Mkufunzi wa mafunzo Laurence Chuma akitoa maelekezo kwa washiriki kabla ya kunza mafuinzo.
Mratibu wa mafunzo Alphonce Stima aliyeshika karatasi akitoa maelekezo jinsi washiriki watakavyopatiwa mafunzo.
Baadhi ya washiriki wakisikiliza maelekezo jinsi mafunzo yatakavyoendeshwa
...................................................
Mtandao wa jinsia
Tanzania Gender Networking Programme (TGNP) unaendesha mafunzo ya utawala bora kwa viongozi wa vijiji, kata na wilaya mkoani mbeya yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kiuongozi kwa viongozi walioko madarakani.
Mafunzo hayo anaendeshwa katika
ukumbi wa Cofe Gorden uliyopo maeneo ya sokoine jijini mbeya ambapo yameanzi
leo na yanatarajia chukua muda wa siku tano.
Akizungumza na Highlands fm katika mafunzo hayo muwakilishi wa mtandao
huo Alphonce Stima amesema lenglo la mafunzo hayo ni kuwaimarisha watendaji wa
serikali na jamii kwa ujumla…
Aidha Stima mafunzo hayo
yamegawanyika katika makundi mawili ambapo siku mbili za mwanzo zitawahusisha
watendaji wa kata, madiwani na wakurugenzi wa Halmashauri na siku zinazofuatia
watashirikishwa washiriki mbali mbali wa ngazi za jamii.
Hata hivyo baadhi ya washiriki wa
mafunzo hayo wakiwemo madiwani kutoka katika kata za ijombe, mshewe na tembela
wamesema wanatarajia kunufaika na mafunzo hao licha ya kuwepo madarakani kwa
muda mrefu pia wanapata uwezo mkubwa wa kiutendaji.
Na, Lumemo blog
Post a Comment
Post a Comment