Diwani kata ya Mshewe Fabian Mwakasole
Mtendaji wa kijiji cha Njelenje Emanuel Kalimoja akiwa katika chumba ambacho imehifadhiwa mipira ya maji
Tabibu wa Zahanati ya Njelenje Allen Mboma akimsafisha kidonda mgonjwa wake katika zahanati hiyo
Tenk la maji lililotegwa katika shule ya msingi Njelenje kwaajili ya kufuna maji wakati wa mvua
Esau kilunda mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya msingi Njelenje akiwa ofisini kwake
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Njelenje wakitoka kuchota maji kwaajili ya matumizi ya hapo shuleni.
Wakazi wa kijiji cha Njelenje kata ya Mshewe wilaya ya
mbeya vijijini wameilalamikia serikali kwa kutowawekea miundombinu ya maji
inayopelekea kukosekana kwa maji safi na salama kwa zaidi ya miaka kumi na
mbili.
Wakizungumza na Mtandao huu wakazi hao wasema ni zaidi
ya miaka kumi na mbili sasa kijiji chao kimekuwa na tatizo la maji licha ya
kuzunguza na viongozi wao katika mikutano ya hadhara pasipo mafanikio.
Wakazi hao wamesema kutokana na hali hiyo wanalazimika
kwenda kuchota maji katika makorongo ambapo maji hayo hayajathibitishwa
kitaalamu hivyo kuwapelekea wakati mwingine kusumbuliwa na matumbo.
Aidha wamesema wanalazimika kutembea umbalia wa zaidi
ya kilometa kumi ilikufika katika makorongo hayo ya maji hivyo kwa mwendo wa
kwenda na kurudi ni zaidi ya kilometa 30 wanazotembea katika kutafuta maji na
wakati mwingine wamekuwa wakienda katika makorongo hayo wakikosa maji kutokana
na watu kuwa wengi wakifuata maji hayo.
Kwaupande wake Diwani wa kata hiyo Fabian Mwakasole
amekiri kuwepo kwa tatizo hilo kwa zaidi ya miaka kumi na mbili na kusema kuwa
yeye tatizo hilo alishalifikisha katika halmashauri ya wilaya hiyo lakini mpaka
sasa hakuna utekelezaji licha ya Rais Kikwete kutoa ahadi ya kupeleka maji
katika kata hiyo mwaka 2010 alipotembelea katika kata hiyo.
Mwakisole amesema hatua inayosubiriwa kwa sasa ni
bajeti ya mwaka 2014/2015 ambapo serikali imetenga Tsh, Mil. Mia saba kumi na
tano kwaajili ya mradi wa maji kutoka kijiji cha mshewe kupitia Njelenje mpaka
Mjele hivyo wanasubiri utekelezaji wake.
Amesema siku za nyuma kulikuwa na maradi wa maji
ulikuwa ukitokea mshewe mpaka njelenje lakini watu ambao siowaaminifu kutoka
kijiji jirani cha muvwa walikatakata mabomaba kwa lengo la kupeleka maji katika
mashamba yao ili kumwagilia mashamaba hayo.
Kufuatia hali hiyo tenki lililojengwa njelenje ambalo
lilikuwa likitumika kwasasa halina maji kwa muda mrefu sasa.
Hata hivyo Mganga mkuu wa zahanati ya njelenje Allan
Mboma amesema tatizo la maji limekuwa kubwa mpaka kupelekea kushindwa kutoa
huduma stahiki kwa wagonjwa wanaofika katika zahanati hiyo kwa lengo la
kupatiwa matibabu hasa kinamama wajawazito wanaofija kujifungua maana katika
huduma ya uzalishaji maji hutumika kwa wingi sana tofauti na vyumba vingine.
Lumemo blog ilibahatika kukutana na mganga huyo
akimuhudumia mgongonjwa mwenye tatizo la kidonda ambapo maji aliokuwa akitumia
si sahii na nihaba kupita kiasi.
Hata hivyo blog hii ililazimika kufika katika shule ya
msingi Njelenje ambako ni moja kati ya sehemu yenye uhitaji wa maji kwaajili ya
shughuli mbali mbali shuleni hapo na kuonana na mwalimu mkuu msaidizi ambapo
mwalimu huyo amesema tatizo hilo ni kubwa hivyo hawaelewi hatima yake ni nini
na kuiomba serikali kulitilia mkazo katika kulipatia ufumbuzi wake.
Na, Lumemo blog
Post a Comment
Post a Comment