Mratibu wa mafunzo hayo kutoka TGNP Alphonce Stima akifanya maandalizi ya mafunzo.
Afisa mtendaji wa kijiji cha Ilota kata ya mshewe Maclaud Mwasanjingu akisoma mrejesho wa mafunzo ya siku ya kwanza.
Muwezeshaji wa mafunzo Lawrence Chuma akifanya maandalizi ya mafunzo.
Washiriki wa mafunzo wakiwa darasani wakimsikiliza muwezeshaji wakati mafunzo yakiendelea ukumbini.
Washiriki wakiwa katika foleni ya chakula cha mchana baada ya mafunzo.
Washiriki wakiwa katika picha ya Pamoja mara baada ya kufunga mafunzo
WATUMISHI wa Halmashauri, ya Wilaya ya Mbeya
vijijini,watendaji na wanahabari wametoa wito kwa serikali kupanga bajeti
halisia iliyoibuliwa na wananchi itakayokidhi mahitaji na usimamizi mzuri
wa rasilimali ili iweze kunufaisha jamii ya watanzania walio wengi
badala ya kunufaisha wachache.
Wito huo umetolewa na washiriki wa
mafunzo ya utawala bora na bajeti, yaliyoandaliwa na mtandao wa jinsia Tanzania
Gender Networking
Programme (TGNP) yaliyofanyika katika ukumbi wa Coffee Gardan uliyopo eneo la Sokoine
jijini Mbeya, ambapo wamesema kuwa endapo serikali itazingatia
matakwa ya miradi iliyoibuliwa na wananchi malalamiko hayatakuwepo na imani kwa
serikali itaongezeka.
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya vijijini
wakizungumza na Blog hii kwa nyakati tofauti wametoa maoni
yao kwamba nivema serikali ikapanga bajeti inayolingana na mapato yaliyopo
Afisa mtendaji wa Kijiji cha Njelenje Kata ya
Mshewe Emanuael Kalimoja ameshauri jamii ianze kujenga utamaduni wa
kupanga bajeti kuanzia ngazi ya familia huku Afisa elimu shule za
msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Wende Mbilinyi amesema tatizo kubwa
viongozi wa serikali wanapanga bajeti bila kuweka vipaumbele vya kuangalia matumizi
na mapato yanayopatikana.
Kwa upande wake mshauri elekezi wa mafunzo
hayo, Lawrence Chuma akizungumza mara baada ya kuhitimisha mafunzo hayo kwa
awamu ya kwanza amesema changamoto zilizopo katika kufikia dhana ya utawala
bora ni kutokana na baadhi ya viongozi kutokubali wananchi wanapotaka kuhoji
maswali ili kujua mustabali wa miradi ya maendeleo yao.
Na, Lumemo blog
Post a Comment
Post a Comment