwa Bwana
Harbinder
Singh Sethi hana hati halisi ya hisa za Kampuni ya
Mechmar
katika IPTL maana zilizuiwa na Mahakama ya British
Virgin
Island. Hivyo Kamati inaitaka Serikali kwenda mahakamani
kuomba
mapitio ya hukumu ya Jaji Utamwa, J na kwa kutumia
ushahidi huu
ili kuirejesha IPTL katika hali iliyokuwa awali.
Mheshimiwa
Spika, Kamati pia imeridhika kuwa Mkataba wa
IPTL
uligubikwa na tuhuma za ufisadi toka kuanza kwake, tuhuma
ambazo mara
kadhaa zimethibitishwa na maafisa waandamizi wa
Serikali na
hata Baraza la Kimataifa la Usuluhishi wa Migogoro ya
Uwekezaji
(ICSID 1) kupelekea kushusha gharama za uwekezaji
wa mitambo
hiyo. Mkataba huu pia umekuwa ukikiukwa mara kwa
mara bila
kujali (impunity) ikiwemo kukosekana kwa Kamati ya
pamoja ya
uendeshaji kama ilivyoonyeshwa katika taarifa ya CAG. 94
Kamati
inaitaka Serikali, kwa mujibu wa Sheria na kwa kutumia
mkataba wa
mauziano umeme kati yake na IPTL, kuuchukua
mtambo huu
na kuumilikisha kwa Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO).
Mheshimiwa
Spika, Kamati inakubaliana na Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa
Hesabu za Serikali kwamba Benki ya Standard Chartered
ilikuwa na
madai yake katika IPTL kufuatia kunununua deni
lililotolewa
kwa IPTL na mabenki ya Nchini Malaysia. Vile vile
Kamati
imethibitisha kuwa mkopo uliotolewa ni wa thamani ya
Dola za
kimarekani 105 milioni, lakini zilizotumika kwa ajili ya
mradi huu ni
Dola za kimarekani 85 milioni tu. Hata hivyo, Kamati
inapenda
kulifahamisha Bunge lako tukufu, kama
tulivyokwishasema
huko awali, kwamba kupitia malipo ya ‘capacity
charges’
kati ya mwaka 2002 – 2006 ambapo TANESCO ililipa
ziada ya
shilingi 152 bilioni, deni hili lilipaswa kuwa limelipwa.
Ikumbukwe
kuwa ‘capacity charges’ ni malipo ya mtaji na mkopo
na sio
malipo ya huduma ya umeme ulionunuliwa. Kwa maana hii
Benki ya
SCB-HK haipaswi kuwa na madai yeyote yale dhidi ya
Serikali ya
Tanzania au TANESCO wala haki ya dhamana ya 95
Serikali kwa
IPTL. Kwa kuwa Kamati inapendekeza kuchukuliwa
kisheria kwa
Kampuni ya IPTL na kuimilikisha kwa Shirika la
TANESCO,
Serikali ielekezwe kwanza kuchunguza malipo ya
‘capacity
charges’ yaliyolipwa kati ya mwaka 2002 – 2006 kama
yalihudumia
mkopo kabla ya makubaliano yeyote na Benki ya SCB
– HK ili
kukwepa kulipa mkopo huo mara mbili.
Mheshimiwa
Spika, Kamati imethibitisha kuwa Bwana Harbinder
Singh Sethi
kwa makusudi na kwa lengo la kujitwalia fedha
alifanya
udanganyifu, kuwasilisha nyaraka za kughushi za umiliki
wa hisa 70%
za Kampuni ya Mechmar katika Kampuni ya IPTL
kwenda
Kampuni ya PiperLink iliyopo ‘offshore’ na kisha kwenda
Kampuni
anayomiliki ya PAP. Vile vile Bwana huyu alifanya ujanja
kwa
kushirikiana na viongozi waandamizi wa Serikali, maafisa wa
BRELA na
maafisa wa ngazi ya chini wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania na
hivyo kufanikiwa kuchota fedha asizostahili jumla ya
shilingi 306
bilioni kutoka Benki Kuu ya Tanzania. Fedha hizo
ziliwekwa
katika akaunti nambari 9120000125294 ya Kampuni ya
PAP iliyopo
Benki ya Stanbic, jijini Dar es Salaam, akaunti ambayo
ilifunguliwa
tarehe 28 Novemba 2013 kwa kazi maalumu na kisha
kufungwa
tarehe 16 Septemba, 2014. Kamati imeridhika kuwa 96
Bwana
Harbinder Singh Seth alikiuka Sheria za kodi, alijipatia mali
asiyostahili
na hivyo kuhujumu uchumi wa Nchi yetu na
alitakatisha
fedha haramu kwa kuzitumia kununua hisa 30% ya
Kampuni ya
VIP inayomilikiwa na Bwana James Rugemalira kwa
thamani ya
dola za kimarekani 75 milioni.
