Muwezeshaji wa mafunzo ya ufuatiliaji wa rasilimali za umma Lawrence Chuma
Inaelezwa kuwa chanzo cha
baadhi ya viongozi wa umma kutokuwa na uhusiano mzuri na wanachi wao vijijini
na kujiona ni miungu watu na kuzikalia taarifa za mapato na
matumizi ni ukosefu wa ‘utawala bora’ na kutopevuka kwa demokrasia miongoni
mwao.
Mtandao wa jinsia
Tanzania Gender Networking Programme (TGNP) umetoa mafunzo katika
ukumbi wa Coffee Garden Jijini Mbeya, kwa baadhi ya wananchi
kupitia vituo vya taarifa na maarifa kutoka Kata za Tembela,Mshewe na
Ijombe wakiwemo na wanahabari ili kuwajengea uwezo na ufahamu wa haki zao
katika ufuatiliaji hali inayowasabaisha kupaza sauti zao
kwa watendaji kuacha kuwachukulia kama wapinga maendeleo pindi
wanapofuatilia taarifa za miradi yao.
Sarah Jailos ni ni mmoja kati ya washiriki wa mafunzo
hayo ambeye pia ni Mwenyekiti wa kituo cha taarifa na maarifa cha Twigushe
,Kata ya Ijombe mkoani Mbeya kumekuwa na changamoto kati yao na viongozi
wao pindi wanapotaka kupata taarifa ya miradi yao, viongo hao wamekuwa
wakiwaita ni wapinga maendeleo.
Aidha, Sabina Mwalyego ambaye ni Mwenyekiti wa
kituo cha taarifa na maarifa Kata ya Mshewe amesema changamoto kubwa alioipata
ni baada ya Serikali kuwapatia fedha zaidi ya sh,mil. 31 kwaajili ya kujenga
nyumba tatu za walimu ambapo mkuu wa shule hiyo alijenga nyumba moja yenye
thamani ya sh, mli.5 badala ya nyumba
tatu kama ilivyokusudiwa ndipo wao kama viongozi wa kituo cha taarifa na
maarifa walilazimika kufuatilia kwa ukaribu ili kubaini ubadhirifu aliyoufanya
mkuu huyo.
TGNP ilianza kutoa mafunzo ya dhana
ya utawala bora na suala la bajeti kwa watumishi wa halmashauri ya
wilaya ya Mbeya vijijini,madiwani,wanahabari na watendaji wa kata na
vijiji na hatimaye kwa wananchi kupitia vituo vya taarifa na
maarifa ambavyo vinafanya kazi na mtandao huo wa kijamii tangu september 16
mwaka huu, lengo likiwa kushirikishana na kujifunza umuhimu
wa kufuatilia matumizi na rasilimali za umma ili kuboresha
uwajibikaji,utawala bora katika ngazi hizo.
Mwisho.
Na, Lumemo blog
Post a Comment
Post a Comment