3.2 Kamati
inapendekeza kama ifuatavyo: -
3.2.1
Mheshimiwa Spika, Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa
(TAKUKURU)
na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) mara moja
wachukue
hatua ya kumkamata Bwana Harbinder Singh Sethi na
kumfikisha
mahakamani kwa makosa ya Anti money laundering,
ukwepaji
kodi na wizi. Kamati pia inaelekeza Serikali kutumia
sheria za
Nchi, ikiwemo sheria ya ‘Proceeds of Crime Act’
kuhakikisha
kuwa Bwana Harbinder Singh Sethi anarejesha fedha
zote
alizochota kutoka Benki Kuu ya Tanzania. Kwa kuwa suala hili
ni suala la
utakatishaji wa fedha haramu, Mamlaka ziwasiliane na
mamlaka za
Nchi nyingine kuhakikisha mali za Bwana huyu
zinakamatwa
na kufidia fedha hizo.97
3.2.2
Mheshimiwa Spika, Kamati imethibitsha kuwa Bwana James
Rugemalira
aliuza hisa ambazo Kampuni yake ya VIP inamiliki
katika IPTL
na kulipwa na Bwana Sethi kutoka katika Fedha za
Akaunti ya
Tegeta ESCROW. Kamati imethibitisha kuwa fedha
kutoka
akaunti za Kampuni ya PAP katika Benki ya Stanbic
zilizofunguliwa
maalumu kwa ajili ya kupokea fedha kutoka
Akaunti ya
Tegeta ESCROW iliyokuwa Benki Kuu zilipelekwa katika
Akaunti
nambari 00151002368801 na Akaunti nambari
00151002368802
za Kampuni ya VIP ziliyopo Mkombozi
Commercial
Bank.
Kwa mujibu
wa Taarifa ya CAG na kuthibitishwa na Mkurugenzi
Mkuu wa
TAKUKURU fedha hizo pia ziligawiwa kwa watu
mbalimbali
binafsi. Kamati haina tatizo na watu wawili kuuziana
makampuni
yao kwa thamani wajuazo wenyewe, au jinsi ya
kuzitumia
fedha zao, ama kuwachagulia watu wa kuwagawia,
lakini
Kamati imejidhihirishia kuwa fedha iliyotumika kulipia
manunuzi
hayo ni fedha ambayo sehemu yake ni ya umma
iliyochotwa
bila huruma wala aibu, kutoka Benki Kuu. Hivyo,
Kamati
inazitaka mamlaka za uchunguzi kuhakikisha kuwa fedha
hizo
zinarudi Benki Kuu hata ikibidi kwa kufilisi mali za watu wote 98
waliofaidika
na fedha hizo kwa thamani ya fedha walizopewa na
Bwana
Rugemalira.
Mheshimiwa
Spika, baadhi ya waliofaidika na fedha hizo ni
Viongozi wa
Umma ambao wanapaswa kuzingatia Sheria ya
Maadili ya
Viongozi wa Umma (Sheria namba 13 ya Mwaka 1995)
ambayo
inawataka kutoa taarifa ya zawadi wanazopokea au
malipo
wanayolipwa. Vyombo vya uchunguzi vifanye uchunguzi
kutambua
kama walifuata matakwa ya sheria na hatua mahsusi
zichukuliwe,
ikiwemo kuvuliwa nyadhifa zao zote za kuchaguliwa
na/au
kuteuliwa, kufilisiwa mali zao na kushtakiwa mahakamani
kwa mujibu
wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
ibara ya 132
(1) – (6).
3.2.3
Mheshimiwa Spika, Kamati pia imethibitisha kwamba fedha
zilizolipwa
kwa Watu binafsi zilitokana na Akaunti ya Tegeta
ESCROW
zilizolipwa kwa PAP ambayo si mmiliki halali wa IPTL.
Kwa maana
hiyo fedha hizo zilitolewa kwa watu hao kama rushwa
na
kuzitakatisha fedha hizo haramu. Aidha, kamati inapendekeza
kwamba
Akaunti zote zilizohusika na miamala hii haramu ya
Akaunti ya
Tegeta ESCROW, akaunti zao zifungwe (freeze) na 99
wenye
akaunti hizo walazimishwe kurejesha fedha hizo kwa
mujibu wa
Sheria (Anti Money Laundering) ikiwa ni pamoja na mali
zao
kufilisiwa. Kwa upande wa viongozi wa Kisiasa wawajibike na
Watumishi wa
umma wafukuzwe kazi.
3.2.4
Mheshimiwa Spika, Kamati imejiridhisha kwamba, suala la
akaunti ya
Escrow ni jambo la utakatishaji wa fedha (Money
Laundering),
kama alivyosema Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU
katika
mahojiano yake na Kamati. Kamati inazitaka mamlaka
zinazohusika,
ikiwemo Benki Kuu kuzitangaza benki za Stanbic na
Mkombozi
Commercial Bank kama asasi za utakatishaji fedha
(Institutions
of Money Laundering Concern).
3.2.5
Mheshimiwa Spika, Aidha, Kamati inalikumbusha Bunge lako
tukufu
pendekezo muhimu lililotolewa na Kamati Teule ya
Mheshimiwa
Dkt. Harrison Mwakyembe kuhusu sakata la maarufu
la Richmond.
Kamati ilipendekeza:
“Mkataba
kati ya TANESCO NA Richmond Development
Company LLC
na sasa Dowans Holdings S.A. kama ilivyo
mikataba
kati ya TANESCO na IPTL, SONGAS, AGGREKO 100
na Aistom
Power Rentals inatoa unafuu usiostahili kwa
makampuni
hayo ya umeme na kuiumiza TANESCO na
hatimaye
watumiaji na walipa kodi kimapato, k.m.
mikataba
hiyo kuwa na vipengele vya kuibana TANESCO
kuyalipa
makampuni hayo kodi zinazohusika na
uendeshaji
(operations) matengenezo/marekebisho ya
mara kwa
mara ya mitambo (maintenance) gharama za
bima, ada za
mawakili na washauri elekezi (consultants)
gharama za
mafuta na gesi ya kuendeshea mitambo,
gharama za
ukodishaji mitambo (capacity charges)
ambazo
TANESCO hulipa kila mwezi si chini ya wastani
wa shilingi
bilioni 2 kwa kila kampuni, izalishe au
isizalishe
umeme. Kamati Teule inatoa rai kwa Serikali
kuwa
mikataba yote hii ipitiwe upya mapema
iwezekanavyo
kama ambavo mikataba ya madini
knavyopitiwa
upya sasa na Serikali. Bila kufanya hivyo,
mzigo mkubwa
wa gharama za umeme utawaelemea
wananchi na
kushindwa kufikia azma ya Serikali ya
maisha bora
kwa kila Mtanzania.”101
Mheshimiwa
Spika, Kamati inapendekeza kwamba, azimio hili
litekelezwe
kwa kupitia upya mikataba yote ya umeme ambayo
inalitafuna
Taifa letu.
3.2.6
Mheshimiwa Spika, Kamati imejiridhisha kuwa Bodi ya Shirika la
Ugavi wa
Umeme Nchini (TANESCO) bila sababu zozote za msingi
ilikataa
mapendekezo ya Menejimenti ya Shirika ya kutoruhusu
uchotwaji wa
fedha kutoka Benki Kuu akaunti ya Tegeta ESCROW
na hivyo
kusababisha kulikosesha Shirika fedha zake inazohitaji
sana
kutokana na hali mbaya ya Shirika. Ikumbukwe kuwa Shirika
la TANESCO
lilipata hasara ya shilingi bilioni 467.7 katika mwaka
wa fedha
unaoishia Desemba 31, 2013. Hasara hiyo imekuwa
ikiongezeka
mwaka hata mwaka toka mwaka 2010 (bilioni 5),
2011
(bilioni 43), 2012 (bilioni 177) na hivyo hadi kufikia Desemba
31, 2013,
jumla yote kuu ya hasara (accumulated loss) ilikuwa
imefikia
shilingi trilioni 1.45.
Kamati pia
imethibitisha kuwa Bodi ya TANESCO mpaka sasa
haijatekeleza
hukumu ya ICSID 2 na kukokotoa upya viwango vya
malipo ya
‘capacity charges’ na hivyo kupelekea TANESCO na
Serikali
kuendelea kuilipa IPTL/PAP kila mwezi shilingi Bilioni 4.5 102
($2.6m kila
mwezi) izalishe au isizalishe umeme. Kamati inaitaka
Serikali
kuvunja mara moja Bodi ya TANESCO na TAKUKURU
iwafungulie
mashtaka ya matumizi mabaya ya ofisi wajumbe wote
waliohusika
kupitisha maamuzi hayo ya kifisadi, ili iwe fundisho
kwa wajumbe
wengine wa bodi za Mashirika ya Umma kwamba
watahukumiwa
kwa maamuzi mabovu wanayoyafanya.
3.2.7
Mheshimiwa Spika, Kamati imethibitisha kuwa Katibu Mkuu wa
Wizara ya
Nishati na Madini aliingia makubaliano ya kutoa fedha
katika
Akaunti ya Tegeta ESCROW bila kujiridhisha kikamilifu kuwa
maamuzi ya
hukumu ya ICSID 2 yalikuwa bado kutolewa na hivyo
kusababisha
fedha kutolewa bila kukokotoa upya gharama za
‘capacity
charges’, jambo ambalo limesababisha kupoteza fedha za
umma.
Vile vile,
Kamati imebaini kuwa, Katibu Mkuu hakufanya uchunguzi
wa kina (due
diligence) kujiridhisha uhalali wa Kampuni ya
Mechmar
kuuzwa kwa Piperlink na baadaye kuuzwa kwa PAP, na
hivyo
kusababisha fedha za akaunti ya Tegeta ESCROW kulipwa
kwa
asiyestahili na kinyume cha Mkataba wa akaunti ya Escrow.
Kwa maana
hiyo, Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, 103
pengine kwa
uzembe wake ama kwa kukusudia kwa sababu
anazozijua
yeye mwenyewe zaidi, amesaidia uchotwaji na
hatimaye
utakatishaji wa fedha haramu.
Mheshimiwa
Spika, Kamati pia imethibitisha uzembe wa hali ya
juu
uliofanywa na Katibu Mkuu huyo, kushindwa kujiridhisha kama
masharti ya
Sheria ya kodi ya Mapato Sura ya 333, Kifungu cha
90(2)
yalitekelezwa. Kifungu hicho kimsingi kinaitaka mamlaka ya
‘approval’’
ya uhamishaji wa Makampuni kutotambua Kampuni
mpaka kwanza
kodi za uhamishaji ziwe zimelipwa na hati za
malipo ya
kodi zimetolewa na mamlaka ya kodi.
Mheshimiwa
Spika, Kamati inapendekeza kuwa uteuzi wa Katibu
Mkuu huyu
utenguliwe, na TAKUKURU wamfikishe mahakamani
mara moja,
kwa kuikosesha Serikali Mapato, matumizi mabaya ya
ofisi na
kusaidia utakatishaji wa fedha haramu.
3.2.8
Mheshimiwa Spika, Kamati imethibitisha kuwa Naibu Waziri wa
Nishati na
Madini alisema uongo Bungeni kwa kutamka kauli
ambazo
zilizokuwa na lengo la kupotosha umma kuhusu akaunti ya
Tegeta
ESCROW ikiwemo kutoa kauli ambazo zingeweza 104
kusababisha
Nchi kuingia kwenye mgogoro wa kidiplomasia na
nchi ya
Uingereza.
Kamati
inapendekeza kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini
(Madini)
achukuliwe hatua kali za kinidhamu ikiwemo kutenguliwa
uteuzi wake.
Kamati pia inapendekeza kuwa Naibu Waziri huyu
afikishwe
mbele ya Kamati ya Bunge ya Maadili ili aadhibiwe kama
Mbunge kwa
kusema uwongo Bungeni ili liwe fundisho kwa
wabunge
wengine kuhusiana na kauli wanazotoa ndani ya Bunge
lako tukufu.
3.2.9
Mheshimiwa Spika, Kamati imethibitisha kuwa Waziri wa Nishati
na Madini
amekuwa, mara kwa mara, akilipotosha Bunge lako
tukufu na
Taifa kwa ujumla kuhusiana na Fedha za Akaunti ya
Tegeta
ESCROW kwamba ndani ya fedha hizo hakukuwa na fedha
za umma.
Mheshimiwa
Spika, hata mtu wa kawaida angeweza kujua
kwamba
washirika wa ‘Tegeta Escrow Account’ ni akina nani na
masharti ya
kutoka kwa fedha hizo kwenye akaunti ni yapi kwa
mujibu wa
Mkataba wa uendeshaji wa akaunti hiyo. 105
Hata hivyo,
katika hali ya kushangaza, aidha kwa makusudi ama
kwa sababu
anazozijua vizuri zaidi mwenyewe, Waziri wa Nishati
ananukuliwa
kwenye kumbukumbu rasmi za Bunge, Kwa nguvu
kubwa na kwa
kujiamini, akitetea uchotwaji wa fedha hizo
kinyume na
masharti ya Mkataba wa Escrow.
Aidha,
Kamati imebaini kuwa Waziri wa Nishati na Madini ndiye
alikuwa
dalali mkuu aliyewakutanisha Bwana Harbinder Singh Sethi
na Bwana
James Rugemalira, tena katika ofisi ya Umma; na
pengine hii
ndiyo iliyokuwa sababu ya upotoshaji huu. Waziri wa
Nishati na
Madini alifanya udalali huo akijua dhahiri kuwa Bwana
Sethi hana
uhalali wa kisheria kufanya biashara kwa jina la IPTL.
Iwapo Waziri
wa Nishati na Madini angetimiza wajibu wake
ipasavyo,
Fedha za Tegeta ESCROW zisingelipwa kwa watu
wasiohusika,
na Nchi ingeweza kuokoa mabilioni yaliyopotea kama
kodi za VAT,
Capital Gain Tax na Ushuru wa Stempu ambazo ni
sawa na
takribani shilingi bilioni 30. 106
Mheshimiwa
Spika, Kamati inapendekeza kuwa Mamlaka yake
ya uteuzi
itengue uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini kutokana
sababu hizo
zilizoelezwa.
3.2.10
Mheshimiwa Spika, Kutokana na kukua na hivi sasa
kukomaa kwa
vitendo haramu vya wizi wa fedha ama mali za
umma na
kukua ama kukomaa kwa vitendo vya rushwa kubwa na
uhujumu
uchumi, inapendekezwa kwamba Bunge lako Tukufu
liridhie
kuitaka Serikali kuanzisha kitengo maalumu cha
kushughulikia
rushwa kubwa (grand corruption) kitakachokuwa na
nguvu ya
kuendesha mashtaka kwa uhuru kamili, na kwamba
Bunge lako
Tukufu liridhie kuanzishwa kwa Mahakama Maalum ya
kushughulikia
Rushwa kubwa itakayoshughulikia kesi za rushwa
zitakazokuwa
zikipelekwa kwake na kitengo maalum cha
kushughulikia
rushwa kubwa.
3.2.11
Mheshimiwa Spika, Kamati imethibitisha kuwa
Mwanasheria
Mkuu wa Serikali alitoa ushauri ulioipotosha Benki
Kuu ya
Tanzania kuhusiana na hukumu ya Jaji Utamwa J. Kwa
kutumia
madaraka yake vibaya, Mwanasheria Mkuu wa Serikali
aliagiza
kodi ya Serikali yenye thamani ya shilingi 21 bilioni isilipwe 107
na hivyo
kuikosesha Serikali mapato adhimu. Mwanasheria Mkuu
wa Serikali
kwa kujua na kwa makusudi alilipotosha Bunge na
Taifa kwamba
mgogoro uliopelekea kufunguliwa kwa Akaunti ya
ESCROW
ulikuwa ni mgogoro wa Wanahisa wa IPTL badala ya
mgogoro kati
ya TANESCO na IPTL. Kamati inapendekeza kuwa
uteuzi wa
Mwanasheria Mkuu wa Serikali utenguliwe mara moja na
kisha
afikishwe mahakamani kwa matumizi mabaya ya Ofisi
yaliyopelekea
Serikali kupoteza mabilioni ya fedha.
3.2.12
Mheshimiwa Spika, Kwa upande wa Waziri Mkuu
kuhusiana na
suala hili, Kamati iliipitia kwa umakini Katiba ya
Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 iliyoainisha
Kazi na
Mamlaka ya Waziri Mkuu na kubaini kuwa, kwa mujibu wa
Ibara ya 52
(1):
“Waziri Mkuu
atakuwa na madaraka juu ya udhibiti,
usimamiaji,
utekelezaji wa siku hata siku wa kazi na
shughuli za
Serikali ya Jamhuri ya Muungano.”
Na, Ibara ya
52 (2), inayosema; 108
“Waziri Mkuu
atakuwa kiongozi wa shughuli za Serikali
Bungeni.”
Kisha Kamati
ikajiuliza maswali kadhaa. Kwa mfano katika kutaka
kubaini
ukweli na kujiridhisha Kamati ilijiuliza maswali yafuatayo
kuhusu
Waziri Mkuu:
(a) Je,
Waziri Mkuu alikuwa anajua sakata la utoaji wa
fedha katika
Akaunti ya Tegeta ESCROW?
(b) Je,
Waziri Mkuu alitimiza wajibu wake kwa mujibu wa
Ibara ya 52(1)?
(c) Je,
Waziri Mkuu wakati akitoa matamshi yake Bungeni
alikuwa
akitimiza wajibu wake kwa mujibu wa Ibara ya
52 (2)?
(d) Je, nini
maana, uzito na ukweli wa matamshi ya mara
kwa mara ya
Waziri Mkuu ndani na nje ya Bunge
kuhusiana na
suala hili?
(e) Je, Waziri
Mkuu alitoa maamuzi au maelekezo yoyote
ya kuzuia
jambo hili lisifanyike?109
Mheshimiwa
Spika, Baada ya kupitia vielelezo vilivyomo kwenye
ripoti ya
CAG, Kamati imejiridhisha pasipo mashaka kuwa, Waziri
Mkuu,
alikuwa ana taarifa zote kuhusiana na mchakato mzima wa
kuchotwa
fedha kutoka katika akaunti ya ESCROW.
Ushahidi
ulioletwa na ofisi ya CAG kwenye Kamati unaonyesha
kuwa Waziri
Mkuu alikuwa akipata taarifa za jambo hili. Na Kamati
imesikitishwa
kuona kuwa Waziri Mkuu hakuchukua hatua zozote
kuzuia
muamala huu usifanyike.
Mheshimiwa
Spika, Kamati, kwa kuzingatia kielelezo namba 22,
inathibitisha
bila shaka kwamba, Waziri Mkuu alikuwa analijua
jambo hili
vizuri na kwamba aliridhia muamala huu ufanyike. Ndiyo
maana katika
maelezo yake ya Bungeni mara kadhaa Waziri Mkuu
alithibitisha
kuwa fedha za Escrow hazikuwa fedha za Umma.
Mheshimiwa
Spika, Mwalimu Julius Nyerere katika kitabu chake
cha Uongozi
Wetu na Hatma ya Tanzania aliandika:
“…kubadili
Waziri Mkuu sio jambo la ajabu. Ndugu
Rashid
Mfaume Kawawa alikuwa Waziri Mkuu wangu 110
kwa muda
mrefu. Hakuwa amefanya kosa lolote; lakini
nilitaka
kumbadili na kuteua Waziri Mkuu mwingine.
Nilimwita,
nikamwambia hivyo. Tukakaa pamoja mimi
na yeye,
tukashauriana na kukubaliana nani anafaa
kushika
nafasi yake. Nikamteua Hayati Edward Moringe
Sokoine.
Najua kuwa watu wa aina ya Rashidi Kawawa
ni adimu
sana Duniani, hawazaliwi kila siku; hata hivyo
ni jambo la
kushangaza kidogo kwamba viongozi wetu
wa Mageuzi,
hata bado hatujafa, wanaona kuwa ni
kosa kuwakumbusha
kuwa vyeo walivyonavyo ni
dhamana.
Wanadhani kuwa Uwaziri ni Usultani;
ukishakuwa
Sultani utakufa sultani! Nadhani
wanakosea.
Nchi hii imewahi kung’oa Masultani wa kila
aina.
Tukianza kuvumilia Masultani wa kuchaguliwa,
tutapanda
mbegu ya Masultani wa kuzaliwa. Narudia;
kumbadili
Waziri Mkuu sio jambo la ajabu. Anaweza
kujiuzulu,
anaweza kufukuzwa Nchi isitikisike. Lakini
huwezi
kumtimua Rais wa Nchi bila kuitikisa Nchi
yenyewe. Ni
vizuri jambo hili likatamkwa waziwazi na
likaeleweka
sawasawa. Maana watu wengine
wananong’ona
nong’ona kuwajibika kwa Rais kana 111
kwamba ni
jambo la mchezo mchezo tu. Kulazimika
kumchukulia
hatua Rais wa nchi ni mkasa na balaa kwa
Nchi yeyote
ile.”
Mwisho wa
kunukuu.
Mheshimiwa
Spika, ni dhahiri kwamba viongozi wenye mamlaka
makubwa
wanapaswa kila wakati kukumbuka kauli ya muasisi wa
Mapinduzi ya
Zanzibar na Muasisi wa Muungano, Sheikh Thabit
Kombo,
ambaye alikuwa akipenda kusema ‘weka akiba ya
maneno’.
Ni wazi
kwamba maneno ya Waziri Mkuu hapa Bungeni
yaliuaminisha
umma kuwa fedha zile siyo fedha za umma kiasi
kwamba
gazeti la Serikali la Daily News la tarehe 1 mwezi Mei,
2014,
likachapisha habari yenye kichwa kikubwa cha habari ‘IPTL
clean Deal –
Pinda’. Na ofisi ya Waziri Mkuu haikukanusha.
Mheshimiwa
Spika, ni jambo la kushangaza kuona kwamba,
jambo kubwa
na zito kama hili lingeweza kufanyika bila ya
mamlaka za
juu, hususan Mhe. Waziri Mkuu kufahamu. 112
Mheshimiwa
Spika, kwa uzito na unyeti wa jambo hili, kwa
vyovyote
vile, Waziri Mkuu anapaswa kuwajibika kwa kauli zake na
kwa
kutokutekeleza wajibu wake wa kikatiba ipasavyo, ili
kurejesha
imani ya wananchi kwa serikali yao na viongozi wao wa
kisiasa.
3.0
HITIMISHO
Mhesimiwa
Spika, napenda kukushukuru sana kwa kuiamini
Kamati yetu
kwa kuikabidhi jukumu hili nyeti. Nakuhakikishia
kwamba kazi
hii imetekelezwa kwa haki iliyojengwa katika msingi
wa Taarifa
ya Ukaguzi Maalum wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa
Hesabu za Serikali, na vyanzo vingine muhimu
vikijumuisha
maelezo ya Ofisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU)
na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA).
Mheshimiwa
Spika, Kamati inatoa shukrani za dhati kwa vyombo
vya habari
kwa kuwapasha habari Watanzania kuhusiana na suala
hili. Kwa
namna ya pekee kabisa Kamati inalipongeza gazeti la
The Citizen
kwa msimamo wake thabiti bila kujali vitisho.113
Mheshimiwa
Spika, Kamati yetu inayo imani na Bunge Lako
Tukufu
kwamba litaitumia Taarifa hii ipasavyo katika kutekeleza
Wajibu wake
wa kuisimamia na kuishauri Serikali itekeleze wajibu
wake katika
misingi ya haki, uadilifu, uzalendo, usawa, uwazi na
uwajibikaji.
Tunawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge wote
kwani katika
kipindi chote cha kuandika Taarifa hii mlitutia moyo
kwa kuonesha
dhahiri kwamba mnaihitaji Taarifa yetu ijadiliwe
Bungeni.
Mheshimiwa
Spika, naomba pia kuishukuru Ofisi ya Spika kwa
maelekezo
thabiti ya namna ya kutekeleza jukumu hili.
Naomba pia
kumshukuru Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas D.
Kashillilah
na Wajumbe wa Sekretarieti yake kwa ushauri makini
katika
kipindi chote ambacho Kamati ilikuwa ikitekeleza jukumu
hili.
Kipekee nawashukuru pia Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za
Serikali, Ndg. Francis Mwakapalila, Mkurugenzi
Mkuu wa
Ofisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Dkt. Edward
Hoseah na
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini, Bw.
Rished Bade
kwa ushirikiano walioipatia Kamati.114
Mwisho,
nawashukuru Watumishi wote wa Bunge na vyombo
vingine vya
kiusalama vilivyohusika katika kuisaidia Kamati
kutekeleza
jukumu lake.
Mheshimiwa
Spika, naomba Bunge lako tukufu lipokee Taarifa
hii,
lijadili na kupitisha mapendekezo yote tuliyoyatoa kuwasilisha.
Mheshimiwa
Spika, naomba kutoa hoja.
Zitto Zuberi
Kabwe, Mb.
MWENYEKITI
KAMATI YA
BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI (PAC)
26 NOVEMBA,
2014.
Post a Comment
Post a Comment